Tahadhari: CHADEMA kazi ya kukiimarisha chama si lelemama,waacheni wanaojinadi kuhusu urais wajinadi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malumbano ama yana kuzwa kwa makusudi na vyombo vya habari au ni mkakati maalumu wa kuvuruga umaoja na mshikamano uliopo ndani ya CHADEMA.Mbinu hizo zinazo jaribu kutumiwa na wafuasi wenu ilihali muda na wakati wa kujinadi haujafika ni gelesha ambayo mkiingia mkenge mtasababisha malumbano yasiyo na tija na kuwaacha maadui zenu wakipeta pasi na sababu. Pia niwakumbushe kuwa rais ajaye waamuzi ni sisi Watanzania,cha msingi chama kupitia viongozi wake wajipange kimkakati kuboresha msingi na matawi nchi nzima na kuwa karibu na Watanzania ili kujua matatizo ya Watanzania nini,hata kama wakishika dola wajue wanaanzia wapi.

Wananchi wamechoshwa na kauli ambazo zinaonekana kuwa na mashiko kuliko hata matatizo yenyewe yanayo wakabili.Kuitwa mheshimiwa au kutoitwa hakuleta muamko wa kutatua matatizo yanayo wakabili Watanzania.

Mapesa yametoroshwa nje ya nchi,waliokwiba pesa za EPA wanapeta mtaani,nchi inaendelea kuwa omba omba kwa kuwa tu kodi za walalahoi zinagawanywa kwa walafi wachache. Kwa kuwa wana Watanzania wamewaweka mioyoni mwao kiimani na kimatendo basi fursa hii si ya kuipoteza kwani WAtanzania wana tarajia mengi tokan kwenu wakiamini CHADEMA ni pambazuko jipya lenye nia ya kumkomboa Mtanzania huyu.

Muda wa kurumbana haupo hivi sasa,hatuhitaji kuambiwa serikali imefanyia nini,sisi si vipofu hatuoni tunataka kuona na si kusikia. CHADEMA mkumbuke kuwa,Watanzania wamechoka kweli kweli na si masihara,kuchoshwa huku ni zaidi ya miaka hamsini hivyo basi tunaamini Tanzania ya kweli si ya maneno matupu kwani haki siku zote huenda na wajibu,hatuwezi kwenda kushoto tu,kushoto lazima kuwe na kulia hapo ndipo mwendo ukamilika.
 
Back
Top Bottom