Tafiti: Wagonjwa wa moyo nchini waongezeka kutoka 60 hadi 500 kwa siku

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
1,384
3,406
Wataalam wa moyo wamesema magonjwa ya moyo yanazidi kuongezeka Nchini huku imani potofu zikiendelea kusambaa kuhusu tiba ya magonjwa hayo.

Mkurugenzi wa Tiba katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Tatizo Waane amesema awali walikuwa wakipokea wagonjwa 50 hadi 60, lakini hivi karibuni wagonjwa wamefikia 300 hadi 500 kwa siku huku Watoto wakiwa 30 hadi 40.

Amesema: “Takwimu zinaonesha karibu asilimia 30 ya vifo Duniani vinasababishwa na magonjwa ya moyo.

“Takwimu za hapa Nchini zinaonesha takribani asilimia 30 ya Watanzania wana shinikizo la juu la Damu, asilimi 30 wana tatizo la ongezeko la lehemu kwenye damu na asilimia 33 hadi 35 wana uzito uliokithiri na hivyo wako katka hatari ya kupata magonjwa ya moyo.”

Ameongeza kuwa mtindo mbaya wa maisha ukiwemo ulaji mbaya, unjwaji pombe, matumizi ya tumbaku na kutofanya mazoezi vinachania magonjwa ya moyo kwa kiasi fulani.”

Chanzo: Swahili Times
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom