Tafsiri ya Kiingereza kwa Kiswahili kwenye Google | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri ya Kiingereza kwa Kiswahili kwenye Google

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Lucchese DeCavalcante, Jun 4, 2010.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nimejaribu kutafsiri kwenye google langunge tool imeleta kiswahili hiki nimecheka sana...


  When I stepped into the house I saw this very very beautiful girl with a wonderful smile I never stop starring at her

  Wakati i kupitiwa na ndani ya nyumba nikaona msichana mzuri sana sana na tabasamu ajabu mimi kamwe kuacha nyota saa yake
   
 2. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli google translate ni msaada kiasi lakini haiwezi kutafsiri. Kuna lugha kadhaa ambako matokeo ni afadhali kwa mfano kutoka Kiingereza kwenda Kifaransa, kijerumani au kihispania. Pale nimeona matokeo ya kitu kama 95 % sahihi - ambayo inaleta lugha baya hata kama inaeleweka kimsingi.

  Kimsingi mashine inachukua tafsiri neno kwa neno. Kwa lugha ndogo kama Kiswahili badi hawakuandaa bado nafasi nyingi kwa kila neno; tena wanahitaji mifano na sentensi nyingi sana za kulinganisha. Katika mfano wako inaonekana ya kwamba "at" imechukuliwa kama tangazo ya saa (at 5 o'clock) kwa hiyo wameingiza "saa yake" badala ya "kwake".

  Kwa lugha inayotumia misemo na nahau yaani lugha ya picha ni tena hatua nyingine kubwa.

  Kwa Kiswahili naona: google inaweza kusaidia wakati mwingine - mara nyingi haisaidii!
   
Loading...