Ndugu zangu,
Moja ya habari kubwa kwenye magazeti ya leo ni habari kuwa wadau wakiwemo wanazuoni kuitahadharisha ZEC kuhusiana na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi uliofanyika na ukafutwa kule Zanzibar.
Kasoro hizo zirekebishwe ili uchaguzi ufanyike, matokeo yatangazwe na Wazanzibar waendelee na kazi za kujenga uchumi wao na wa visiwa vyao.
Tayari wananchi walio wengi visiwani wako katika wakati mgumu kiuchumi na kijamii kutokana na kadhia hii ya kisiasa kutokana na uchaguzi ambao haukwenda vema. Na kwenye wananchi walio wengi ni vijana ambao hawakuwa na ajira kabla ya uchaguzi na mazingira ya sasa yanawaweka katika wakati mgumu zaidi.
Ni dhahiri, Wazanzibar wanyonge walio wengi hii leo ni walio wagonjwa kiuchumi na wenye kuhitaji tiba ya haraka ili warejeshe matumaini yao. Vijana walo wengi hawana ajira na hawana hakika yao ya leo na kesho.
Inafahamika, ajira kwa walio wengi visiwani inatokana na sekta ya utalii ambayo sasa iko kwenye umahututi kutokana na hofu ya kutokea machafuko ya kisiasa yenye kuwatisha wawekezaji na watalii wenye mazoea ya kutembelea visiwa hivyo.
Kwa hali halisi ilivyo sasa uchaguzi wa marudio ndio mujarab kwa maana ya tiba kwa watu wa visiwani. Wenye kufikiri kususia uchaguzi huo hawawezi kuwa na dhamira ya dhati ya kutaka kuwasaidia Wazanzibar katika hali walizonazo sasa.
Taadhari inayotolewa sasa kwa ZEC kuhusu kurekebisha kasoro za nyuma ndilo jambo, wapenda amani wote tunalopaswa kulihimiza ili tusije tukarudi tulikotoka.
Kama taifa, na kama wazalendo katika nchi tuliyozaliwa na tunayoipenda, tukubaliane, kuwa si kwa maslahi mapana ya nchi yetu, Bara na Visiwani, kutanguliza siasa iliyotawaliwa na uchu wa madaraka uliojengwa kwenye msingi wa maslahi binafsi, kufanya yale yatakayochochea uhasama na chuki zaidi miongoni mwa wananchi wa visiwani.
Na wenye kutaka kutenda dhambi hii, wasije wakashangaa pia watakavyokataliwa na Watanzania walio wengi , wa Bara na Visiwani, wasiopendezwa na matendo yao hayo.
Maggid Mjengwa,
http://mjengwablog.com
0754 678 252