Tafsiri ya usemi "Wanaume wa Dar"

A.J

Senior Member
Jun 9, 2015
139
147
UFAFANUZI KUHUSU NENO WANAUME WA DAR

Wanaume wa Dar ni tabia haijalishi unaishi wap, mfano we mwanaume :-

1. Unaishi Tabora ndani afu unamtext mwanaume mwenzako una mwita My, dear etc., wewe pia ni mwanaume wa Dar.
2. Unaishi Mwanza ila wimbo wako bora ni "ninogeshe" ya nandy, we nae ni mwanaume wa Dar‍♂‍♂
3. Uko Arusha ila unakula soda na biscuits unashiba na kulala kabisa usiku, wewe ni mwanaume wa Dar.
4. Unaishi Kigoma ila TV show unazoangalia ni Shilawadu, Chereko na Ng'aringa'ri, wewe ni mwanaume wa Dar.
5. Unakaa mbeya ila unaagiza chips yai afu unakazia iwe na tomato nyingii, we ni mwanaume wa Dar.
6. Uko Iringa ila unachatt kwa kuandika x badala ya s, lmao, lol wewe ni wa Jiji la Makonda
7. Unaishi Singida ila umemfollow Bob Risky, James Delicious na Kaoge, wewe ni mwanaume wa Dar, tena Uwanja wa Fisi.
8. Unaishi Musoma ila una dressing table ndani, wewe ni mwanaume wa Dar.
9. Unaishi Simiyu ila uktoka kuoga unavua kila kitu ndiyo upake mafuta, wewe ni mwanaume wa Dar.
10. Unaishi Mtwara ila unaweka status picha ishirini, wewe ni mwanaume wa Dar.

Amani iwe nanyi wanaume wa Dar mlioko mikoani.

COPIED
 
Kumbe wewe wa darisalama moto
Mambo haya ni utani mkuu, kwani wakaazi wa Dar es Salaam si wapo mchanganyiko?

Mfano mimi nilishakaa Dar vipindi viwili tofauti, mikoani pia nimekaa na ndio nimezaliwa kijijini

Tanzania ni yetu sote mkuu na Dar es Salaam kuna makabila yote tena wengine wanaingia na kutoka kila siku
 
Watu wanapotoshana, fanya enquiry fupi sana, hili neno lilizaliwa kinywani mwa watu ambao ulimwengu wao ni wa nyuma sana, au hawana hela (wakijiita wagumu), watu wasiotaka kubadili muelekeo wa maisha yao, watu wanaodhani maisha ya kimaskini ndio stahiki Ya maisha ya mwanamume
 
Though baadhi ya yaliyotajwa hapo ni mienendo ya watoto wa kike kwenye ulimwengu wa wanaume. wapo wanaume wanaofanya hayo mambo, sio tu maeneo ya mjini, kuna mahala kunaonekana kwa WAGUMU, tembelea ARUSHA
 
Back
Top Bottom