Tafsiri ya mnyumbuliko maizi kizani ni tofauti na uhalisia nuruni

.
Teresa-Esposito__Oscurita_g.jpeg

Jr
 
Kuna vitu tunaviona ni vidogo sana maishani na hatuvipi umuhimu wowote, lakini vimebeba maana kubwa sana nyuma yake
Wenzetu wenye kuwaza zaidi ya kuwaza wamevifuatilia, kuvifanyia utafiti na kupata majibu ya kushangaza mno.....
Uhalisia wa mwanadamu kizani ni picha pindu ama ni kinyume na uhalisia wa nuruni... Yaani kwenye macho ya gizani.. Tafsiri pana zaidi ni rohoni picha asili inayokuja kwa mara ya kwanza ni picha ama umbo pindu ama picha kinyume...

Mboni ya jicho ambayo kiuhalisia ndio taa iletayo mwanga wa uono picha ama umbo la asili linaloikamata ni picha pindu ama ama umbo kinyume... Na baadae taarifa hupelekwa kwenye medulla na kurekebishwa... Lakini hapa itategemea mboni iko kwenye uono gani... Wa kizani ama nuruni? Kama ni wa kizani basi medulla itajitahidi kurekebisha taarifa husika ili mambo yaende sawa... Kitu ambacho ni kigumu mara nyingi.. Lakini kama ni kwenye uono wa nuruni basi automatically kila kitu kitaenda sawa
Mifano ipo mingi na hata sasa asubuhi hii ukijiandaa na mishemishe unaweza kujaribu... Kumbuka uono wa kizani si lazima kuwe na kiza la hasha bali hata kufumba macho ni uono wa kizani
Sasa basi fumba macho kisha sogelea kabati lako la nguo ukiwa na nia ya kufungua mlango wa kushoto ama kulia... Ukishaushika fumbua macho utajikuta umeshika ambao sio... Mara chache mno watu hupatia...
Huo ulikuwa ni mfano mmoja tu lakini kuna nguo, vidani, viatu nknk... Ukikivaa gizani lazima utakosea kwa tafsiri ya macho ya nuruni... Kama ni nguo utageuza nje ndani ama nyuma mbele, kama ni saa hivyo hivyo nknk
Vitu vichache ambavyo hutakosea ni vile vyenye alama maalum kama kofia za kapelo, viatu nk...
Hapa tunapata nini? Hapa tunapata dhana mbili au tatu hivi...
. Ufahamu wa uono kiroho ni tofauti kabisa na ufahamu wa kimwili nuruni
. Asili ya matendo yetu tafsiri zake na fikra tengefu hurekebishwa na kufanyiwa uwiano macho ya mwili yanapokuwa angavu nuruni
. kwamba kila kitu kiasili kina uwili usioshabihiana... Yaani juu/chini, hasi /chanya, kushoto /kulia, mbele/ nyuma nknk
Na ukitaka ithibati zaidi juu ya hili ni kwamba fumba macho kisha tembea... Utajikuta usipoenda kulia basi utaenda kushoto... Ni ngumu mno kwenda mstari mnyoofu ukiwa katika macho ya kizani... Kwa hiyo mboni za macho ndio kipima rada na kuleta uwiano usiokinzana na uhalisia.....
Tunapozungumzia jicho la tatu tafsiri yake halisi ni jicho la kiroho na ndio maana kuna baadhi huhoji wale wavutao bangi na kuanza kufanya vitu vya ajabu.... Hii hutokea kwasababu jicho la nuru linakuwa limezingwa hivyo basi
Penye kina kirefu baadhi ya wavutaji huona ni kirefu
Upande wa kushoto huona wa kulia
Mdogo humuona ni mtu mzima kabisa na shikamoo atampa
Mashimo madogo atayaona ni madimbwi makubwa anaweza hata aanze kuruka....
Hali hii hutokea pia kwa walevi ndio maana wengi huenda kulia ama kushoto
Hapa mnyumbuliko maizi/tambuzi unakuwa haufanyiwa mchakato wa utambuzi ili kuleta uwiano wenye uhalisia katika maisha... Hawa tunaowaita vichaa tatizo lao ni kufungwa kwa mboni ya jicho inayoleta uwiano kwa kurekebisha taarifa zote zitokazo kwenye chimbuko la uono.. Jicho la kizani ama jicho la rohoni....

Jr
Nondo zako mkuu hazijawahi kuwa nyepesi....endelea kutupa maarifa.
 
Wale ni walemavu wenye namna nyingine ya kuweza 'kuona'

Ok so sio lazima uwe na macho ya Nuruni ili ung’amue mambo yaliyopinduka.
Ndio maana tukapewa milango ya fahamu tofauti ili kusaidiana katika ung’amuzi. Waweza usione ila ukasikia sauti na kung’amua jambo au usisikie, usione ila ukaonja na kung’amua jambo.
Hata hivyo nakubaliana nawe ktk hoja yako, nilikuwa nachangia tu wazo mbadala
 
Asante sana..mchango wako ni mzuri na nimeuelewa utali

The best an effective way that has no side effects ni meditation pekee... But how many knows about it... How many can be ready to practice?

Jr
Hapa napata shida kidogo, nimekusoma sehemu, unaweza kuwa jicho la tatu ni kwa watu maalum, siyo kila mtu anaweza kulitumia. Meditation ni kuamsha jicho la tatu, is it practicable to any person? Can any person perform it? Natamani Sana niijue Meditation Mshana, guidance, if any, please.
 
Hapana si kwa watu maalum ila kuna ambao wana kipawa asili, kuna wepesi wa kugain kwa haraka na kuna wengine mpaka wajikunje hasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom