Tafiti zinazofanywa na taasisi za kiraia mikoani zinatatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao?

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
Kumekuwa na taasisi nyingi za kiraia zikitaka kufanya utafiti wa mambo mbali mbali kwenye mikoa na halmashauri zake, taasisi nyingi ni zile za wazawa na chache kutoka nje.

Pamoja na taasisi hizo kumekuwepo na rundo la wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wakifanya tafiti kwa ajili ya kutimiza malengo yao ya kielemu na mara nyingi wamekuwa wakisema katika proposal zao kuwa tafiti hizo zitasaidia jamii husika kutatua matatizo yao.

Swali, je tafiti za watafiti zinasaidia jamii husika kutatua matatizo?. Au ndio watu wamejitengenezea njia ya kupiga fedha za wafadhili.

Taja taasisi iliyowahi fanya utafiti katika kata/kijiji chako na hadi leo haijawahi leta matokeo ya utafi huo, na ungependa uishauri nini Serikali juu ya taasisi na wanafunzi wasioleta mrejesho wa matokeo ya tafiti kwenye sehemu zilizofanyiwa tafiti?.
 
Back
Top Bottom