Tafsiri yangu Kutoka barua ya kurugenzi ya mawasiliano Ikulu

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Ni wazi kabisa Mh Pinda na mama Makinda hawana busara! Niwazi Raisi hakubaliani na posho, ila kwa kuwa ni people's pleaser amesukumia wasio na busara kuamua
 
Rev, what happened maana sidhani kama wote tunaweza kujua ni barua ipi unayoiongelea? Au si wote tumweza kuiona hiyo barua.
 
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
 
Najiuliza sipati jibu juu ya haya:
-Bunge huwa linataka Rais afanye nini juu hizi posho zao?
-Rais ni sehemu ya mchakato wa kupandisha posho hizi?
-Ni kweli Bunge limeanza kulipa posho hizi?
 
Najiuliza sipati jibu juu ya haya:
-Bunge huwa linataka Rais afanye nini juu hizi posho zao?
-Rais ni sehemu ya mchakato wa kupandisha posho hizi?
-Ni kweli Bunge limeanza kulipa posho hizi?

Kuna wingu zito kwenye kila hatua tunayopita kama nchi sasa hivi. Naona kila institution inafanya kazi kwa maslahi yake maana sielewi vitu kama hivi kuonekana kama havina taratibu. Inawezekanaje kulipwa pesa bila idhini ya serikali?
What is going on? Huu upoyoyo umepitiliza mipaka
 
Ni wazi kabisa Mh Pinda na mama Makinda hawana busara! Niwazi Raisi hakubaliani na posho, ila kwa kuwa ni people's pleaser amesukumia wasio na busara kuamua

Ni wazi pia Raisi hana msimamo. Kama hakukubaliana na posho alitakiwa aseme hivyo sio kuzunguka mbuyu!
 
Hata hao kurugenzi ya Mawasiliano wa Ikulu hawako sawa. Koz wao wamekanusha taarifa iliyotolewa na Gazeti la Mwananchi nadhani ingekuwa Busara kama wangekanusha kama gazeti limekosea kumkariri Waziri mkuu na Spika. Je wao Kurugenzi ya Mwasiliano ya Ikulu wanakubali au wamekataa kuwa Spika na Pinda hawakusema walichoandika Mwananchi???


Kama yes / No wanawachukuliaje viongozi hao wakubwa katika taifa hili???? Sidhani kama Pinda angelitolea tamko hili swala bila kuwasiliana na Rais. Kifupi haileweki nani mkweli nani muongo na generally wote ni wasanii.
 
Kwa hili, raisi wetu amethibitisha kuwa kazi imemshinda. Badala ya kutoa maamuzi anatoa porojo. Ukiwa kama kiongozi kama huwezi kufanya maamuzi katika jambo lolote wewe hufai kuwa kiongozi. Hapa raisi wetu amejidhihirisha kuwa ni pumba kabisa. Inapofikia wakati hata kupingana hadharani kati ya raisi na waziri mkuu mjue nchi iko hatarini. Ee Mungu tuokoe na janga hili la viongozi
 
Kwa hili, raisi wetu amethibitisha kuwa kazi imemshinda. Badala ya kutoa maamuzi anatoa porojo. Ukiwa kama kiongozi kama huwezi kufanya maamuzi katika jambo lolote wewe hufai kuwa kiongozi.

Hapa raisi wetu amejidhihirisha kuwa ni pumba kabisa. Inapofikia wakati hata kupingana hadharani kati ya raisi na waziri mkuu mjue nchi iko hatarini. Ee Mungu tuokoe na janga hili la viongozi

Nanavyofahamu mimi huu ni mwaka wa sita Tanzania haina Rais, kuna jamaa yupo kimagumashi tu hapo Magogoni. Tanzania ni moja wapo ya maajabu ya dunia, miaka sita bila rais!

 
Ninachojua mimi Waandishi wa Habari huwa hawaweki katika gazeti habari ambayo hawajaifanyia upekuzi hasa haya magazeti binafsi kwani wanabanwa na sheria.

Sasa kama Ikulu wanapinga na Spika amethibitisha:

NASHAURI:

Wabunge waanike hadharani katika magazeti Payrol zao za malipo kuanzia kikao kilichopita.

Kwa kuthibitisha hili IKULU itoe tamko kuhusu payroll za Wabunge ziwekwe hadharani.

Tutajua nani anatuletea siasa katika Uhalisia wa mambo!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom