Kwa kuwa spika kaamua kwa makusudi kupindisha katiba na kanuni za Bunge na akiwa na lengo moja tuu la kuuhadaa umma wa watanzania walioko nje kuwa kinachofanyika hakina mantiki, ila ni jambo tuu ambalo linafanywa na watu ambao hawana au hawajui utaratibu , ni mwongozo wa ajabu sana kuwahi kutolewa na Spika yeyote yule.
Katiba inachosema ni kuwa ili kuweza kumwondoa Waziri mkuu lazima hoja iwasilishwe kwa maandishi na iwe imeungwa mkono na wabunge asilimia 20 ya wabunge wote .Sasa jambo la ajabu la kwanza ni kuwa Spika hajapelekewa hoja mezani kwake na katika mazingira ya ajabu kabisa anatoa uamuzi wa jambo ambalo halijawasilishwa kwake kwani anapaswa alipokee kwa maandishi.
Mbili, alichofanya Zitto jana na kutoa tangazo kwa wabunge ambao wako tayari kupiga kura ya kumwondoa PM na hoja yake ilipaswa kuungwa mkono na wabunge kwa kusaini kuwa wanaunga mkono hoja ya kupiga kura ya kukosa imani na waziri mkuu. Sasa huyu Mama anaamua kutoa hukumu kwenye jambo ambalo halipo ni uamuzi wa ajabu kabisa na linaonyesha uwezo wake ulivyo mdogo katika kutazama mambo na kuweza kuyaamulia .
Tatu, hakuna Mbunge ambaye amesema kuwa kesho ndio PM anaondolewa , ila kwenye kanuni za bunge wameandika kwenye kifungu cha 133 (3) "hoja ya kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tuu kama ;
(a) "taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya wabunge wote itatolewa kwa Spika,siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni";
sasa kiherehere cha spika kutoa uamuzi wakati hoja haijawasilishwa kwake nini maana yake?
Kifungu cha (4) "Hoja inayotolewa chini ya kanuni hii na iliyotimiza masharti ya katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri"
sasa hapa kifungu hiki ndio naona kinamfanya mama kiti kisiweze kuenea kwani anatakiwa kuiwasilisha mapema iwezekanavyo na kama ataona kuwa mapema ni Bunge lijalo ama atapaswa kuitisha Bunge hapo ntawaachia magwiji wa sheria waweze kuliongelea maana , kama hatafanya hivyo, hivi PM ambaye wabunge hawana imani naye atapaswa kupisha mpaka kura iamue ama ataendelea kukalia kiti? Hapa ndipo penye presha kwa mama na wabunge wa CCM.
Huu ni sehemu ya ushahidi mkubwa kuwa Spika wa Bunge huwa hafuati kanuni katika kufanya maamuzi yake , na hivyo anapaswa na yeye kufanyiwa kazi kwa mujibu wa kanuni za bunge kifungu cha 134 ambacho hakihitaji hata saini za wabunge ila ni mbunge mmoja kuwasilisha taarifa hiyo na hatimaye atapigiwa kura na theluthi mbili ya wabunge.
Nafikiri, kuna haja sasa kwa wananchi wetu kila mmoja akawa anawaelewesha kuhusiana na kanuni na sheria mbalimbali ili pindi wanapopotosha basi wakutane na wananchi ambao wanaelewa