SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

Jurudyiza

Member
Jul 15, 2021
70
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Pole sana mkuu, umenikumbusha jamaa yangu aliniambia kwamba amemaliza TSH 5,000,000/= Ila alivyopata ajira akanieleza kwamba anaenda kutafuta mtaji wa FX akiwin ajira ndio basi ila namuona huu ni mwaka wa tano na anayobidii ya kazi sijui kama kweli bado mawazo anayo ya kuiacha kazi hiyo.
Milioni 5 za demo naamanisha Sina haraka na hela.
Nikishajua hela zitakuja tu.
Stick on process mane it's take care yenyewe
 
Milioni 5 za demo naamanisha Sina haraka na hela.
Nikishajua hela zitakuja tu.
Stick on process mane it's take care yenyewe
Hapo sawa, sasa ukitaka kujua uchawi upo kaweke real hata kama ulikuwa na mafanikio kwenye demo utashangaa kila kitu kinagoma
 
"usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu."

Hii ndo point.
Sahihi, wengi wanaingia bila elimu na huishia kulia
 
Nakumbuka kuna mdogo angu flan hv yupo IFM pale ndo alikuwa kila wiki tukionana mara Forex mara Bitcoin bas nikamuangalia na kumsikiliza mwisho nikamwambia bro mi MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE hayo mambo yenu vijana mi siamini kabisa hivyo vitu. Even though I am around early 20's hii ni kama warning sign kwangu

Nikamuona hayuko Pleased na jibu langu bas nikamwambia kama wewe unaamin Take risk then gain advantage! Ila usisahau Shortcut is a wrong cut!
Bas akachukua Take risk then gain advantage! But haikujibu iliyotoa majibu ilikuwa Shortcut is a wrong cut!

So sad kila nikikumbuka alipoteza kama tsh 500k na maisha ya chuo yalivyo nilimhurumia kweli nikamsaidia nusu hasara 250k tokea siku hiyo ameomba kad ya kujiunga na BARAZA LA WAZEE TZ
Nimepoteza kama milioni kwenye Forex. Nimefuta account na kuondoa subscriptions za apps na website za chochote kuhusiana nayo. Nimeiacha kwa kuwa inanipa stress, nakuwa mtumwa naitumikia na siwezi fanya kitu kwa uhuru. Afya ya akili ilidorora na mwili ukadhoofika, nasoma mpaka usiku natumia muda wa kusoma masomo alafu nakula za uso. Nilikuwa na ratiba ndefu ya kuisoma na kutrade

Humu HAKUNA HATA NMOJA anayeweza toa evidence ya kupata faida kwa miezi hii sita. Forex ni ngumu mno na wengi wanaoizungumzia positively wanaishi kwa matumaini, sio kwamba haiwezekani ila ni kwamba wote wanaodai wanaijua wana hasara zaidi kuliko ambao hawajui hata pip ni nini kwa vile hawa ignorants hawajapoteza hela na muda uko.

Nimeweka jumla ya 1.3M mara tofauti since January last year, nimetrade mwenyewe wapi, nikatumia signal wapi, nikaacha kwanza nisome vitabu nikarudi tena wapi. Mara ya mwisho nimeweka hela nikatrade wiki mbili hela zimebaki kiasi kilekile nikatoa hela zangu nikazama kwa David Sportswear, nikala maisha mtaani na nilifurahia hayo maamuzi. Nimetoka kifungoni sirudi tena, kwanza performance class ilishuka

Ukiwa mcha Mungu hutoboi Forex, ukiwa mhuni itaisoma uijue kabisa alafu ushindwe kupata faida uanzishe mafunzo na uuze signal za uongo na kweli. Wauza nguo akina Vunjabei tunawajua, tajeni waliofanikiwa kwa Forex hapa bongo tuwajue
 
Kabisa kiongozi hapo nakuunga mkono, labda hatujafahamu kilichopo nyuma ya mfumo, kwa mfano nina rafiki yangu yeye alikuwa anafanya biashara hii kupitia binary kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa na USD 1200 kwenye account yake baada ya wiki mbili ilipanda hadi USD3400 nilitamani sana anielekeze, kweli alijitahidi kunitafutia vitabu pamoja na audio za training ambazo na yeye aliniaminisha ndizo zimemsaidia, nami nilianza kufanya biashara hiyo kupitia demo akaunti wiki iliyofuata nilienda kwake kufuatilia alupofikia nikiamini angalau kwa speed aliyokuwa nayo ningemkuta na USD zaidi ya 5000 lakini nilikuta tayari ameunguza akaunti yake na hapo ndipo nilianza kuiona biashara hiyo kama sehemu ya kupoteza fedha zako. Hivyo ni kweli kabisa wengi wanachezea za uso.
Huyo ni mjinga Sana anaunguza account ya dola 3000
 
Hahahaha hii ni kawaida sana mkuu, mfano Mimi nilikuwa trader nafahamu sana huyu rafiki yako kilichomuangusha ni kutokuwa na despline ..na inaonesha haya kufikisha hiyo 3000 ni kama solo lilienda upande wake vizuri tu. So akaona huu ni mteremko hivyo alipoingia sokoni tena akaingia kwa ile ile mbinu take bila kuzingatia 'risk management' hivyo mzigo ulipoanza kushuku inaonesha hakuwa na uwelewa wa kutosha hivyo aliacha ukatembea hadi mzigo unaisha wote haha ..hii biashara mkuu itakupeleka na kukupeleka hadi upate akili ya "kuwa na nidhamu" tena ya hali ya juu hapo ushachoma akaunti siyo chini ya kumi ..wanasema "Invest what you can afford to loose" hivyo ni lazima uwe umejiandaa kisaikolojia kufanya hii business..
 
Sahihi, ni biashara zenye ushawishi ila kukumalizia fedha zako ni rahisi sana
Watu watabisha tu ila wanaofanikiwa ni wachache sana kuliko wanaopoteza, mfano kwenye forex wengi wao saiv wameacha Ku trade wanapiga hela za wajinga kwenye kuuza signal za uwongo na kufundisha. Ila nyuma ya pazia wamechezea za uso balaa
 
Wako busy na kusambaza link zao ili wapate bonas za wageni wanaojiunga na kupigwa za uso
 
Nimepoteza kama milioni kwenye Forex. Nimefuta account na kuondoa subscriptions za apps na website za chochote kuhusiana nayo. Nimeiacha kwa kuwa inanipa stress, nakuwa mtumwa naitumikia na siwezi fanya kitu kwa uhuru. Afya ya akili ilidorora na mwili ukadhoofika, nasoma mpaka usiku natumia muda wa kusoma masomo alafu nakula za uso. Nilikuwa na ratiba ndefu ya kuisoma na kutrade

Humu HAKUNA HATA NMOJA anayeweza toa evidence ya kupata faida kwa miezi hii sita. Forex ni ngumu mno na wengi wanaoizungumzia positively wanaishi kwa matumaini, sio kwamba haiwezekani ila ni kwamba wote wanaodai wanaijua wana hasara zaidi kuliko ambao hawajui hata pip ni nini kwa vile hawa ignorants hawajapoteza hela na muda uko.

Nimeweka jumla ya 1.3M mara tofauti since January last year, nimetrade mwenyewe wapi, nikatumia signal wapi, nikaacha kwanza nisome vitabu nikarudi tena wapi. Mara ya mwisho nimeweka hela nikatrade wiki mbili hela zimebaki kiasi kilekile nikatoa hela zangu nikazama kwa David Sportswear, nikala maisha mtaani na nilifurahia hayo maamuzi. Nimetoka kifungoni sirudi tena, kwanza performance class ilishuka

Ukiwa mcha Mungu hutoboi Forex, ukiwa mhuni itaisoma uijue kabisa alafu ushindwe kupata faida uanzishe mafunzo na uuze signal za uongo na kweli. Wauza nguo akina Vunjabei tunawajua, tajeni waliofanikiwa kwa Forex hapa bongo tuwajue
Ukiwa mcha Mungu hutoboi wewe umeona mbali
 
Back
Top Bottom