Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Zinaongea kitu gani sasa? Kwanini hao walionyanyua mikono miwili juu wasingekufa wao? Au kwanini hao ambao mkono mmoja uko chini mwingine juu (JK na Ben) wasingekufa hao??

Hakuna ukweli wowote kwenye unavyovisema, ila hizo vitu vinatafsiriwa tu baada ya matukio kutokea. Ndio maana mnaishia kutafsiri tu mara wa kati ndio wamekufa, mara wa kulia na kushoto, mara wamekufa kwa kufatana mtililiko kwa jinsi walivyojipanga mstari n.k
Watu ni wajinga sana, na mwingine humu anasema aandike kitabu juu ya hili Yan nimecheka kwa dharau.
Watu hawana wigo mpana wa kufikiri ujinga umetawala
 
Watu ni wajinga sana, na mwingine humu anasema aandike kitabu juu ya hili Yan nimecheka kwa dharau.
Watu hawana wigo mpana wa kufikiri ujinga umetawala
😂😂😂😂😂 Kwamba jamaa aandike kitabu wanunue..

Huyu jamaa anawapiga sana fix humu. Watanzania tuna safari ndefu sana, hatutaki kushughulisha bongo zetu kabisa
 
Habari kaka Mshana,

Hizo ni coincidence tu hazina uhusiano na nguvu wala miujiza yoyote kila jambo ni vile unavyolitazama, mimi sikubaliani na wewe.

Kama picha ilipigwa zamani kivipi leo niione sawa wakati nyakati zinabadilika? ni lazima nione mabadiliko mengi tu kwa kua muda nao umepita ipo hivyo tu.

Nikipiga picha leo na mbuzi wangu nyumbani baada ya miaka mitano yule mbuzi hatakuwepo labda amechinjwa au vyovyote na mimi pia nitakua pengine kama asili ya maisha ilivyo hakuna nguvu wala nini inayotumika hapa.
Hujaelewa, hoja ya Mshana Jr
 
Picha zinaongea, picha zinaishi picha zinatoa ujumbe maalum usioonekana kwa macho ya kawaida mpaka wakati ufike

Ukipata muda chukua album yako ya picha pitia picha za zamani ulizopiga na marafiki ndugu jamaa na hata watu usiowafahamu

  • angalia mpangilio wa jinsi watu walivyosimama au kukaa nk
  • angalia mpangilio wa rangi au mavazi
  • angalia body language

Kwa mshangao wa ajabu utakuta kwenye picha fulani watu fulani waliosimama pamoja siku huyo au kuchuchumaa au kuvaa nguo za aina moja nk

  • wote wamekufa
  • wote ni matajiri
  • wote wameoa/wameolewa nyumba moja
  • wote tabia zao zinafanya nk

Kwa mshangao mkubwa angalia body language utajikuta unaona kabisa hao

  • walikuja kuoana
  • walikuja kuwa maadui wakubwa
  • walikuja kuwa marafiki wa damu nk

Tunapojipanga tupige piga na kubadili badili mikao na nafasi si kwa akili zetu bali kuna nguvu nje ya ufahamu wetu nguvu ya kiroho ndio inafanya kazi

Ni nguvu hiyo inayoamua:

Usimame wapi na kwa nini
Ukae wapi na kwa nini
Ufuatane na nani na kwa nini
Umtazame nani na kwa nini

Ni nguvu ya uvutano kwenye ulimwengu wa roho inayotengeneza matukio yote haya na huja kudhihirika baada ya kipindi fulani kupita...haya yanatokea si kwa utashi wetu wala uamuzi wetu wala nguvu zetu

Sijapata picha nyingine lakini naomba kuweka hii

  • angalia mfanano wa rangi za mavazi
  • body language
  • nafasi kwenye kusimama
  • umbali na ukaribu

Unafikiri walipanga kwa makusudi huu mkao?

Lipumba na Slaa ni ndugu nini.
 
Back
Top Bottom