Tahadhari: Kama una majini usijifukize na nyungu

son of a teacher

JF-Expert Member
Jul 30, 2017
515
1,364
Majuma kadhaa nyuma Mh Rais na waziri wa tamisemi walishauri wananchi kujifukiza na nyungu kama kinga yacovid 19 lakini walisahau jambo moja tu kuwa miongoni mwa wananchi kuna wenye mashetani na maruhani.

Nyungu ni kiboko ya wachawi na majini na hii nina ushahidi nao kuna ndugu yetu alitupiwa mashetani na ilifikia hatua akipandisha mashetani anakuwa mtata na anakuwa na nguvu za ajabu na wakati mwili wake mdogo na hata siku 3 hali chakula ndipo alipoletwa mganga na kutengeneza nyungu na tulimkamata jamaa yetu tena tukiwa 7 mijibaba yenye nguvu na kumfukiza nyungu

Asikuambie mtu dogo (shetani) maana sauti ilikuwa tofauti na ya dogo alikuwa anatetemeka kwa hofu na kuanza kuomba msamaha hatorudia tena kusumbua na tukaweka nae mkataba deal amruhusu kijana ale na hapohapo alikubali haraka nk nk

Tahadhari kwa wenye majini usijifukize na nyungu utapandisha bure

NB:nyumba yenye nyungu mchawi,jini haingii harufu inamkereketa san

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema wenye mashetani wasitumie nyungu, wakati huo unadai Kijana wenu Mwenye mashetani alisaidiwa na nyungu. Huyo shetani anaogopa mvuke wa majani, anazuga tuu, halafu shetani ni mwongo, eti mliingia nae mkataba, badala kumfukuza atoke.

Usiruhusu Kijana wako kuwa jumba la mapepo, majini n.k Fukuza, tumia jina walilopewa wanadamu kufukuzia mashetani, linajulikana.
 
Jina la Yesu.
 
Njia hiyo ni ya shetani kabisa, ninashangaa tulikataa kuipigia magoti corona tukamkimbilia Mungu kwa maombi, mwisho tukamaliza kuipigia magoti corona kwa njia ya nyungu, na hapo ndipo penye ukubwa wa akili za shetani, unamkataa na kumpinga huku kule anakugeuza kwa kukujia na sura nyingine na kukupiga ngwara.
 
Sijui lakini contents kwa maana ya mimea inayotumika huenda ni tofauti na ya mzee kalumanzila 😃😃😃
 
Jambo hili huna uelewa nalo na umekariri kutokana na kisa kimoja, nyungu zipo za aina tatu kwa ujumla wake...kuna nyungu safi, nyungu chafu na nyungu tiba.

Nyungu safi hii hupendwa sana na majini na unapojifukiza ndiyo unawatawalisha na kuwafurahisha zaidi na hutumika kwenye kuwapunga majini nk.

Nyungu ya pili ni nyungu chafu ambayo hii hutumika kuwafukuza majini mwilini mwa binadamu na nyungu ya tatu ni nyungu tiba, ambayo hii hutumika kutibu kama dawa nyingine na si lazima ihusiane na ushirikina.

Tofauti ya nyungu hizi ni kubwa sana, nyungu safi hutumia miti mbali mbali ya kunukia ambayo ni maalum na pia kuna upangaji wake na taratibu zake ndani ya sufuria, nyungu chafu hujumlisha madawa yanayokera harufu yake na yenye nguvu maalum ya kumpa kero jini, na hii pia ni kwa taratibu maalum.

Nyungu tiba haina taratibu zozote maalum wala manuwizi ila tu ni vile unavyoelewa miti fulani ikichanganywa ni dawa basi unatumia kama tiba nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema wenye mashetani wasitumie nyungu, wakati huo unadai Kijana wenu Mwenye mashetani alisaidiwa na nyungu. Huyo shetani anaogopa mvuke wa majani, anazuga tuu, halafu shetani ni mwongo, eti mliingia nae mkataba, badala kumfukuza atoke.

Usiruhusu Kijana wako kuwa jumba la mapepo, majini n.k Fukuza, tumia jina walilopewa wanadamu kufukuzia mashetani, linajulikana.
Ni kwa JINA LA YESU KRISTO pekee majini, marhani, mapepo, mashetani, nk hutii na kwa Jina hili kila goti litapigwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom