Tafsiri ya nguvu ya umma ni salamu tosha kwa watawala

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,109
People's power ni tafsiri kubwa Sana na nzito ambayo kwa macho ya kimwili huwezi kuitafsiri zaidi ya kutoa kejeli lakini kwa walioisoma ibara ya 8 ya katiba ya JM wakajua tafsiri ya sheria juu ya nguvu ya umma inayotoa mamlaka na madaraka kwa serikali wataelewa nazungumzia nini.

Leo hukumu ya kesi ya uchochezi iliyokuwa ina mkabili mwanaharakati na mwandishi wa vitabu Yericko Nyerere ilimtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya shilingi milioni 5,naye akachaguwa kulipa fedha hiyo kupitia nguvu ya umma.

Kama mtakumbuka,hukumu hii ina akisi kesi aliyo wahi kushitakiwa muasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu J K Nyerere na serikali ya kikoloni(sedition offense)

Hii ina dhihirisha wazi kuwa pamoja na mapambano ya kudai uhuru aliyokumbana nayo Mwalimu,bado serikali ya awamu ya tano kupitia bunge lake haikuona madhara ya sheria hii kandamizi ya kikoloni ambayo ina ondoa mamlaka ya kisheria ya ibara ya 18 juu uhuru wa majadiliano.

Moja ya contents za case hii ni pamoja na kuchochea kuandikwa kwa katiba mpya,kuujadili Muungano n.k.

Ukitafakari mamlaka tuliyopewa wananchi kwa mujibu wa katiba na ukizingatia maudhui ya hukumu iliyo mtia hatiani mshtakiwa Yericko utaona kuwa Tanzania hakuna soveregnity state na bado tupo chini ya utawala wa kikoloni,ambao mwafrika ana Mtawala mwafrika mwenzake kwa nguvu bila kujali takwa la kikatiba.

Muungano unaojadiliwa au kuunganishwa si wa vitu Bali ni wa nchi na nchi,ambazo nchi hizo zipo chini ya mamlaka ya wananchi. Unapo mhukumu mwananchi kujadili hatima ya nchi yake maanake umeinajisi katiba.

Fedha zimechangwa na wananchi walioguswa na wanaopinga mfumo kandamizi unao nyang'anya mamlaka ya wananchi kuamua hatima ya nchi yao. Zimelipwa milioni 5 ambazo zimechangwa na wenye nchi yao.

Maanake nini,hizi ni SALAMU tosha kwa Watawala wanaoamini nguvu ya dola. Lakini ni mwangaza tosha unaoakisi chuki na kutoiamini serikali yao juu ya dhuluma na ubadhirifu wa matumizi mabaya ya sheria.

Kesi ngapi za jinai watu wanafungwa kwa kukosa faini lakini wananchi hawaguswi kuchangia,serikali iliwahi kujiuuliza!!!!

SALAMU hizi ni SALAMU za ukombozi dhidi ya batili ndo maana wananchi wanachanga kwa hasira. Tusichukulie poa,pengo linalo tengenezwa baina ya serikali na wananchi ni kubwa Sana lakini pia si afya njema kwa mustakabali wa amani ya nchi.

Ni muhimu dola kujitazama kwa macho ya rohoni kwa kuwa hakuna dola yeyote duniani iliwahi kushindana na nguvu ya umma ikashinda,hivyo basi tusiishie kufurahia hizo penalty bila tafakuri ya kina.
 
Yaani kudai Katiba Mpya ni uchochezi! Kuhoji mfumo wa Muungano wetu nao ni uchochezi! Kama ni hivyo, basi kazi ipo. Wacha tu niendelee kujificha humu jukwaani kupitia ID fake.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom