Tahadhari: Figisufigusu na vitendo vingine vya kihuni vinaweza kuanza wakati wa kampeni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
Napenda kuwaasa makamanda wote kuwa hawa mabwana wanaweza kutufanyia figisufigisu na vitendo vingine vya kihuni kama vile kukamata makamanda watakaokuwa wanawapigia kampeni wagombea wetu na hata wagombea wenyewe wanaweza kukamatwa au kuwa harassed kwa njia moja au nyingine.

Kwa makusudi mabwana hawa wanaweza kutumia lugha chafu na za kuudhi au hata kuchochea wafuasi wao watufanyie fujo ili na sisi tukijubu basi wapate sababu za kutukamata hivyo tuwe makini na lugha zetu wakati wa kampeni na hata tukichokozwa makini namna ya ku-react.

Jambo lingine muhimu ni kuwaandaa wapiga kura kisaikolojia wakati wa kampeni juu ya uwezekano wa kumwagwa kwa idadi kubwa ya wavaa sare na magari yao vituoni siku ya tukio kwa lengo la kuwatisha hivyo waambieni mapema kuwa hali hiyo ikitokea isiwatishe bali wajitokeze kwa wingi.

Cha msingi zaidi mjitahidi kukusanya ushahidi wa vitendo vya kihuni siku ya tukio ili mpate ushahidi wa kupeleka mahakamani maana kunaweza kukawa na fitina nje ya uwanja(wakati wa kampeni) na fitina ndani ya uwanja(vituoni siku ya tukio).

Ikiwezekana pia mumuombe Nassari awape vile vifaa vyake vya kurekodia au mtafute vingine vya aina hiyo ili mvitumie kuchukulia matukio siku hiyo.

Najua ushahidi huo wa picha unaweza kukataliwa mahakamani ili cha msingi hapa ni baadae kuja kusambaza ushahidi huo kwa wananchi ili mnapolalamika muwe na ushahidi wa picha regardless ushahidi huo utakubaliwa mahakamani au laa.

Tutambue tu hawa mabwana wameshaharibu na hawakubaliki mbinguni wala duniani hivyo hawaoni hatari kufanya lolote kwa masilahi yao maana wameshakata tamaa..
 
Ukiona kampeni zimeenda salama ujue vyama serious vya upinzani havikushiriki....

Ukiona Polisi wanaingilia kati ujue vyama serious (Ukawa) vimeshiriki!

Yaani sasa hivi huwezi ukatofautisha kati ya Polisi na UVCCM!
 
Ukiona kampeni zimeenda salama ujue vyama serious vya upinzani havikushiriki....

Ukiona Polisi wanaingilia kati ujue vyama serious (Ukawa) vimeshiriki!

Yaani sasa hivi huwezi ukatofautisha kati ya Polisi na UVCCM!

Siasa za nchi hii hivi sasa zimeharibiwa na shithole brains zilizoshika nafasi nyeti za maamuzi.
 
Mbona mnaanza kulialia...huyo mpemba hakubaliki kuanzia dole, mwembe kiwete wala mchamba wima na bado mnamleta kino ambapo wenzenu CUF wamesimamisha.. i think ur decision is a shithole
 
Back
Top Bottom