Tafsiri ya anayesimamia na anayesimamiwa, nani ana mamlaka juu ya mwenzie?

Centrehalf

JF-Expert Member
Jun 9, 2013
509
145
Salaam, naomba kupewa tafsiri halisi ya ibara ya 100 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Katika ibara hiyo kuna kipengele kinachoelezea kazi moja wapo ya bunge ni kushauri na kuisimamia serikali. Ndio maana nimeona niulize kwa wataalam wa sheria kama kazi ya bunge nipamoja na kuisimamia serikali ni kwanini bunge linashikwa na kigugmizi inapofika suala la kuiwajibisha serikali? Je ni kweli bunge haliwezi kuiwajibisha serikali? Au ni gia za spika wa sasa kujaribu kulinda serikali inapo boronga. Naomba tuchangie kitaalam zaidi kuliko kishabiki ili tujifunze.

Nawasilisha.
 
bunge linaweza kuiwajibisha serikali. kama maazimio ya pac yangepita kama yalivyo basi ktk katiba kipengele cha ' kuisimamia serikali' kingekuwa kimezingatiwa lakini bunge lilipokuja na maazimio mapya yalipunguza nguvu yake kutoka 'kuisimamia 'na kwenda "kuishauri" ..Unaweza ukaona sasa kushauri sio kuwajibisha kwasababu ni lugha inampa uhuru anaeshauriwa kwamba azingatie au asizingatie. mim sio mwanasheria ila naona tafsiri na matumiz y maneno hayo mawili yako kama nilivoeleza. wachambuz waje waelezee zaidi
 
wabunge wa chama tawala wakiwa wengi bungeni wanashindwa kuisimamia selikari badala yake wanailinda ili isianguke
 
kiukweli kabisa kwa katiba tuliyonayo, bunge lina mamlaka sio tu ya kuisimamia serikali bali hata ya kuiondoa kabisa serikali. tatizo ni uongozi wa bunge na wingi wa wabunge kutoka kwenye chama kilicho madarakani.
na cha mwsho naamini kabisa ccm hawatakuwa tayari kum-impeach rais kwa sababu wakifanya hivyo hata wao wanarudi kwenye uchaguzi kitu ambacho wengi wao hawana uhakika kama wananchi watawachagua tena au hta kama watapitishwa na chama chao tena kugombea.
kwa kifupi wametanguliza masilahi ya matumbo yao mbele kuliko ya taifa.
 
Back
Top Bottom