Tafsiri ya Kiswahili ya Breaking News

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Vyombo vya Habari vinatuchanganya, Chombo kimoja kikasema, Breaking News ni Mpasuko wa Habari, hii ilikuwa wakati wa Kifo cha Ditopile, Redio Moja inasema Breaking News ni habari Mahsusi.

Lakini tunaona wengine wanasema Breaking News ni Habari Motomoto, kuna wengine wanasema hilo halifai, kwani Mfano habari iwe ya Majonzi utaiitaje Motomoto.

Wengine wanasema Habari Mpya na wengine Habari za Hivi Punde. Kuna Mkanganyiko hapa na naomba mwenye Tafsiri Sahihi ya Neno, Breaking News atufafanunulie.
 
Tafsiri sahihi ni Habari Mpya. Isipokuwa kwa lugha ya kiingereza maneno yanoyutumika yana weight na impact zaidi na yamezoeleka sana na hivyo yanaweza kumvuta msikilizaji zaidi. Hivyo kutufanya tuanze kutahayari kutafuta maana ambayo inaweza pia kuwa na impact kama hiyo ndio tunapojikuta tunaanza kutafsiri moja kwa moja (direct translation) kwa sababu ya athari za kisaikolojia kufikiri kwamba tukisema tu Habari Mpya haisisimui na kuwa na uzito ule ule. But other things are simpler than they sound.
 
'Habari mpya zilizotufikia sasa hivi hapa studio" waachane na mambo ya kuiga kila kitu cha wazungu wanataka kukitafsiri kwa kiswahili. Watafute maneno yao ambayo yatamfanya msikilizaji asikilize kwa makini. Na wakati mwingine hizo breaking news za CNN au BBC wala hazina uzito mkubwa unaostahili ziitwe breaking news
 
Back
Top Bottom