Kanye2016
JF-Expert Member
- Jun 4, 2016
- 2,466
- 2,440
Nimeona sio vibaya nikatoa tahadhari au angalizo kwa ndugu zangu wenye usafiri binafsi ambao wanapenda kwenda nao Airport ya Julius Nyerere International Airport either kusindikiza ndugu jamaa na marafiki au kupokea wasafiri.
Katika hali ya serikali kuongeza mapato kumetokea na ongezeko la faini nyingi pale JNIA, mfano wiki iliyopita na wiki hii iliyoanza leo nimejionea watu wakitozwa faini kwa makosa ambayo kawaida hayakuwa yakitozwa.
Mfano wa makosa hayo ni kama;-
1) Ukiegesha gari lako katika parking iliyowekwa na matairi ya gari lako yakikanyaga mstari mmoja au yote ujue gari litawekwa minyororo na utatakiwa ulipe faini. Unachotakiwa ukipaki gari lako hakikisha lipo ndani ya mistari miwili ile iliyopo, kabla ya kuondoka hakikisha unakagua maana itakutoka si chini ya mwekundu.
2) Ukisahau kufunga dirisha au ukafunga lakini pakawa na nafasi ya mtu kuingiza hata mkono ujue utapigwa faini tu, gari litawekwa minyororo ile na haitoki lazima utoe chao kwanza.
3) Hakikisha ukifika airport egesha gari lako na wewe utoke ndani ya gari, kama ni dereva nenda kule arrival au departure ukasubiri kule maana ukikaa ndani kwenye gari lililoegeshwa ni kosa pia wakikukuta wenye njaa zao utalipa faini tu na risiti utapewa.
4) Halikadharika, pakiwa na mlango wa gari umesahau kuufunga utalipishwa faini tu.
N.B: Kuna watu wamepewa kazi hiyo ya kukagua gari baada ya gari yaliyokuwa yameegeshwa pale wakisaidiana na askari polisi wanaozungunga pale; so muwe makini na vyombo vyenu.
Na hayo ni baadhi tu ya makosa ambayo nimeyaona binafsi na watu wakalipishwa faini, hivyo kuweni makini.