Tafsiri ya Kujivua Magamba CCM inapotoshwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri ya Kujivua Magamba CCM inapotoshwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LINCOLINMTZA, Apr 29, 2011.

 1. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF, Nimekuwa nikifuatilia tafsiri ya kujivua magamba kwa CCM ndani ya jamvi letu, naona wengi wetu tunaangalia kwa mtazamo wa hasi sana.

  Mwenyekiti wa CCM taifa, Mh JK alitangaza rasimi kuwa CCM inahitaji kujivua gamba lake tarehe 5.2.2011 katika sherehe za CCM zilizofanyika Dodoma. Lengo lake lilikuwa ni kukibadilisha Chama Cha Mapinduzi ili kiwe na mvuto zaidi kwa wananchi. Na hilo halikupata publicity sana.

  Katika vikao vya NEC na CC, CCM iliamua kuvunja sekreteriati nzima iliyokuwa chini ya Yusuph Makamba, uamzi ambao ni mngumu kwa kweli ikifuatiwa na kuwataka wanaodaiwa mafisadi kuchukuliwa hatua kama kuvuliwa nyazifa ndani ya chama. Haya maamuzi ndo yaliyopata publicity kubwa sana.

  Pamoja na mambo yote hayo, wanajamvi wengi wamekuwa wakitoa tafsiri tofauti kwa kile JK alichokisema "Kujivua gamba" kwa kulinganisha na nyoka na kusahau kwamba huo ni msemo wa kiswahili wa kawaida kabisa. Mimi nafikiri tujadili zaidi lengo la kujivua gamba kwa taifa na siyo kuwa na tafsiri ya kila mtu bila kujali ushambiki.

  Kama mtu hajaelewa maana ya kujivua gamba kwa CCM, ni vizuri kuwauliza wao wenyewe waseme walikuwa wanamanisha nini kisha tujadili ujumbe na siyo tafsiri potofu. Naomba kutoa hoja.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu umeeleweka sana na hongera kwa kuhighlight huku kuingizwa kwa maono hasi na wapinzani wa CCM juu ya kujivua gamba.

  Nilivyolielewa maana halisi ya kujivua gamba ni marekebisho au reshuffle ndani ya uongozi.

  CCM imekuwa wepesi katika kufanya hivyo katika uongozi wake ingawaje hivi karibuni ilichelewa sana katika kufanya hivyo.
  Wale wa siku nyingi katika chama watakumbuka ule msemo wa KUNG'ATUKA wakati Mwalimu akiwa Mwenyekiti.

  Anayepoteza maana halisi ya kujivua gamba anafikiri it is a single move na umesafika!

  La hasha, it is a process na ndio maana tunaendelea kusikia gamba litaendelea kuvuliwa hadi ndani ya serikali.Kisiasa na hasa wasomi wa politika, this is a silent class struggle to gain the upper hand katika kuongoza nchi.

  Mafisadi, the bourgeoisie,wamejaribu kuiteka CCM ili biashara zao ziende vizuri.Katika hilo wameshindwa kwa sasa, na inaelekea watashindwa maana uchaguzi wa 2010 umeonyesha kuwa CCM isipowatema , na wao watakwenda na maji!!

  Kwa wanaofuatilia mageuzi haya ya kisiasa , this is a textbook example of social conflicts in society.

  Ndio maana kila nikiandika nauliza je msimamo wa CHADEMA ni upi katika hili?

  Hii ni kwa sababu hata CHADEMA wana wafanyabiashara wengi tu katika uongozi wao kama walivyo kina RA na EL na AC.
  Wakiipata nchi je kama the RACHEL group wataachia biashara zao? Tuna guarantee gani katika hilo.

  Hivyo basi kujivua gamba works both ways.
   
 3. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bure kabisa.

  Acheni watu wajadili kile wanachoona na maoni yao ni nini. Hii si karne ya kudanganya watu wazima wenye akili. Kinachofanyika ni mchezo wa kuigiza ndio sababu watu wanaweka tafsiri zao kulingana na wanavyoona kile kinachotokea na kujaribu kukipa maana.
  Vinginevyo tunataka tuone uhalisia wa matendo, watu waliofanya vibaya au makosa hatua zinachukuliwa.

  Vinginevyo maana zinazotolewa humu jamvini ni sahihi na zinawakilisha mawazo ya wananchi walio wengi pamoja na wanachama wa chama hicho cha magamba.
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Kwa CCM Kujivua gamba ni kuwafukuza RA EL na EC full stop. Acha blah blah wewe
   
 5. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kijiko na Uma kiko palepale, hizo nyingine ni kachumbari. Period.
   
 6. kitungi

  kitungi Senior Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  lipi ni tatizo kati ya haya kuwa na wafanyabiashara kwenye chama au kuwa na wafanyabiashara -mafisadi kwenye chama, naomba unieleweshe kidogo coz sijakuelewa hapo kwenye RED!
   
 7. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wazembe wa kufikiria kama wewe hukimbilia miamvuli ya kujificha (defensive mechanism) bila kuchosha akili zao. Kwa nini usijadili hoja iliyopo mezani?
   
 8. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani wana CDM nini maana ya kujivua gamba?..msije mkajifanya mnajua maana kumbe hamjui chochote, tuanzie hapa.
   
 9. k

  kayumba JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Maana ya kujivua gamba wengi tunaichukulia kama CCM walivyoteeleza na wanavyoendela kutueleza!

  Kuanzia siku ya kwanza by JK, kufuatiwa kikao cha UVCCM, CC NEC na mikutano ya sekretarieti mpya!

  Nafikiri wote tunapata maana ya kujivua gamba!

  Usishangae kwanini wengi hawaelewi, ni kwasababu CCM haitendi jinsi mjivua gamba ambavyo angepaswa kutenda....!
   
 10. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwani haya niliyoandika ni maoni yako wewe? Haya ni maoni yangu ambayo mimi naona ni sahihi kuyawakilisha hapa jamvini yajadiliwe. Kwa hiyo wewe unawasemea wengine? Usifikiria wanajmvi wote wanamawazo (maoni) kama yako. Toa maoni yako siyo ya wengine na wala usihukumu watu hapa kwani sikujui na hunijui.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu umeliweka point blank, mfanyabiashara ni mtu anayefanya kazi kwa faida katika kila jambo, na hatakubali apate loss kama fursa anaziona zipo wazi.

  Kuna a very fine line kati ya mfanyabiashara na mfanyabiashara fisadi.

  Fisadi ni yule ambaye ulafi unazidi kuliko kiwango na decision zote anazofanya ni kwa kuendeleza ulaji/biashara zake.

  Sasa mfanyabiashara fisadi akiwa kwenye decision making body maamuzi yake ya kisiasa na kimuelekeo ni katika kupendelea biashara zake na si vinginevyo.

  Mifano iko mingi katika hili na hatuna nia ya kuirudia maana imejadiliwa mara nyingi humu jamvini.

  Vile vile mfanyabiashara, mlipa kodi hana tatizo lolote na serikali na anawekeza-huyu huwezi kumuita fisadi. Tatizo kubwa sana ni mfanyabiashara anayeingia siasa, active politics.

  Biashara na active politics, hivi vitu haviendi pamoja hasa katika siasa zetu za kiafrika. Na hapo nielewe sina maana kuwa wafanyabiashara wasiwe wanachama vyama, nina maana active politics zinazoishia kuwa executive katika fani yoyote.
   
 12. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Kitungi, Wafanyabiashara wengi kama siyo wote duniani ni walafi wa mali. Wao huangalia maslahi yao zaidi na si ya watu wengine.

  Mara nyingi hutoa ushirikiano pale wanapoona kwamba wanaweza kupata kitu. Yaani kwenye upenyo penyeza lupia. Kwa hiyo usiyapuuzie hayo yanayosemwa kwani yanawezekana kwani ndo yanayoisumbua CCM sasa hivi. Kitu ambacho mwl. JK Nyerere alikiepuka sana.
   
 13. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kipindi Zuberi alitaka kujaribu kumvua gamba mwenyekiti na pindi babamkwe wa mwenyekiti alipopata habari, Zuberi alijuta kujaribu....kuvua magamba/magwanda kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
   
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Likes na Thanks zimepotea kabisa hapa lakini zipokee tu mkuu kwa njia ya analog communications
   
 15. m

  mkulimamwema Senior Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa jamaa wanajua vichwa vya JF kuwa vinajumuisha wataalam wa fani mbalimbali na hilo limewapa ccm tumbo joto hata Msekwa kuamua kuongea baada ya ukimya mrefu.

  CCM hawana jipya ED mwaka jana akihojiwa na TBC alisema urafiki wake na JK ni wa muda mrefu na wa kushibana na si wakukutana mitaani leo ndio ccm inamtuhumu kuwa mwizi au fisadi vipi rafiki wa mwizi asiondolewe maana hawezi kula vya wizi na asiwe mwizi hivyo kujivua gamba ni unafiki wa ccm kushindwa kumwambia mwenyekiti wao kwamba naye ni GAMBA na kuelekeza fitina kwa wezi wadogo huku mkuu akibaki ila sisi wana jamii tutaelimisha umma na kuwaambia ukweli wa mambo ccm na serikali yao na wakibeza ukweli wasubiri 2015 pia wajiulize kwanini matamko yao hayaungwi mkono na wananchi wengi hata wanaccm wenyewe.

  Angalia idadi ya wanaccm waliojitokeza kuwapokea MAGAMBA mapya ni ndogo sana kwa chama kikongwe kama CCM.

  Linganisha na matamko ya ukweli ya Mwl NYERERE yalivyoungwa mkono na watanzania mfano Azimio la Arusha mpaka leo wananchi wanalitaka kauli ya MAGAMBA haitadumu hata mwaka 1 ziko wapi za MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, KILIMO KWANZA, HAMSINI KWA HAMSINI na KASI MPYA NGUVU MPYA NA ARI MPYA wapi uongo mtupu wanajamii sisi tungekuwa chama cha siasa.

  Hawa jamaa wangepata shida maana tuna majibu yote ya kuzuia rushwa, upotevu na wizi wa mali za umma, ubora wa elimu na afya, huduma nzuri ya umeme, uongozi bora namna ya kuondoa umaskini wa watanzania yote haya wameshindwa ila wanataka tuwapigie makofi na kuwasifia mi siwapigii labda ccm wenzao wasiojua kusema ukweli
   
 16. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  Tanzanians are always Carried away by funny vocabularies.

  1. JIRUSHE
  2. CHIZIKA
  3. JIACHIE
  4. MZUKA
  5. KUJIVUA GAMBA
  6. KIINTELIGENSIA
  -------------
  -----------
  -----------
   
 17. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu ulitaka kuandika hapa lakini naona unazunguka zunguka, andika tuu mkuu,.
   
 18. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 533
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Hao wamekuja kutetea hoja yao ya kujivua gamba ili ccm iwe na mvuto kwa wananchi, lakini wananchi kwa wakati huu hawapigwi changa la macho, ndio maana wanaanza kuchombeza kwa tafsiri tofautitofauti wakisingizia kwamba wananchi hawajaelewa tafsiri ya kujivua gamba.

  Wananchi wamepiga makelele wakiongozwa na wapigania uhuru wa kweli wa Tanzania siku zote kwamba ufisadi upo ndani ya CCM na ndio unaoleta umasikini wa Mtanzania, ccm mara zote wamakataa katakata na hata m/kiti wa ccm kusimama na mafisadi mbele ya watanzania nakuwaambia ni wazalendo safi yanayoongelewa ni majungu tu, leo hii utamwambia Mtanzania huyohuyo tunatoa mafisadi kwenye chama?

  Hayo yote ni makelele tu ambayo hayamsaidii mwananchi. ccm wakubali na kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadanganya siku zote kwamba sio chama cha mafisadi.

  Mafisadi wote warudishe mali zote walizoiba kwa wananchi wakiongozwa na m/kiti wao na washitakiwe. Hapo ndipo maana ya kujivua gamba itaeleweka, vinginevyo mnapiga kelele za mfa maji, Wananchi sio rahisi kuwaelewa.
   
 19. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  kasi mpya...
  nguvu mpya...
  kasi zaidi....
  hali mpya......
  hayatofautiani sana haya na kujivua gamba kwa maana ya wanaccm
  mwenye macho haambiwi ona na mwenye akili haambiwi fikiri mwisho wa siku kila kitu kipo waziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 20. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Embu waache hawa mambo yao ya kujitia wanapotoshwa kimaana hata kwa maana ya kwao wao ya kujisafisha hivi toka wamesema mafisadi watoke mbona hatuoni hata mmoja akitajwa hadharani kana kwamba hawawajui? tungeamini kweli kuwa maana yao ni ya kweli endapo wangesema jamani tunajivua gamba haya fulani na fulani na fulani nyinyi mafisadi, umechukua moja mbili tatu, jamani tutabinafisha kwa manufaa ya uma na mahakani mtaenda ili iwe fundisho kwa wengine.

  Waache danganya toto ya kuturingishia pipi na hali wakijua hela ya kununyua hiyo pipi, hakuna gamba ni maneno tu na political manipulation kwa umma wa matanzania.

  Miaka itapita magamba yatabaki na kuota sugu nasi tusipokuwa raia wa kujua nini tunatakiwa kufanya tutabaki tunaringishiwa pipi na huku maisha yetu yanakuwa duni wachache wanaenjoy
   
Loading...