Tahadhari:cancer ya jino, hospital ya muhimbili

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
Ndugu wana JF wenzangu wasalam,
Baada ya salamu napenda kuelezea kisa cha hivi karibuni kilichotokea cha mama mmoja kupoteza maisha baada ya kupata kansa ya jino iliyotokana na uzembe wa madaktari wa muhimbili.

Kabla ya kupata kansa hiyo na hatimaye kufikiwa na mauti hayo mama huyo aliende hospitali pale muhimbili ili kupata matibabu ya jino lake baada ya kuona maumivu ya jino yakiongezeka siku hadi siku, baada ya Dr. Kumcheki aligundua jino lake limetoboka hivyo alipendekeza kuliziba kwa risasi na kupewa dawa ya kupunguza maumivu . Lakini pamoja na kupata matibabu hayo bado alipata maumivu makali siku hadi siku na kila anaporudi pale muhimbili hupewa dawa za kutuliza maumivu na dawa zinapo kwisha hali hurudia palepale. Baada ya kuhangaika sana, mtu mmoja alimuelekeza aende kwa Dr. Mmoja ana clinic ya meno pale kariakoo, mara tu Dr alipomchunguza aligundua risasi ile aliyowekewa kwenye jino imegusa fizi, ndipo dr alipotaka kujua ni wapi aliwekewa risasi ile yule mama aliposema ni muhimbili basi dr huyo alimpigia simu dr mkuu wa kitengo cha meno ambeye wanafahamia na kumueleza kilichotokea kwa mama mama yule haraka dr huyo wa muhimbili alimwambia ahakishe anaondoa na kusafisha risasi iliyoko kwenye jino kirha kumpeleka pale muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Ndipo ilipogundulika risarh aliyoekewa imesababishia kansa ya jino hali iliyomfadhaisha sana yule mama na kufanya azimie baada ya kupata tarifa hiyo

Ilibidi aende ocean road cancer institute ili kuanza matibabu haraka lakini tunasikitika kabla hajaanza matibabu mauti ilimkuta hivyo kuaga dunia.

Ilisemekana Dr. Aliyemuekea risasi ile ili kuziba tundu kwenye jino alikuwa ni mwanafunzi, hivyo natoa tahadhari kwa wale wote watakaopenda kupata matibabu muhimbili hasa ya jino kuwa makini sana .
 
Tuthibitishie kuwa hiyo risasi ndio ilisababisha kansa,..au alikuwa nayo kabla?usiropoke tu kijana uwe na adabu wewe,..
 
Pole kwa wafiwa na roho ya marehemu Mungu ailaze mahali pema peponi. Nafikiri njia pekee ya kujua sababu ya kifo ni kufanya uchunguzi wa kina(post mortem) ambao utatoa sababu hasa ya kifo. Ninaweza kuliweka hili sawa kwa mfano ufuatao;Jana kuna babu alifariki baada ya kuanguka akiendesha baiskeli na kuvunjika mguu. Ndugu waliamini hvyo,lakn madaktari wakawa na mashaka juu ya sababu ya kifo. Ilibidi post mortem ifanyike,na ikagundulika kwamba tayari huyu mzee alikuwa na kansa ambayo imeshasambaa(metastasis) na hyo ndiyo sababu ya kifo. Uchunguzi ni lazima kuondoa utata kama huo wa huyo mama.
 
Hamna kitu sensitiv kama jino. Nawasihi usithubutu kumpa Dr bomu achezee meno yako, bora uingie gharama au uwe kibogoyo.


Mbona bongo hali inatisha, kawaida Daktari mwanafunzi haruhusiwi kufanya ishu kubwa kama hizi. Kuna siku Dr mwanafunzi atachiwa afanye upasuaji.
 
Duh kama chanzo ni hayo matibabu ya jino...kazi tunayo maana dr vijana wengi ndiyo wanaofanya hizo kazi.
 
Dah, kuna kipindi wakati nipo sekondari fulani mitaa ile walikuja kuomba wanafunzi wakatuchunguze meno.
Sijui walikuwa wanatufanya nini maana hadi leo nahisi meno yangu hayapo sawa.
Tuweni makini jamani.
 
Maskini mama wa wa2 alikufa kabla babu wa loliondo hajaoteshwa!!! Si angekuwa amepona!!!
 
Tuthibitishie kuwa hiyo risasi ndio ilisababisha kansa,..au alikuwa nayo kabla?usiropoke tu kijana uwe na adabu wewe,..

ulitaka niweke vyeti vya uchunguzi hapa? Au ulitaka ushahidi gani? Na niushauri 2 nimetoa ukiuwamini au usipoamini ni juu yako.
 
Hayo yote yawezekana. Siku moja nami nilienda pale kupata Matibabu ya Meno si unajua sasa nimeng'oa Jino la 11 sasa. Nilipofika pale nilitanguliwa na mama mmoja wa makamo akaniambia anakuja kung'oa jino ambalo limemsumbua sana kutoka na maumivu na ukizingatia aliweka Risasi miaka ya 1975 sasa anaona ang'oe alipofika alinitangulia mimi Dr. Akamwita alipoingia ndani mi sijui kilivyo endelea mara tulizuiliwa kuingia kwanza baada ya Dk 45. Naona mhudumu wa Mochwari anakuja anabeba mwili wa marehemu kwenye kifaaa maalum cha kubebea kama kitanda na kuondoka nae tulipouliza tuliambiwa uongozi upo kwenye kikao kutokana na ishu hiyo, Sasa nikajiuliza Maswali Kulikoni??? lakini nichogundua yule mama alikuwa na Low Presha na alimwambia Dr. lakini kutokana na wingi wa watu na yeye Dr. anataka kujifunza akamwambia sio tatizo wewe njoo. Hii Story ya kweli miaka 7 iliyopita sasa
 
Dah, kuna kipindi wakati nipo sekondari fulani mitaa ile walikuja kuomba wanafunzi wakatuchunguze meno.
Sijui walikuwa wanatufanya nini maana hadi leo nahisi meno yangu hayapo sawa.
Tuweni makini jamani.
HACHA HIZO WEWE HIYO ILIKUWA NI SDS (SHOOL DENTAL SERVICES) huwa hakuna oral sugeries zinazofanyika hapo,zaid ya examination. Sasa kinachofanya meno yako kutokuwa sawa na nn?
 
nikuamini kwa porojo,.leta takwimu inayosema hivyo,..[eti risasi iliyowekwa na mwanafunzi imesababisha kansa]wewe,...risasi ni GRAPHITE,..sasa sema ilikuwa ni risasi kweli au unatumia lugha ya porojo?niamini nini ?unatoa ushauri kwa kitu usichokijua?koma kabisa
 
Hamna kitu sensitiv kama jino. Nawasihi usithubutu kumpa Dr bomu achezee meno yako, bora uingie gharama au uwe kibogoyo.

Mbona bongo hali inatisha, kawaida Daktari mwanafunzi haruhusiwi kufanya ishu kubwa kama hizi. Kuna siku Dr mwanafunzi atachiwa afanye upasuaji.

Huwa wanapasua pia! Labda tu kama haujafika pale kwa upasuaji. Niliuliza nikaambiwa watajuaje kama hawatompasua mtu kikwelikweli?. Ila dokta bingwa anatakiwa awe jirani akiwaelekeza!
 
Back
Top Bottom