Kuna msemo unasema matendo huongea zaidi kuliko maneno.
Sasa hivi, kila kona ya nchi ni kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe. Wapo wanaosema kuwa kesi hiyo ya ugaidi dhidi ya Mbowe na Makomandoo wetu, ni ya kuwabambikizia. Wanasema hivi kutokana na mazingira ya hawa watu kupewa hiyo kesi, kukosekana kwa kiashiria chochote mpaka sasa cha kuashiria mipango na maandalizi ya ugaidi:
1) kwenye mipango - hakuna shahidi hata mmoja wa upande wa Serikali aliyethibitisha kulikuwa na vikao vya kupanga ugaidi namna utakavyotekeleza
2) kwenye maandalizi - hakuna shahidi yeyote aliyeonesha au aliyeleta zana zilizoandaliwa kutekeleza ugaidi.
Lakini hawa wote wanaosema kuwa kesi hii ya ugaidi ni ya kubambikiza, wanalalia kwenye maana ya ugaidi kama ilivyotafsiriwa kimataifa.
Lakini kwa tafsiri ya kimatendo ya Polisi, Serikali, CCM, na Rais wa Tanzania, maana ya ugaidi, uchochezi, na kuvuruga amani, vina tafsiri tofauti kabisa.
1) Ugaidi - kwa kuzingatia kauli za mara kwa mara za Polisi, na kauli ya Samia, bila shaka, gaidi ni mtu yeyote ambaye anapingana na kauli ya Rais. Yena Samia alifafanua vizuri sana maana ya ugaidi kwa tafsri ya Kitanzania, pale alipokuwa akijibu ombi la Zito, aliposema kuwa Mbowe hakumheshimu. Kwa hiyo kutomheshimu yeye Samia, ni ugaidi. Rais alisema kwamba suala la katiba mpya lisubiri. Mbowe akasema hatuwezi kusubiri. Kwa sababu Mbowe alipinga kauli ya Rais, hivyo ni gaidi.
2) Uchochezi - CCM imekuwa ikifurahia ujinga wa Watanzania. CCM inawaambia Watanzania ni matajiri, lakini wakati huo huo wapo wanaoshindwa kupata hata milo mitatu iliyo bora. Mtanzania yeyote anaweza kuwekwa ndani na DC masaa 48, halafu akakuachia. Huna hata pa kuhoji. Ukiwaambia wananchi kuwa hiyo siyo haki, wewe ni mchochezi kwa sababu watanzania wanatakiwa wabakie kwenye ujinga, kwa nini wewe unataka waondoke kwenye ujinga? Hilo ni kosa la uchochezi.
3) Kuvuruga Amani - kwa tafsiri ya kimatendo, kwa Tanzania, kuvuruga amani ni kuuweka ukweli mahali peupe. Ukweli unaohusiana na uchafu wa muundo mbaya wa utawala unatakiwa kufichwa. Ukisema kwamba mihimili miwili, yaani Bunge na Mahakama, ipo tu kinadharia, lakini kiuhalisia ipo kwenye kwapa za Rais kwa sababu Jaji mkuu anateuliwa na Rais, majaji wanateuliwa na Rais, viongozi wote wa mahakama huteuliwa na Rais, na huko Bungeni, Rais asipomtaka spika au mbunge yeyote atamfukuza kama alivyofanyiwa Ndugai au Tundu Lisu, wewe unahatarisha amani ya nchi. Kwa nini unayaweka mambo ya kweli hadharani, wakati kila mtanzania jukumu lake kuu alilolipewa kwa njia ya kificho ni kumsifia na kumwabudu Rais?
4) kuharibu Umoja wa Kitaifa - kwa tafsiri ya kimatendo ya CCM, Serikali, Polisi na Rais, umoja wa kitaifa, unakuwepo kama wote mkikubaliana kuishi katika ujinga na kuruhusu mtu mmoja tu kufikiri. Angalia umoja ulioopo ndani ya CCM. CCM, kwa utafiti wa TWAWEZA ndiyo chama kinachopendwa zaidi na wajinga. Na kutokana na kuwa na wajinga wengi, mshikamano wao ni mkubwa, na huo ndio umoja wa kitaifa unaotakiwa kuwepo. Sasa ukitaka wewe kufikiri badala ya kumsifu Rais na kuitikia tu NDIYOOOO, unahatarisha Umoja wa Kitaifa.
Kwa hiyo kwa tafsiri ya kimatendo ya CCM, Serikali, Polisi na Rais, Mbowe ni gaidi.
Kwa tafsiri ya kimatendo ya CCM, serikali, Polisi na Rais, wanaofikiri na kuhoji, wote hao wanahatarisha amani, umoja wa kitaifa, na ni wachochezi. Hivyo ni wahalifu.
Kuna machaguo mawili tú - moja ni kuukana utu wetu ili tusiwe magaidi, wachochezi, wavurugaji wa amani na umoja wa kitaifa; na ya pili ni kutii dhamira na utu wetu kama binadamu, dhamira zetu zinazoishi katika ukweli unaotambua kuwa:
1) kuwa Rais haimaanishi mtu ana akili na maarifa kuwazidi watanzania wote. Jukumu lake Rais ni kutengeneza tu mazingira ili karama, vipaji, maarifa na ujuzi wa watu mbalimbali, viweze kustawi na kutumika kwa manufaa ya nchi (mwili ni mmoja, viungo ni vingi).
2) polisi ni mlinzi wa raia. Polisi ni mwajiriwa wa raia, siyo mkubwa kuliko mwajiri wake. Mwajiriwa mjinga, muuaji, mbambikiaji kesi, mwongo, mporaji, anatakiwa kufukuzwa mara moja, iwe kwa hiari au kwa nguvu.
3) mwenye mamlaka ya kuweka mipaka ya mihimili ni mwananchi, na siyo Rais. Wananchi, kwa kupitia katiba, ndio wenye mamlaka ya kuweka ukomo wa kiutendaji na kiutawala wa Rais, Serikali, Bunge, Mahakama, DPP, DCI, Polisi, na ofisi nyingine zote. Mamlaka haya ni ya umma, siyo ya Rais. Anayekiuka au kuvuka mipaka ya katiba, bila ya kujali kama ni Rais, Jaji Mkuu au Spika, anatakiwa kufukuzwa mara moja.