TAHA; Fursa ya biashara Qatar

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,061
5,389
Mkurugenzi wa TAHA dada Jaque,

tumeona namna nchi za kiarabu zimefunga milango kwa nchi ya Qatar, na kipindi hiki cha mfungo ni vizuri mkaanza kunegotiate deals ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa sasa.

Tumieni ushawishi wa serikali na ubalozi wao hapa nchini kupata access. Najua kuna mboga mboga nyingi, matunda, spices, maua n.k hata kama sio sasa hata hapo baadae ili kurusu uzalishaji wa mazao husika.

Pia ni fursa klwa sector zingine nchini hasa food sector, UFUTA, Karanga, Samaki, Nyama [beef, muton, lamb, chicken}. tutumie muda huu vizuri. Kufa kufaana
 
Ukweli Tanzania tuna mboga mboga nyingi kuliko hata mahitaji, tunaangushwa na wadau wasimamizi wa sector
 
Ni fursa kweli , tatizo watu wameconcetrate kwenye siasa na mapenzi na hutawaona kwenye thread kama hizi.

Ila ingekuwa habari kungekuwa na page za kutosha hapa za comments!
 
Qatar kususiwa na warabu pori wenzie wewe mswahili utaiweza!?

Kweli ni fursa ila, inahitaji umakini sana kuichukua na siyo an overnight decision.

Au unataka Tanzania, tuwekwe kwenye kundi la nchi zinazo lisha magaidi!?

Maana Qatar imepewa kesi ambayo nchi yoyote ikijihusisha nayo saaaana hutachelewa kuona press conference kutoka USA, saudia na kwengineko kuwa nchi fulani inasaidia magaidi.
 
Back
Top Bottom