Tahadhali kwa wadada wizi mpya wa Hand bags

duda

Senior Member
Mar 23, 2011
113
25
Habari wana JF, napenda kuwatahadhalisha hasa wanawake na handbags zetu, kuna wizi umezuka hasa maeneo ya kuanzia kijitonyama mpaka mwenge, wanaoiba wanatumia pikipiki, yn anakua dereva na mtu mmoja nyuma then dereva anakumulika taa then anasimama karibu kabisa na wewe, halafu yule mtu wa nyuma anakwapua pochi yako na dereva mara anaondoa pikipiki, imemtokea mdada mmoja juzi pale Bamaga japo alijitahidi kuing'ang'ania pochi yake alichoambulia ni kuburuzwa na kuchunika maana dereva tayari alishaondoa pikipiki hivyo ikabidi aiachie ili asiendelee kuumia.
Tahadhali jamani, tuweni makini na mikoba yetu!!!
nawasilisha
 
aksante kwa taarifa.
dawa ni wadada kuacha kuweka valuables kwenye h/bag. Unapokuwa na vitu vya thaman gharamia hata taxi, maana inaonyesha mambo haya yanafanyika nyakati za jioni au usiku.
 
pk unataka watuwekee hela zetu kwenye matiti??
hii ni njia mbadala lakini big up br,wekeni smu na pesa kwenye vigap vya kati pale usawa wa kifua...kama unacho
 
wizi huo upo sana wanaiba mpk kwenye magari, wanakuja na pikipiki wanavunja kioo wanachukua wanachotaka na moto
 
Kuna jamaa mmoja aliibiwa Laptop kwa staili hiyo ilikuwa mbuyuni hivi au wapi sijui nimesahau jamaa alikwapua na kukimbia nayo
 
ni maeneo mengi sana yanaendesha wizi wa aina hiyo na hasa wale wabebao laptop wawe makini sana kwani wizi wa aina hiyo unaendelea kwa kasi
 
pk unataka watuwekee hela zetu kwenye matiti??
hii ni njia mbadala lakini big up br,wekeni smu na pesa kwenye vigap vya kati pale usawa wa kifua...kama unacho
Imekatazwa na wataalam wa mionzi wanawake kuweka simu karibu na maziwa kwa muda mrefu.
 
Niliwahi nusurika kuporwa laptop ilikuwa wakati natoka natoka Sinza Mori naenda Lufungira, mwenye boda boda alikosea timing ilikuwa saa 2 usiku.

Nimewahi shuhudia pia Dada anaporwa Kipochi chake Mwenge kwa Kakobe.
 
Habari wana JF, napenda kuwatahadhalisha hasa wanawake na handbags zetu, kuna wizi umezuka hasa maeneo ya kuanzia kijitonyama mpaka mwenge, wanaoiba wanatumia pikipiki, yn anakua dereva na mtu mmoja nyuma then dereva anakumulika taa then anasimama karibu kabisa na wewe, halafu yule mtu wa nyuma anakwapua pochi yako na dereva mara anaondoa pikipiki, imemtokea mdada mmoja juzi pale Bamaga japo alijitahidi kuing'ang'ania pochi yake alichoambulia ni kuburuzwa na kuchunika maana dereva tayari alishaondoa pikipiki hivyo ikabidi aiachie ili asiendelee kuumia.
Tahadhali jamani, tuweni makini na mikoba yetu!!!
nawasilisha

Duda Thanks for the information we will have to kaba handbag kwa nguvu zote duh!!!
 
Kuna jamaa mmoja aliibiwa Laptop kwa staili hiyo ilikuwa mbuyuni hivi au wapi sijui nimesahau jamaa alikwapua na kukimbia nayo

Yes hata gari ndogo (saloon) siku hizi zatumika kwa wizi wa namna hiyo. Na waathirika si wadada tu ni wote wakiume kwa wakike. So una briefcase, laptop, handbag au chochote kinachovuta attention yao ni target kwao. Tuwe makini
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom