Tafsiri Yangu: Dhambi Ya Ubaguzi Sasa Imeanza Kututafuna WaTanzania ( Makala, Mwananchi, Jumapili)

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,

Ndugu zangu,

Kule Igunga leo Jumapili wanafanya uchaguzi mdogo kujaza kiti cha ubunge kilichoachwa wazi na Rostam Aziz. Tunawatakia uchaguzi mwema na wa amani. Juma la jana niliandika, kuwa yanayotokea Igunga ni kielelezo cha uendawazimu wetu. Maana, katika mengi, tumeona hata mbegu za chuki zikipandwa kule Igunga. Kuna wanaopandikiza chuki miongoni mwa Watanzania. Na kule Igunga tumeona pia karata chafu ya udini ikitumiwa.

Tafsiri yangu; dhambi ya ubaguzi imeanza kututafuna WaTanzania. Maana, udini ni karata ya hatari kwa mwanasiasa kuicheza katika nchi kama Tanzania. Anayecheza karata ya udini katika siasa ni mtu asiyeitakia heri nchi yetu.

Na achezaye karata ya udini kimsingi ni mbaguzi. Anataka Watanzania waanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Na chanzo cha yote haya ni ubaguzi wa kisiasa ambao tumekuwa nao kwa takribani miaka 50 sasa.

Ubaguzi wa kisiasa ni pale wachache wanapoona wengine hawastahili kushiriki siasa na uongozi wa nchi. Kufanikisha azma yao hiyo watatumia mbinu zote ikiwamo hila na ghilba kwa umma.

Ndugu zangu,

Sisi ni Watanzania na hii ni nchi yetu. Watanzania hatuna utamaduni wa kubaguana kwa misingi ya kikabila na kidini. Tuwapuuze wote wanaofanya jitihada za kutugawa kwa misingi ya udini, ukabila, rangi na hata siasa. Watanzania ni Watanzania.

Mshikamano wetu na mashirikiano ya kindugu ndio yanayotufanya tupigiwe mfano Afrika na duniani.Tunachoshuhudia sasa ni mwelekeo mbaya kwa taifa letu. Kwani, kwa asili na utamaduni, Watanzania tumeishi kwa amani na kuchanganyikana bila kujali tofauti zetu za kidini na kikabila.

Kama taifa, ni jambo jema na la bahati kubwa kuwa nchi yetu haina dini. Kila Mtanzania, kwa mujibu wa Katiba, ana uhuru wa kuabudu dini atakayo. Ana uhuru pia wa hata kutoabudu katika dini ye yote ile. Na hakika, Watanzania hatuna udini. Ni bahati mbaya tu kuna wachache, kwa maslahi yao, wanapandikiza dhana hii ya udini kwa Watanzania.

Nilipata kupigiwa simu na msomaji wangu akiwa kijiji cha Mwambata, Masasi. Alijitambulisha kwa jina la Edward Hassan. Nilimdadisi juu ya mchanganyiko wa Edward na Hassan katika jina lake. Akaniambia; kuwa huko maeneo ya kusini ni kawaida sana. Utamkuta mtu anaitwa Dominic Rashid, John Ramadhan na mengineyo. Ni majina yanayotokana na dini za kimapokeo toka kwa Waarabu na Wazungu. Lakini, Watanzania wana majina ya asili ya koo zao. Majina yasiyotokana na dini za kimapokeo. Mengi ni majina yenye maana fulani.

Ndio, Watanzania tumechanganyika kiasi hata kwenye koo zetu tunatofautiana katika imani za kimapokeo; Ukristo na Uislamu. Ni kawaida kabisa katika ukoo mmoja kuwakuta Waislamu na Wakristo. Kinachowaunganisha wanaukoo hawa ni mila zao za jadi ikiwamo matambiko yao.

Na leo hii, katika nchi yetu, kuna familia zenye wanafamilia wa imani tofauti za kimapokeo; Uislamu na Ukristo. Ni kawaida kumkuta mama Mkristo na baba Mwislamu au kinyume chake. Ni kawaida kuwakuta watoto wa familia moja wenye kufuata imani tofauti.

Swali linakuja; hivi wenye kuhubiri chuki za kidini wanafahamu kuwa watachochea hata vita vya kikoo? Maana, koo zetu nazo zina tofauti za kidini, hususan dini hizi tulizozipokea toka kwa Wazungu na Waarabu.

Ndugu zangu ,

Kuna kila dalili, kuwa sasa baadhi ya viongozi wa kidini na wanasiasa, kwa maslahi yao, wanafanya juhudi za kutugawa Watanzania kwa misingi ya kidini. Tusikubali kugawanywa na tukafikia kuchinjana. Watanzania, Wazalendo wa nchi hii, tuna kila sababu ya kuihami nchi yetu dhidi ya chuki hizi za kidini na kisiasa.

Naam. Uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana. Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia WaTanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.

Bi Mukanyange alisema: ” Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994,” alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao.Ndugu zangu,

Na tufanye yote tuwezayo kuzuia utabiri wa Bi Mukanyange usitimie. Maana, Wahenga walisema; ”Kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Nahitimisha.

http://mjengwa.blogspot.com
 
Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Umaskini na Njaa vimeshika kasi haya yote yatatokea moja baada ya Jingine. Maana hakuna tena anayemuogopa Mungu zaidi ya kukidhi mahitaji ya Tumbo na fahari za Dunia.

Kupinda ukweli kwa masilahi ya kufurahisha kundi ama mtawala ni utamaduni unaozoeleka sasa kwa viongozi wa Dini.

Tusubiri fedheha huko tuendako
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,387
25,251
Na Maggid Mjengwa,

Ndugu zangu,

Kule Igunga leo Jumapili wanafanya uchaguzi mdogo kujaza kiti cha ubunge kilichoachwa wazi na Rostam Aziz. Tunawatakia uchaguzi mwema na wa amani. Juma la jana niliandika, kuwa yanayotokea Igunga ni kielelezo cha uendawazimu wetu. Maana, katika mengi, tumeona hata mbegu za chuki zikipandwa kule Igunga. Kuna wanaopandikiza chuki miongoni mwa Watanzania. Na kule Igunga tumeona pia karata chafu ya udini ikitumiwa.

Tafsiri yangu; dhambi ya ubaguzi imeanza kututafuna WaTanzania. Maana, udini ni karata ya hatari kwa mwanasiasa kuicheza katika nchi kama Tanzania. Anayecheza karata ya udini katika siasa ni mtu asiyeitakia heri nchi yetu.

Na achezaye karata ya udini kimsingi ni mbaguzi. Anataka Watanzania waanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Na chanzo cha yote haya ni ubaguzi wa kisiasa ambao tumekuwa nao kwa takribani miaka 50 sasa.

Ubaguzi wa kisiasa ni pale wachache wanapoona wengine hawastahili kushiriki siasa na uongozi wa nchi. Kufanikisha azma yao hiyo watatumia mbinu zote ikiwamo hila na ghilba kwa umma.

Ndugu zangu,

Sisi ni Watanzania na hii ni nchi yetu. Watanzania hatuna utamaduni wa kubaguana kwa misingi ya kikabila na kidini. Tuwapuuze wote wanaofanya jitihada za kutugawa kwa misingi ya udini, ukabila, rangi na hata siasa. Watanzania ni Watanzania.

Mshikamano wetu na mashirikiano ya kindugu ndio yanayotufanya tupigiwe mfano Afrika na duniani.Tunachoshuhudia sasa ni mwelekeo mbaya kwa taifa letu. Kwani, kwa asili na utamaduni, Watanzania tumeishi kwa amani na kuchanganyikana bila kujali tofauti zetu za kidini na kikabila.

Kama taifa, ni jambo jema na la bahati kubwa kuwa nchi yetu haina dini. Kila Mtanzania, kwa mujibu wa Katiba, ana uhuru wa kuabudu dini atakayo. Ana uhuru pia wa hata kutoabudu katika dini ye yote ile. Na hakika, Watanzania hatuna udini. Ni bahati mbaya tu kuna wachache, kwa maslahi yao, wanapandikiza dhana hii ya udini kwa Watanzania.

Nilipata kupigiwa simu na msomaji wangu akiwa kijiji cha Mwambata, Masasi. Alijitambulisha kwa jina la Edward Hassan. Nilimdadisi juu ya mchanganyiko wa Edward na Hassan katika jina lake. Akaniambia; kuwa huko maeneo ya kusini ni kawaida sana. Utamkuta mtu anaitwa Dominic Rashid, John Ramadhan na mengineyo. Ni majina yanayotokana na dini za kimapokeo toka kwa Waarabu na Wazungu. Lakini, Watanzania wana majina ya asili ya koo zao. Majina yasiyotokana na dini za kimapokeo. Mengi ni majina yenye maana fulani.

Ndio, Watanzania tumechanganyika kiasi hata kwenye koo zetu tunatofautiana katika imani za kimapokeo; Ukristo na Uislamu. Ni kawaida kabisa katika ukoo mmoja kuwakuta Waislamu na Wakristo. Kinachowaunganisha wanaukoo hawa ni mila zao za jadi ikiwamo matambiko yao.

Na leo hii, katika nchi yetu, kuna familia zenye wanafamilia wa imani tofauti za kimapokeo; Uislamu na Ukristo. Ni kawaida kumkuta mama Mkristo na baba Mwislamu au kinyume chake. Ni kawaida kuwakuta watoto wa familia moja wenye kufuata imani tofauti.

Swali linakuja; hivi wenye kuhubiri chuki za kidini wanafahamu kuwa watachochea hata vita vya kikoo? Maana, koo zetu nazo zina tofauti za kidini, hususan dini hizi tulizozipokea toka kwa Wazungu na Waarabu.

Ndugu zangu ,

Kuna kila dalili, kuwa sasa baadhi ya viongozi wa kidini na wanasiasa, kwa maslahi yao, wanafanya juhudi za kutugawa Watanzania kwa misingi ya kidini. Tusikubali kugawanywa na tukafikia kuchinjana. Watanzania, Wazalendo wa nchi hii, tuna kila sababu ya kuihami nchi yetu dhidi ya chuki hizi za kidini na kisiasa.

Naam. Uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana. Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia WaTanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.

Bi Mukanyange alisema:  Naogopa, kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994, alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauaji yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao.Ndugu zangu,

Na tufanye yote tuwezayo kuzuia utabiri wa Bi Mukanyange usitimie. Maana, Wahenga walisema; Kamba hukatikia pabovu. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Nahitimisha.

http://mjengwa.blogspot.com
Tuna ombwe la uongozi wakuu hasa Mkuu wa nchi,watawala na wananchi waliobaki hasa kwa nchi changa kielimu na demokrasia wanafanya kwa kusoma mlengo wa mkuu wa nchi.nchi zilizoendelea zote zilianzia kwa kupata Marais wanamapinduzi kweli.tabia ya watz kipindi cha Nyerere si ya kipindi cha Mwinyi hadi sasa.Kiongozi wa juu anapaswa kuwa na msimamo wa wazi na asiwe mnafiki.haya ya udini yameasisiwa na ccm kwa manufaa yao ya kutawala.hili ni dhahiri na bado mnaogopa kusema wazi! Kuna redio na magazeti yanaandika na kutangaza vitu vya ajabu tupo kimya! Msimamo wa wazi wa Rais unatengeneza foundation kwa viongozi wote.Mjengwa na wengine hebu semeni ukweli na kwa uwazi,tuache kuandika makala za kimafumbo hazisaidii,tuwataje kwa uwazi wote na kwa ushahidi wanaoeneza udini.CCM wanatuharibia nchi kwa kuchanganyikiwa na upepo wa mabadiliko.UDINI UNALETWA NA CCM KIPROPAGANDA FULL STOP!
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,503
3,041
tatizo ni hawa wazee pusi na paka na wanao wazunguka kama yule anayeonyesha pistol hadharani kama tuko somalia wao wameisha kula nchi wanataka kutuachia balaa, hao no kuwashughulikia ipasavyo wasituharibie nchi na maisha
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,503
3,041
infawact hili gamba la huyu aliye toa silaha kama tuko al shaba linatakiwa livuliwe baada ya uchaguzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom