Tafuta wa kufanana nae;usikimbilie tu kuoa,just kuoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafuta wa kufanana nae;usikimbilie tu kuoa,just kuoa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,499
  Likes Received: 5,727
  Trophy Points: 280
  Wakufanana Naye!

  [​IMG]Tafiti nyingi zinafanana na zinakubali kwamba ndoa nyingi imara ni zile ambazo mke na mume huwa na sifa nyingi zinazofanana.
  Kundi la watafiti lilikusanya ndoa 35 (wanawake na wanaume 70) ambazo ziliwekwa katika makundi matatu kundi la kwanza lilikuwa la wale ambao ndoa zako zilikuwa za furaha, kundi la pili zile zilikuwa ni zile wanandoa walikuwa na wakati mgumu kuishi pamoja na kundi la tatu la wale walikuwa njiani kuachana.

  Majibu yalikuwa ni kwamba wale walioishi kwa furaha walifanana sana katika mambo mengi (general activities), walikuwa marafiki na walifanana katika kujihusisha binafsi na mwenzake.
  Wale ambao hawakuwa na furaha kuishi pamoja hawakufanana katika utendaji wa mambo yao kila siku, pia hawakufanana linapokuja suala la mwitikio wa hisia zao. ​
  Wale waliokuwa wanataka kuachana kila mmoja alikuwa na sifa nyingi zisizofanana kabisa.

  Kiwango cha furaha katika ndoa huweza kujieleza kutokana na kufanana kwa wanandoa katika sifa binafsi walizonazo.
  Hii ina maana wanandoa wakifanana kiuchumi, tabia, mazingira, tamaduni, matumizi ya pesa, kiwango cha energy, uwezo wa kuongea na kusikiliza, kiimani, kihisia nk inakuwa rahisi kila mmoja kutegemea nini kutoka kwa mwenzake.

  Hivyo ukitaka kuwa na ndoa imara ni muhimu kuwa na balance account ambayo kufanana ni zaidi ya tofauti kwa sbabu kila tofauti iliyopo inahitaji kupatanisha na kuweka kuikubali hata kwa maumivu.

  BWANA Mungu akasema,
  Si vema huyu mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
  Mwanzo 2:18
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nina wasiwasi na hiyo Mwanzo 2:18

  Bibilia za kiingereza imeandikwa hivi:

  Genesis 2:18 (New International Reader's Version)
  The Lord God said, "It is not good for the man to be alone. I will make a helper who is just right for him."


  Genesis 2:18 (New American Standard Bible)
  Then the LORD God said, "It is not good for the man to be alone; (A)I will make him a helper [a]suitable for him."

  Cross references:
  1 Corinthians 11:9
  (A) for indeed man was not created for the woman's sake, but woman for the man's sake.

  1 Corinthians 11:9 (English standard version)
  (A) Neither was man created for woman, but woman for man.​
   
 3. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hili ndugu yangu ni somo gumu,GUMU SANA, ambalo hata uprofesa haufui dafu.
  Inabidi kila Ijumaa na Jumapili Masheikh Mapadre na Maparoko walieleze kwa mahubiri mahsusi hasa kwa vijana kati ya 18-35yrs.Kwa waliozaidi ya umri huo then it is too late na aliyeingia katika mtego wa ndoa ataswim na matatizo aliyojitwaalia mpaka mwisho wa maisha yake.
   
Loading...