hengo
JF-Expert Member
- Jun 6, 2011
- 402
- 50
Katika hali isiyo ya kawaida wimbi la vijana wanaodurufu(copy) na kuuza CD`s,VCD`s na DVD`s mbalimbali hasa za maigizo,muziki na nyimbo lazidi kuongezeka siku hadi siku katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani mikoa ya Dar es salaam,Mwanza,Dodoma na Arusha na hivvo kutapeli watu kwa kuwauzia bidhaa hizo feki pia kwenda kinyume na sheria ya hakimiliki. kitendo hiki ni kosa na kinyume cha sheria.
Siku za karibuni kumeibuka kikundi la vijana mkoani Dodoma katika maeneo mbalimbali ya mji hususani stand ya Jamatini,majengo,stand kubwa changombe,makole na ipagala wakiuza CD`s,VCD`s na DVD` mbalimbali ambazo zimechakachuliwa.Kitendo ambacho ni kosa na nikinyume cha sheria ya hati miliki inyozuia mtu yeyeote kudurufu(kupigachapa/copy) kazi ya msanii kwa lengo lolote lile.
Vijana hao jana tarehe 16.03.2012 wameonekana wakifanya biashara hiyo maeneo ya Jamatini kuanzia mida ya Jioni saa 12 hadi saa mbili usiku wakiwa na gari yenye namba T.670AAW ambayo hutumia kurusha matangazo na kubebea bidhaa hizo
Aidha imebainikakuwa vijana hao wanamiliki vibanda vya kuonyesha VIDEO katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma kama vile makole karibu na msikiti,majengo na chang`ombe
Ili kulinda haki, maslahi na heshima kwa wasanii wetu jamii kwa ujumla ikishirikiana na vyombo vinavyohusika na uthibiti wa haki za wasanii pia vyombo vya dola haina budi kuwachukulia hatua za kisheria watu hao kukomesha swala hili.Inapendeza kuona sheria ya hakimiliki iko hai na inafanya kazi kulinda haki za wasanii wote.
Umma na wa kazi wadodoma hawanabudi kujihadhari na vijana hao,pia kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kila waonapobaini makosa kama hili na mengine yakitendeka.Aidha vyombo husika vinapaswa kufatilia swala kadri inavyostahili.