Tafsiri "UPDATE"

Namtih58

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
235
46
lipi sawa "SASISHA" au "SASAISHA"

na pia tafsiri ya "VALIDATE" nimeona kwingi ikitumika "sahihisha" lakini kwa maoni yangu itakuwa "to correct"
 
lipi sawa "SASISHA" au "SASAISHA"

Sasisha
ndio sawa zaidi, ingawa sasaisha pia, kwa mawazo yangu, inaleta mantiki. Source: Open Swahili Localization Project (UDSM)

na pia tafsiri ya "VALIDATE" nimeona kwingi ikitumika "sahihisha" lakini kwa maoni yangu itakuwa "to correct"
Kwa kuwa "valid" ina maana ya "halali" basi "validate" haiwezi kuwa sahihisha, bali "halalisha"
 
Kwa hiyo, tafsiri ya "Validation failed" itakuwa ni vipi?

Uhalalishaji shinde
halalishi imeshindwa
Uhalalishaji, matokeo batili

ama .......
 
Kwa hiyo, tafsiri ya "Validation failed" itakuwa ni vipi?

Uhalalishaji shinde
halalishi imeshindwa
Uhalalishaji, matokeo batili

ama .......

uhalalishaji umeshindikana
a(i)meshindwa kuhalalishwa
 
Back
Top Bottom