Tafsiri kuhusu kauli za serikali kuhusu kushambuliwa Dk. Ulimboka na mambo mbalimbali ya kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafsiri kuhusu kauli za serikali kuhusu kushambuliwa Dk. Ulimboka na mambo mbalimbali ya kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Kijana, Jul 10, 2012.

 1. M

  Mzee Kijana JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 748
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 80
  Ni takribani wiki mbili hadi tatu zimepita toka kiongozi wa chama cha madaktari nchini Dr. Stephen Ulimboka aliposhambuliwa na watu wasiojulikana ambao walimpiga nusura kumuua. Watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii walilaani tukio hilo. Nadharia mbalimbali zilizungumzwa kuhusu tukio hili. Nadharia kubwa iliyotawala fikra za wengi ni kuwa Dr. Ulimboka alihujumiwa na watu wa serikali ili kuzima cheche zake na mgomo wa madaktari. Serikali ilitoa kauli kuwa haihusiki na tukio na hilo. Lakini wadau wengi hawaiamini serikali na bado ile dhana kwamba inahusika ipo kwenye vichwa vya watu. Sasa hebu tujiulize maswali yafuatayo kuhusiana na namna watu walivyoupokea utetezi wa serikali:

  1. Kwanini watu hawaiamini serikali inaposema haikushiriki kumhjumu Dr. Ulimboka?
  2. Kwanini serikali hiyohiyo inapotoa kauli nyingine watu bila kufanya utafiti wanaipokea na kuiamini lkn kauli nyingine wanazipinga? Mfano mzuri ni suala la UAMSHO Zanzibar. Serikali iliposema UAMSHO wamechoma makanisa kila mtu aliamini na wengine bila hata kufanya utafiti.

  Hoja yangu ni kuwa kama tuna mashaka na kauli za serikali basi tushuku kauli zote na tusiwe wanafiki kwamba sasa hivi serikali ikisema hivi tunaamini na wakati mwingine hatuamini. Serikali hiyohiyo hupongezwa na kupigiwa vigelegele ikisema watu fulani wako na hupondwa ikifanya tofauti na wale wanaoipongeza. Tuwe objective mara zote tunapopokea na kutafsiri kauli za serikali. Mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu.
   
Loading...