johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,723
- 141,582
Hali ni tete katika kituo cha kimara kama ilivyoripotiwa na Benjamin Mzinga wa ITV msongamano wa abiria ni mkubwa na watu wanaathirika kwa kuumizana na kukosa hewa.
Source: ITV mubashara!
=====
Katika hali ya kuonekana kuchoshwa na kutosikilizwa kwa malalamiko yao, abiria wanaotumia mradi wa Mabasi ya Mwendokasi waamua kuoandia dirishani
Kwa muda mrefu abiria hao wamekuwa wakilalamikia utaratibu wanaouita mbovu wa watoa huduma hiyo ya usafiri.
Mapema leo kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa madereva wa mabasi hayo wamegoma kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yao
UDART imesema katika hali isiyo ya kawaida madereva wawili wanadaiwa kutoa mabasi ndani ya kituo hicho kwa makusudi na kwenda kuziba milango mikubwa miwili ya kutokea mabasi hayo na hivyo kusababisha mabasi mengine kushindwa kutoka ikizingatiwa ilikuwa ni nyakati za asubuhi ambapo mabasi yote yanapaswa kuanza safari zake. Madereva nao wadai kutolipwa Mshahara kwa Wakati.