Tafsiri yake... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri yake...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ngoshwe, Jun 11, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MWENZENU TAFSIRI YA HUU WIMBO JAMBO ULIKUWA UNALENGA AMANI LAKINI ULILKUWA NA MAANA ZAIDI YA HAPO HASA MAMBO YALIVYO SASA, VILIO VYA WATANZANIA VIMEJIDHIHIRISHA KWENYE MENGI NA KUKUMBUKA UTAWALA ULIOPITA NA KUSEMA "BORA CHE NKAPA!!!"


  HIYO AMANI INAYOZUNGUMZIWA UENDA IKAWA IMEKWISHA POTEA KATIKA SAIKOLOJIA YA WENGI IKITAFSIRIWA KWA MAPANA YAKE..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ujumbe ni mzuri kwa kadiri ya muono wake,na wewe kama una ujumbe wako kuhusu popote unaona hapaendi vizuri unaweza kutoa maoni yako.kazio ya kulinda nchi ni yetu sote. safi sana misholi
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Hizo suti... Mhh
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wake nampa pongezi. Lakini mistari iliyotoka nje ya maana ni pale anaposema "Kiongozi atakayelinda amani kwa nguvu zake zote" - Amani hailindwi kwa mtutu wa bunduki wala ubora wa jeshi na silaha kali walizo nazo. Amani hudumishwa kwa nchi kuwa na misingi ya haki na usawa. Katika dhulma au uonevu amani huwa haipo kwani suala la Amani ya nchi linahusu mawazo ya watu zaidi kuyafanya yawe katika kujiona ni wazalendo na wanatendewa haki katika kila nyanja, kuanzia ya kuwa na maisha bora, kuwa na haki ya kuchagua kiongozi wanaemtaka wao bila kuingiliwa maamuzi yao na watawala kwa kubadili matokeo ya kura.

  Kwa ujumla amani ni suala la ki-saikolojia zaidi ya kutisha watu kwa kuwaua ama kuwakamata na kuwaonesha cha mtema kuni. Amani ni haki na usawa, amani ni kushughulikia wezi wa mali za umma ili wananchi wasijejichukulia sheria mikononi mwao siku. Amani ni kutokuonea wananchi kwa kuwabambikia kesi ili watoe rushwa. Kwa ujumla Tanzania hatuna amani bali tumetulia tu na siku utulivu nao ukiondoka basi tusishangae kuona hayo anayoimba Misholi ni mambo ya kawaida. na ikitokea hapo ndipo mawazo ya kulipa visasi yatakapokuwa kama uyoga na ni ngumu sana kuyafuta kwa mtutu wa bunduki na vitisho bali ni kwa haki na usawa kwa raia wote bila kujali itikadi zao wala rangi na jinsia zao

  Amani si suala la Rais wala chama cha siasa bali ni suala la jamii nzima ikiongozwa katika misingi ya haki na usawa. Kiongozi yeyote atakayekuwa tayari kutekeleza haya atakuwa anadumisha misingi ya kukukua kwa amani na kudumu kwa utulivu.
   
Loading...