Tafsiri ya usaliti ya Zitto na umaarufu wa kibuzwagi

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Tafsiri ya usaliti ya Zitto na umaarufu wa kibuzwagi

Prudence Karugendo

WIKI mbili zilizopita niliandika nikiishauri CHADEMA ifanye mambo yake kichama na si kimitandao. Nikaonyesha tofauti kati ya chama cha siasa na kikundi cha wanaharakati.

Sasa nimefarijika sana kuona CHADEMA inafanya mambo yake kichama, kwa maana halisi, ikiwa imejitofautisha na kikundi cha wanaharakati. CHADEMA imefanya maamuzi magumu kama chama kilichokomaa kwa kuwavua nyadhifa waliokuwa viongozi waandamizi wa chama hicho bila kuujali umaarufu waliokuwa nao ndani ya chama hicho.

Sababu umaarufu wa mtu mmoja mmoja ni tofauti na nguvu ya chama, maana yake ni kwamba, kwa watu binafsi, umaarufu ni wa wahusika ndani ya chama, na kwa chama, nguvu ya chama inajengwa na wanachama wote katika umoja wao ambao ndio wenye chama. Kamwe vitu hivi viwili haviwezi kutunishiana misuli.

Waliovuliwa nyadhifa ni Kabwe Zubeir Zitto, maarufu kama Zitto Kabwe, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Dk. Kitilla Mkumbo, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, na Samson Mwigamba, aliyekuwa mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha.

Watu hao watatu wamevuliwa nyadhifa zao kutokana na kufanya usaliti na uhaini ndani ya chama. Kilichothibitisha usaliti na uhaini wao ni waraka ulioandaliwa kwa siri, unaoelekeza namna ya kufanya mapinduzi ndani ya chama. Lakini waraka huo ukaja kufumaniwa na wataalamu wa chama na baadaye kuwekwa mikononi mwa viongozi wa chama.

Ndani ya kikao kilichowavua nyadhifa viongozi hao hawakusema lolote lenye kupingana na hukumu iliyotolewa, sana sana Zitto alikiri kuwa chama kimefuata utaratibu wake. Kwa ufupi ni kwamba walinyamaza, na kawaida ya mashtaka kunyamaza ni kukiri kosa.

Lakini baada ya siku tatu wavuliwa nyadhifa hao wakapata nguvu ya ziada iliyojionyesha kwamba ilikuwa na msukumo kutoka nje ya chama, wakazungumza na waandishi wa habari.

Picha ya msukumo huo ilijiweka wazi baada ya watu wasiojulikana wala kutambulika ndani ya CHADEMA, wakiwamo Wana UVCCM kuonekana ndio waratibu wa mkutano huo!

Katika makala hii nitamuangazia zaidi Zitto kutokana na sababu maalumu. Utetezi wa Zitto alioutoa katika mkutano ule, badala ya kuutolea kwenye kikao cha chama kilichomvua nyadhifa, kumbuka wanahabari si waliomvua nyadhifa, ulikuwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa asingeweza kukisaliti chama alichokitumikia kwa zaidi ya nusu ya umri wake.

Utetezi wake huo moja kwa moja unahalalisha madai yaliyomwandama mpaka akavuliwa nyadhifa zake kwenye chama. Sababu usaliti au kusaliti ni kitendo cha kwenda kinyume cha mwenendo mzima ambao mtu anakuwa ameapa au kuaminisha wengine kuwa ataufuata.

Anayotuhumiwa na kushutumiwa nayo Zitto yako wazi kama nitakavyojaribu kuonyesha hapa chini.

Kwa vile Zitto anasema mwenyewe kuwa ameitumikia CHADEMA kwa zaidi ya nusu ya maisha yake, halafu baadaye akaonekana anakwenda kinyume cha mwelekeo wa chama chake, hata kama kinakoelekea hakufai, basi akubali kuwa amekisaliti.

Mfano, CHADEMA haiwezi kusema kwamba Mwigulu Nchemba kaisaliti, sababu yule yupo kuhakikisha kwamba CHADEMA inaporomoka na kuangamia, naye anajigamba hivyo. Kinyume chake ni usaliti kwa chama anachokitumikia, CCM.

Kinachoweza kulalamikiwa na CHADEMA kutoka kwa Mwigulu ni uvamizi na si usaliti, ila kwa Zitto ni usaliti.

Kwa hiyo wale wote walioyumbishwa na kauli ya Zitto ya kwamba asingeweza kuisaliti CHADEMA, waelewe kuwa aliitoa kauli hiyo ili kuwafurahisha waandaaji wa mkutano wake huo bila kuifanyia tafakuri tafsiri ya neno usaliti.

Tukirudi nyuma kidogo, ni kwamba Zitto alikuwa ametokea kupata ushabiki mkubwa ndani ya CHADEMA, baadhi ya wanachama na wapenzi wa chama wakampenda sana na kujenga imani naye. Ikafikia wakati hata yeye akaanza kujiona kuwa ndiye CHADEMA na CHADEMA ndiyo yeye!

Hivyo akaanza kujiona kuwa yeye ndiye anayekipatia chama umaarufu. Kwa hiyo umaarufu wake akauona uko juu ya umaarufu wa chama. Hapo ndipo Zitto akanikumbusha wimbo wa Kihaya wa "Nkurukumbi niyo yazaire Mahinja", unaomaanisha kwamba mwanamke mlemavu asiye na miguu wala mikono kutokana na ugonjwa wa ukoma, ndiye mama mzazi wa mrembo aitwaye Mahinja.


Kwa hiyo usimpige wala kumtukana kama unamtamani Mahinja. Hebu tuangalie nyuma tena ili tukajikumbushe ukweli ulivyo. Umaarufu wa Zitto umeanzia bungeni akiwa mbunge kwa tiketi ya CHADEMA, pale alipouvalia njuga mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Baadaye alisimamishwa vikao vya Bunge kwa kilichodaiwa kwamba alilidanganya Bunge, Julai 2007.

Buzwagi, neno la Kisukuma lenye asili ya Kisumbwa, lina maana ya mambo yanayojitokeza kwa kuchipua bila mpangilio ulioratibiwa. Pengine mvua zimenyesha na majani kujiotea, basi majani hayo ni buzwagi. Kwa hiyo hata Zitto, kwa umaarufu alioupata kutokana na mkataba wa mgodi wa Buzwagi ambao alikuwa hakuupanga yeye, ni umaarufu wa kibuzwagi. Umaarufu uliojitokeza bila yeye kuutafuta.

Ni kwamba baada ya Zitto kufukuzwa bungeni, chama chake, CHADEMA, kilimbeba mgongoni na kumzungusha karibu nchi nzima kikiyataja aliyoyasema na kumsababishia kufukuzwa bungeni.

Hivyo CHADEMA ikawafanya watu wamuonee huruma kijana aliyeonekana ni jasiri, huku wakichanga na wengine kuahidi kumchangia pesa kwa ajili ya kufidia mshahara na posho alivyovikosa kwa kipindi chote alichokuwa nje ya Bunge. Kwa maana hiyo ni CHADEMA iliyompatia Zitto umaarufu tofauti na yeye anavyotaka kuwaaminisha watu kuwa amekipatia chama hicho umaarufu. Yeyote anayeuelewa umaarufu wa Zitto kabla ya hapo aueleze na aseme alishaifanyia nini CHADEMA kilicho zaidi ya wanachama wengine.

CHADEMA imemjenga Zitto na kumpa umaarufu mkubwa uliouzidi uwiano wa umuhimu wake, umaarufu wa kibuzwagi, ikitegemea matokeo makubwa zaidi kutoka kwake. Lakini kinyume chake zikajitokeza tuhuma na shutuma lukuki dhidi yake, zikiwamo za yeye kukikosesha chama hicho, tena kwa makusudi, zaidi ya majimbo 50 ya uchaguzi. Hizo ni tuhuma na shutuma za kukisaliti chama.

Mbali na tuhuma zinazohitaji mlolongo mrefu kuzithibitisha, zipo tuhuma za wazi kabisa kwamba Zitto alikuwa na zaidi ya miezi saba bila kukanyaga kwenye ofisi za makao makuu ya chama chake wakati akiwa Naibu Katibu Mkuu!

Je, hilo linaleta picha gani zaidi ya picha ya usaliti? Rafiki yangu mmoja anayedai kuwa anapendelea kuongelea hoja bila kuwagusa watu wala kuwajadili, anasema alipousoma waraka unaotajwa hakuona mahali popote panapoonyesha usaliti wala uhaini.

Ni wazi kwamba mtazamo wake unakinzana na maelezo ya watayarishaji wa waraka huo waliokiri kwamba waraka husika ulikuwa wa siri. Kukiri kwa watayarishaji kuwa waraka ulikuwa wa siri tayari ni kukiri kuwa ulikuwa wa kihaini. Vinginevyo waraka huo ungekuwa wa wazi ukifuata taratibu zote za chama. Lakini usiri ulioufunika waraka huo hauwezi kuondoa shaka kwamba pengine ulikuwa unaandaa vikundi kwa ajili ya vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, kitu ambacho ni uhaini uliopitiliza.

Tutaona kwamba CHADEMA, kama ilivyokuwa ANC ya Afrika Kusini enzi za makaburu, ni chama kinachopata msukosuko mkubwa kutoka kwa watawala. Watawala wanakisakama chama hicho kwa njia zote hasa kwa kutumia nguvu za dola. Misukosuko hiyo wakati mwingine inaonekana imelenga hata kupoteza uhai, uwe wa wanachama, wapenzi na hata wa viongozi wa chama. Ni jambo la kushangaza kwamba karibu mara zote ambazo CHADEMA imepata misukosuko ya aina hiyo, mikubwa na ya hatari, Zitto huwa hayupo.

Nimepokea simu nyingi na ujumbe mwingi wa maandishi kutoka kwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA wa sehemu mbalimbali nchini wakiuliza kwamba; kwa nini karibu mara zote ambazo CHADEMA inakumbana na mabavu ya vyombo vya dola kiasi cha vyombo hivyo kupoteza uhai wa wananchi na wanachama wasio na hatia Zitto huwa hayupo?

Wanasema sehemu nyingi anazokuwapo Zitto huwa hapatokei patashika zinazosababishwa na mabavu ya vyombo vya dola. Wanazitaja sehemu kama Nyololo, Mufindi Iringa ambako viongozi wa CHADEMA walishambuliwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na kuishia kuuawa mwanahabari, Daudi Mwangosi, kwamba mbali ya kutokuwapo Zitto, hajawahi hata kwenda kutoa pole! Wanataja Morogoro ambako aliuawa muuza magazeti katika shambulio lililoonekana kuilenga CHADEMA, Zitto hakuwepo wala hakwenda kutoa pole. Wanataja Soweto, Arusha, ambako bomu lilirushwa kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA na kuua watu kadhaa, Zitto hakuwapo na wala hajawahi kwenda kutoa pole! Swali wanalojiuliza ni kwamba hiyo inatokea tu kwa bahati aliyo nayo Zitto au huwa anazo habari za kiintelijensia zikimtahadharisha asiende kwenye maeneo husika?

Yanasemwa mengi kwa wakati huu, mengine kwa nia njema na mengine kwa nia mbaya. Lililo la muhimu ni kuyatafakari maneno haya ili kuangalia ni lipi la kutilia maanani na lipi la kupuuza.

Mfano, kwa upande wangu sijawahi kumshabikia Zitto hata mara moja, maana mara zote nimeyapima aliyoyafanya kuona kama kuna alichowazidi wengine, lakini sijawahi kukiona.

Huwa namchukulia kama nilivyomwelezea hapo juu. Ni kwamba naamini kabisa kuwa umaarufu alio nao ni wa kibuzwagi, si umaarufu ulioratibiwa kutokana na juhudi zake binafsi, bali unaochipuka tu kutokana na hali ilivyo. Kwa maana hiyo watu wote wanaoyapenda mageuzi ingebidi wafanye tafakuri ili kumwelewa mtu huyu vizuri kabla ya kumwachia kuwapoteza kimkumbo.
 
Zitto could be the greatest and smart "double agent" this country ever produced.

Zitto is not easy!!!
 
Last edited by a moderator:
Dah! Huu msumari wa moto! Tafakuri hii imeshehezeza fikra nzito. abwe utajitanzua vipi? Kwa miezi saba, Naibu Katibu Mkuu hakuwahi kufika ofisini? Dah, hii ndio sababu tosha ya kunofua cheo hiki kwa huyu ndugu!
 
Tunakujua padre karugendo wewe ni mchumia tumno kupitia kwa mbowe, mwanachama supporter mtiifu wa padre mwenzako dk Slaa, ni lazima tu umchukie zito kwa sababu ya udini wenu unowasumbua, tunaomba muanze mchakato wa kumfanya mbowe na lema wenye heri.
 
Hapo Karugendo kasema ukweli,na kuna mengi zaidi ya hayo ambayo yanathibitisha picha ya usaliti wa ZZK.
 
Tunakujua padre karugendo wewe ni mchumia tumno kupitia kwa mbowe, mwanachama supporter mtiifu wa padre mwenzako dk Slaa, ni lazima tu umchukie zito kwa sababu ya udini wenu unowasumbua, tunaomba muanze mchakato wa kumfanya mbowe na lema wenye heri.

sasa mtu hajakanyaga ofisin miez saba nayo udini ngoja nikuache na single yako ya kingese hiyo ilio chuja
 
Tunakujua padre karugendo wewe ni mchumia tumno kupitia kwa mbowe, mwanachama supporter mtiifu wa padre mwenzako dk Slaa, ni lazima tu umchukie zito kwa sababu ya udini wenu unowasumbua, tunaomba muanze mchakato wa kumfanya mbowe na lema wenye heri.

Issue ya Zitto lumwagwa CCM ni kama vile mmepigwa msumari kwenye kidonda..lakini haishangazi sana kwani ndio kete pekee mliyokuwa mmebaki nayo,,Karugendo kaja na hoja yake jibu kwa hoja na sio kutuletea single ya udini mara ukabila etc , mambo ya udini, ukabila, & Uzanzibari mambo hayo yamekomaa ndani ya CCM na ukitaka kulijua hilo basi angalia kwenye CC ya CCM au angalia baraza la mawaziri wenu ambao wengi hawana sifa stahili bali wamepewa nafasi hizo kwa kuangalia udini na ukabila na wapi wanatoka, jambo hilo la kipuuzi kamwe halina nafasi ndani ya CDM na ndiko mtu wenu Zitto katika kutapatapa namwona anaelekea kwenye hoja mbofu mbofu
 
Tunakujua padre karugendo wewe ni mchumia tumno kupitia kwa mbowe, mwanachama supporter mtiifu wa padre mwenzako dk Slaa, ni lazima tu umchukie zito kwa sababu ya udini wenu unowasumbua, tunaomba muanze mchakato wa kumfanya mbowe na lema wenye heri.

Shambulia hoja siyo mtoa hoja.
 
Aluuuu...
Watakuja Lumumba team kuchangia maana wao wamekatazwa kuchangia Thread flan flan tofauti na hii...
 
Nimeisoma.He nailed it.Huyu ndio msomi

siku zako zinahesabika
unaishi maishaya mashaka
vijana wote wnakuogopa
umekaa kikikekike
haumaniki, unasemwa pembeni

umekubali kutumiwa
umepofushwa
upand wako umeonekana
sumu uliyobeba haijasahaulika
umenunuliwa

wewe si mwanamapinduzi tena
wewe si mfurukutwa
wewe si mjenga hoja
upepo umekuhcukua
umebeba akili yako na uwezo wako

njaa umekuuma
mbowe ukamsujudia
slaa ukamsikiliza
taifa ukalisaliti

demokrasia inakulilia
ww unaipiga teke
inalia, inapaza sauti

sauti yake kamwe haita nyamaa

hata kizazi chako cha nne

HISTORIA HII INAKUFUATA
 
Zitto kavunja katiba gani?

ni wapi alipoonyesha kuvunja ustawi naumoja wa chama??

karugendo, ulishakuw excommunicated kwenye society ya wenye akili
 
siku zako zinahesabika
unaishi maishaya mashaka
vijana wote wnakuogopa
umekaa kikikekike
haumaniki, unasemwa pembeni

umekubali kutumiwa
umepofushwa
upand wako umeonekana
sumu uliyobeba haijasahaulika
umenunuliwa

wewe si mwanamapinduzi tena
wewe si mfurukutwa
wewe si mjenga hoja
upepo umekuhcukua
umebeba akili yako na uwezo wako

njaa umekuuma
mbowe ukamsujudia
slaa ukamsikiliza
taifa ukalisaliti

demokrasia inakulilia
ww unaipiga teke
inalia, inapaza sauti

sauti yake kamwe haita nyamaa

hata kizazi chako cha nne

HISTORIA HII INAKUFUATA

Uchafu....Povu la Wasaliti waliojivisha kitanzi!
 
Katika hili sakata la Mh. MM, nimefurahishwa na jinsi watu makini na wazalendo, kutoka kada mbalimbali na itikadi tofauti-tofuati; walivyojitoa kuchambua na kujitokeza wazi wazi kutoa maoni yao na kwa wengi wao kuonesha CHADEMA kimachukua hatua sahihi na ya kuwa MM amefanya uhaini. Hili ndilo kubwa na la muhimu kwetu wananchi na CHADEMA kwa ujumla.
 
Tunakujua padre karugendo wewe ni mchumia tumno kupitia kwa mbowe, mwanachama supporter mtiifu wa padre mwenzako dk Slaa, ni lazima tu umchukie zito kwa sababu ya udini wenu unowasumbua, tunaomba muanze mchakato wa kumfanya mbowe na lema wenye heri.

Utaheshimika Zaidi kama nawe utatoa uchambuzi wako kuliko kusema tuna kujua bila kutoa uchambuzi wako
 
Back
Top Bottom