TAHADHALI KWA CHADEMA: Chacha Wangwe na Msiba Wa Regia Mtema

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,270
675
WanaJf hebu tujikumbushe yaliyotokea katika msiba wa chacha wangwe


"Kumeibuka utata juu ya kifo chake hasa kutokana na mkanganyiko wa taarifa baina ya mashuhuda wawili walioshuhudia ajali hiyo huku wengine wakidai kuwa marehemu alipigwa risasi.Hali hiyo ilimlazimu mwenyekiti wa Chadema Ndg Freeman Mbowe kuondolewa na polisi eneo la tukio kutokana na shinikizo la wananchi hao kusema aondolewe katika msiba huo kwasababu ya migogoro ya kiuongozi ndani ya chama chao na kujenga hisia potofu juu ya kifo cha marehemu Chacha Wangwe." Source HAbari LEO


MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, anadaiwa kufanya hafla kubwa Afrika Kusini saa chache baada ya kupata taarifa za kifo cha Makamu wake, marehemu Chacha Wangwe.Habari zilizopatikana kutoka hoteli ya Garden Court jijini Johanesburg ilikoifanyika hafla hiyo Julai 29 mwaka huu, zilisema baada ya Mwenyekiti Mbowe kupokea taarifa za msiba, alifanya hafla ya kuwaaga wajumbe aliokuwa nao huko ili arejee nchini kwa mazishi.

“Kwanza taarifa ilipopatikana, hakututangazia mpaka tulipopata kutoka kwa vyanzo vyetu vingine ndipo tukathibitisha naye…akatuandalia hafla jioni ya siku hiyo,” kilidai chanzo cha habari hii.
Kilidai kuwa kilishangaa kuona katika mazingira yale ya majonzi, kuandaliwa hafla kubwa namna ile.

“Tulishangaa na kumuuliza kwa nini hafla ile, akatujibu kuwa alikuwa akituaga, kwani anarudi nchini kushiriki mazishi ya marehemu Wangwe,” kiliongeza chanzo hicho.


Alipoulizwa ilikuwaje akahudhuria mkutano huo wakati ulikuwa ni kwa ajili ya makatibu wakuu na manaibu wao kutoka vyama vyenye wabunge, Bw. Mbowe alisema alipewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.
“Mimi nilialikwa na watu TCD kuhudhuria mkutano huo,” alisisitiza Bw. Mbowe alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.
Akizungumzia madai kuwa alikataa michango waliyotaka kutoa baadhi ya washiriki aliokuwa nao kwa ajili ya rambirambi na badala yake kudaiwa kuwataka watoe ahadi zao na akifika Dar es Salaam atawatolea, Bw. Mbowe alijibu:
“Wewe zungumza na vyanzo vyako hivyo vikuthibitishie kama hayo yalitokea.”
Bw. Mbowe alimtaka mwandishi wa habari hizi kuwauliza watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) au CCM au TCD kama kweli hayo yalitokea au la kwa sababu nao walihudhuria mkutano huo
Source: UHURU



Mytake:

Magamba wako makini na huu msiba chochote
kinaweza kutokea kwa hiyo cdm kuwa makini

Msiba wa chacha wangwe watu waliogwa hela kufanya fujo
na wanahabari kama kawa wanabahasha zao kwa kuanza
kuandika upupu na upuuzi kama hapo juu

 
Please stop this insinuations!. Don't politicize everything with conspiracy theories!.
Mtu hata hajapumzishwa, unatuletea utumbo kama huu!.
Utu wetu uko wapi?. Nimeamini kweli wengine wetu are wicked!. Wao wanawaza mabaya na maovu tuu!.
 
Please stop this insinuations!. Don't politicize everything with conspiracy theories!.
Mtu hata hajapumzishwa, unatuletea utumbo kama huu!.
Utu wetu uko wapi?. Nimeamini kweli wengine wetu are wicked!. Wao wanawaza mabaya na maovu tuu!.

Ukiambiwa ukweli inakuwa inauma sana
Waandishi ndo waliongoza kuandika upuuzi huu baada ya kupokea bahasha kutoka kwa magamba

Vipi ulikuwa moja wapo?
 
Aisee,
Ni tahadhari nzuri, lakini timing yake si nzuri bana!
Ungeacha tutoke kwenye hatua hii ya mazishi ya mpendwa wetu kwanza!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom