Tafsiri yangu ya Rosta azizi kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri yangu ya Rosta azizi kujiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sada maganga, Jul 15, 2011.

 1. s

  sada maganga New Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,
  Habari kubwa imetufikia; Rostam Aziz kaachia ngazi CCM. Ni habari kubwa.
  Wengine wanasema, kuwa Rostam amejivua gamba. Kuna wanaodai, kuwa ni CCM
  ndio iliyojivua gamba. Ni misamiati tu, isikuumize kichwa.

  Nimesoma hotuba ya Rostam akiongea na ’ Wazee wa Igunga’. Imekuwa utamaduni,
  kama wa enzizile za Mwalimu. Kwenye jambo zito, Mwalimu aliongea na ’ Wazee
  wa Dar es Salaam’. Sio ndio waliomkaribisha mjini.

  Kuna akina sisi tulio tofauti na wale wanaodhani wanajua. Sie tunajitahidi
  kujua. Na hapa ni tafsiri yangu ya kuachia ngazi kwa Rostam Aziz. Kwangu mie
  ilikuwa ni suala la wakati tu; kuwa Rostam hakuwa na njia ya kutokea zaidi
  ya kukubali ’ kujiporomosha’ mwenyewe kutoka kwenye ngazi. Ndio, ni heri
  anayeshuka kwenye ngazi kuliko anayeachia ngazi na kuporomoka. Kushuka
  kwenye ngazi kunaashiria taratibu. Kuna upepo mgumu unavuma ndani ya CCM. Na
  upepo mwingine huangusha miti mikubwa.

  Na Rostam huyu alikuwa ni sehemu ya ’ mapacha watatu’ kama wanavyojulikana
  sasa; Rostam , Andrew na Edward. Kuna wanaoanza kuhesabu siku kabla kusikia
  habari nyingine kubwa; kuwa Edward naye ’ kajiporomosha’ kutoka kwenye ngazi
  za CCM, kisha afutie Andrew. Yote hayo yanawezekana, lakini, kila inapoisha
  arobasitini moja , karata huchangwa upya. Hapo huanza arobasiti mpya. Siasa
  yaweza kuwa kama mchezo wa arobasitini! Na mazingira ya Rostam wa
  Unyamwezini Igunga yaweza kuwa tofauti na ya Andrew wa Usukumani na Edward
  wa Umasaini. Burudani ya siasa inaendelea!

  Na Watanzania tu mabingwa wa siasa za matukio. Leo ni Rostam. Baada ya wiki
  moja Rostam si habari tena. Tunasubiri nyingine, labda itakuja ya Edward na
  baadae Andrew. Na ’ mapacha watatu’ wakishamalizika? Stay tuned; Kuna mpya
  nyingine itakuja.

  Na Rostam pale Igunga kwa wazee wake amezungumzia ’ Afya ya siasa’ ya nchi.
  Hakusema kama ni njema au la. Katikati ya mistari kuna tulioelewa alichotaka
  kusema Rostam. Tena Rostam huyu ambaye kuna wakati iliaminika ndiye yuko
  nyuma ya ’ mikakati’ ya ndani ya Chama chake.

  Leo kaacha kila wadhifa ndani ya Chama. Lakini usisahau, kuwa Rostam amebaki
  na ’ hirizi’ mfukoni. Ni kadi ya chama. Mjinga ni yule anayemwondoa Rostam
  mwenye ’ hirizi’ ya Chama kwenye ’ hesabu’ za mikakati ya CCM.

  Na si amesema mwenyewe; kuwa haikuwa kazi rahisi kwao kuifanya Tabora ambayo
  ni kitovu cha upinzani kuwa mkoa ambao majimbo yote yanayoongozwa na CCM.
  Je, Rostam ’ anatishia nyau’ au kuna mtaji anawekeza kwenye ’ nyumba ’ya
  mchezo wa bao? Na tusubiri tuone.

  Na hii afya ya siasa anayoizungumzia Rostam? Sijui yeye katumia vipimo vya
  kliniki gani. Mie nitapiga mbizi na kuzama zaidi majini. Na hapa unisome kwa
  makini . Ndio, kama nchi Watanzania ni kama wagonjwa tunaotafuta tiba. Na
  tumekuwa ni watu wa kubahatisha tiba kila kukicha. Hata kukimbilia
  abrakadabra ya kikombe cha ’ Babu wa Lolilondo’ ni kielelezo cha maradhi
  yetu na kuhangaika kwetu.

  Mgonjwa hukosa faraja na huzidi kuwa na mashaka pale daktari anaposhindwa
  kufanya diagnos ya ugonjwa husika na kujua ni nini hasa chanzo cha maradhi.
  Kisha daktari anajaribu kumpa mgonjwa dawa akitumaini tu kuwa huenda
  ikamsadia. Lakini, mgonjwa hupata faraja na huingiwa matumaini ya kupona
  pale anapofanyiwa diagnos na daktari anapomtamkia mgonjwa chanzo cha maradhi
  ya kinachomsibu na dawa anayotakiwa kutumia ili apone.Na ndio sisi
  Watanzania; tu wagonjwa tunaofanyiwa majaribio ya dawa ya kutuponesha
  maradhi yetu bila haswa daktari kujua chanzo cha maradhi yetu.

  Nimeandika majuzi tu kwenye Raia Mwema; kuwa Watanzania tunapaswa sasa
  kuvunja ukimya na kuzungumzia mema na mabaya yaliyopita ili yatusaidie
  kujenga misingi imara ya taifa letu hata kwa miaka 50 ijayo. Tuna wajibu wa
  kizalendo wa kutoa ushahidi wetu kwa kusimulia tuliyoyapitia ili waliopo na
  wajao waweze kuyachukua mema na kutorudia makosa yaliyofanyika nyuma.

  Maana, kuna tulioshuhudia Tanzania iliyokuwa na ustawi na dalili za
  kuendelea kustawi. Tumeshuhudia pia ni kwa jinsi gani wingu hilo la
  matumaini lilivyokuwa likipotea kwa kasi ya kutisha na kupisha jua kali
  lililoleta ukame wa kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.

  Na msingi wa haya yote ni ubaguzi wa kisiasa na kutoruhusu mazingira ya
  uwepo wa fikra mbadala. Kuwachukia wenye ’ akili’ na walio tayari kuzitumia
  akili zao kwa manufaa ya nchi yao. Hivyo basi, watu hao hutengwa na mfumo wa
  uongozi wa kisiasa uliopo.

  Na huo ndio msingi wa uwepo w a hoja ya ubaguzi wa kisiasa. Na dhambi hii ya
  ubaguzi wa kisiasa ndilo gamba gumu la kitaifa tunalopaswa kulivua. Maana,
  ndio hali yenye kusababisha maradhi yetu mengi kama taifa ikiwamo ufisadi
  uliotamalaki.
   
Loading...