Tafsiri ya mzalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri ya mzalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bnhai, Jul 14, 2009.

 1. b

  bnhai JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF, mzalendo nchini kwetu tunaweza kumtafsiri vipi? Kuna wengine tumekuwa tukitafsiri mzalendo kwa maana ya rangi na wangine kwa maana ya uzawa. (With ref kwa bwana Mengi tumekuwa tukimuita mzalendo but RA yeye si mzalendo tumemuita kwa majina mengi). Kwahiyo wale polisi Bukoba wanaochukua rushwa na baadae kuvamiwa na wananchi ni wazalendo? Au wale walihusika katika mauaji mbalimbali ni wazalendo? Nini hasa kinamfanya mtu aitwe mzalendo? Mie na wewe tunaitwa wazalendo? Wanasiasa? Uzalendo unapatikanaje?
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mzalendo ni mtu mwenye kuipenda nchi yake, kuwa tayari kuitumikia kwa moyo wote na kwa uadilifu hata ikibidi kufa kwa ajili yake. Kumbe mzalendo lazima awe kwanza mwanachi. Kila mzalendo ni mwananchi. Lakini si kila mwanachi ni mzalendo. Kuna wananchi ambao hawana uzalendo, yaani hawana upendo kwa nchi yao, na hawako tayari kuitumia ncho yao kwa moyo wote na kwa uadilifu.

  Kwa mantiki hiyo si kila mzawa ni mzalendo. Kama hana sifa za hapo juu hawezi kuitwa mzalendo. Na mtu asiye mzawa lakini ni mwananchi baada ya kupata uraia aweza kuwa mzalendo au si mzalendo kutegemea kama anakidhi sifa za hapo juu.

  Uzalendo wa mtu (au ukosefu wa uzalendo) haupimwi kwa tendo moja au tukio moja. Kuwa mzalendo au kutokuwa mzalendo lazima iwe ni tabia ya kudumu inayojionesha nje.

  Kwa wale askari waliopigwa, kama tabia yao ilikuwa ndiyo hiyo ya manyanyaso kwa raia, basi tunaweza kusema si wazalendo kwani hawana upendo kwa nchi na raia wake, na utumishi wao si wa kiadilifu.

  Thread hii imenikumbusha wimbo wa kizalendo tuliokuwa tukiuimba tukiwa shuleni: Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wotee, nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana . . . .
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Uzalendo ni matokeo ya historia iliyotukuka ya mwanachi kutetea ukweli na haki kwa faida ya nchi yake, kusimamia rasilimali au kutumia uwezo wake, cheo chake kwa faida ya nchi yake kwanza kabla hata ya kufikiri kujinufaisha. In relation with Mengi vs RA wote "Si wazalendo ila ni wafanya biashara wanaochumia matumbo yao kwanza na kutumia uwezo na nafasi zao kujinufaisha wenyewe na kugawa wananchi". Mfano wa mwananchi mzalendo ni kama vile Nyerere, Haroub othman, Prof Issa shivji etc. wanaonekana uadilifu wao kwa nchi yao na watu wake.
   
 4. b

  bnhai JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo mtu akijitokeza na kushout yeye mzalendo mbele ya wengine huwa ni kwa maslahi yake. Na tuorodheshe sifa za mzalendo.
  1. Muadilifu
  2. Mkweli
  3. Anapenda Amani na Ustawi wa Wananchi............................
   
 5. jicho la mnyonge

  jicho la mnyonge JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2015
  Joined: Nov 8, 2014
  Messages: 314
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  uzalendo pia ni kuwapa kipaumbele wananchi na wale wanaohitaji msaada kabla ya kuangalia maslahi binafsi , uzalendo ni matendo mema kwa nchi yako kwa kuifanyia uadilifu na haki mazingira yanayotuzunguka kwa mfano kufuata utaratibu muafaka uliowekwa wa kuvua samaki na sio kutumia mabomu kwa lengo la kupata samaki wengi kwa mpigo...au kuharibu mazingira kwa kuchoma moto misitu kwa sababu zozote zile au kuiba nyaya za umeme na mafuta ya transformer haya matendo sio ya kizalendo tabia hizi zimeshika kasi kubwa miaka ya hivi karibuni je tumeghafilishwa na kitu gani mpaka tukapoteza jambo hili la tunu...?

  Aliyekuwa kiongozi wa Marekani Rais Keneddy alipata kuwambia wamerakani , usiiulize serikali ikufanyie jambo lolote bali jiulize umeifanyia nini nchi yako...
   
 6. stanlthecreator

  stanlthecreator JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2015
  Joined: Jan 9, 2014
  Messages: 1,947
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa mantiki hiyo mojamoja list ya wazalendo ni kama hii hapa:
  1. Julius Nyerere
  2. Edward Moringe sokoine
  3. Proffsor Issa shivji
  4. Zito Kabwe
  5. Mchungaji Mtikila
  6. Chacha Wangwe
   
 7. d

  duanzi JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 16,455
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Zito Kabwe ndio mzalendo wa kwanza Tanzania
   
 8. T

  Tunkamanini JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2015
  Joined: Jul 18, 2014
  Messages: 376
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Zitto n mzalendo halisi kama mwl Nyerere
   
Loading...