Ndugu zangu,
Tafsiri yake; Kilichoangaliwa na Majaji si matokeo , bali mchakato wa uchaguzi. Kwamba mchakato ulikuwa batili. Na ilivyo, mchakato unaweza kuathiri matokeo.
Kenya imethibitisha kuwa Mahakama ni kimbilio la mnyonge na mwenye nguvu. Ndivyo inavyotakiwa iwe. Raila Odinga alionekana kichekesho na wale waliokuwa wakiamini kuwa Afrika mgombea aliye madarakani akishinda ni kujisumbua kwenda mahakamani. Hongera Sana Kenya kwa kuionyesha dunia kuwa Afrika uhuru wa Mahakama upo, na kwamba anayeshindwa uchaguzi kama anaona hakutendewa haki aende mahakamani, na si kuandamana na kufanya vurugu.
Maggid,
Iringa.