Tafsiri ya kufanya siasa imegeuzwa maana yake na Serikali hii na kuwa ni uchochezi na usaliti?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Ni ukweli usiopingika kuwa unapokuwa ni kiongozi wa upinzani nchi hii, hususani kutoka Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema katika serikali hii ya awamu ya tano ni sawasawa kuwa umetangaza vita na utaitwa majina mbalimbali mabaya kama vile wewe ni mchochezi na msaliti ambaye unatumiwa na mabeberu!

Hivi inakuwaje kufanya siasa za upinzani nchini ihesabike ni kosa la jinai wakati ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1) inasema wazi kuwa nchi hii itaendeshwa kidemokrasia na katika mfumo wa vyama Vingi??

Kila mtu anajua uendeshaji wa mfumo wa vyama Vingi ni kujibizana kwa hoja majukwaani na siyo kwa "ku-pyupyu" kama afanyavyo Jiwe, kwa kutumia msemo uliozoeleka kipindi hiki unaotumiwa na Jeshi letu la Polisi kuwa tii sheria bila shuruti!

Tunajua kuwa Katiba ya nchi haijaweka mipaka ya kufanya siasa nchi hii, sasa inakuwaje Jiwe atangaze kuwa mwanasiasa mbunge anaruhusiwa kufanya siasa jimboni kwake pekee??

Mbona mnaji-contradict nyinyi wenyewe kwa kuwaruhusu wanaCCM akina Dr Bashiru na Polepole kufanya siasa nchi nzima na huku mkimzuia Katibu Mkuu wa Chadema Dr Mashinji kufanya vivyo hivyo kufanya siasa nchi nzima??

Jeshi la Polisi mnaweza kuufahamisha Umma, je akina Dr Bashiru na Polepole ni wabunge wa majimbo gani hapa nchini??

Mbona mnakiuka maagizo mliyopewa na Rais kuwa viongozi wanaoruhusiwa kufanya siasa ni wabunge pekee tena kwenye majimbo waliyochaguliwa??

Kuna matumizi mabaya kabisa ya madaraka kunakofanywa na Jiwe chini ya mwamvuli wa u-kamanda-in-chifu

Hakika namna Jeshi la Polisi linavyopokea "maagizo" toka ngazi za juu ya namna ya kuwashughulikia wapinzani, hususani viongozi wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, italibomoa Taifa hili na kuhatarisha amani iliyodumu ndani ya nchi hii tokea tupate Uhuru wetu toka kwa mkoloni

Mungu ibariki Tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom