Tetesi: Tafakuri

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
Kama kweli watanzania wanaumia na wizi huu wa mali za umma tuanze shinikizo la haya yafuatayo!.

1.Tuilazimishe serikali itake isitake Rasimu ya Warioba irejeshwe na kupitishwa ili kuondoa kinga kwa maraisi wastaafu na wafike mbele ya vyombo vya sheria na wawaambie watanzania kwa nini haya yalifanyika chini yao na sheria ichukue mkondo wake!.

2.Wale wote waliohusika kuichakachua Rasimu Warioba waombe radhi na wachukuliwe hatua za kinidhamu!.

3.Waliokuwemo kwenye "cabinet"kuanzia cabinet(baraza la mawaziri) la 1990-1995,ambapo walipitisha mkataba mmoja.1995-2005,waliopitisha mikataba ya hovyo mitano na hawa wa 2005-2015,waliopotisha mkataba mmoja wote washtakiwe kwa kuiingizia nchi hasara,masuala ya nchi hufanyika kwa uwajibikaji wa pamoja(collective responsibility)na siyo individual responsibility!.

4.Wabunge wote waliopiga kura ya ndiyo kupitisha sheria ya kodi na ile ya uwekezaji ya mwaka 1997,pamoja na sheria ya madini ya mwaka 2010,wafikishwe mahakamani kwa kuliingizia taifa hasara!.

5.Wabunge wote waliopitisha hoja ya kumfukuza Zitto Kabwe bungeni mwaka 2007 baada ya kumtuhumu waziri Karamagi kuwa alikula rushwa kwenye mkataba kati ya serikali na Barrick Gold wote wafikishwe mahakamani kwa kutetea mkataba wa hovyo na kuipa ruhusa kampuni ambayo haijasajiriwa nchini kuchimba madini na hivyo kulisababishia taifa hasara!.

6.Wale wote waliounda timu ya wataalam wa kulishauri baraza la mawaziri kuhusu mikataba ya madini kuanzia mwaka 1995 mpaka sasa,wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria ili wajibu kama huu ndiyo ulikuwa ushauri wao!.

7.Wale wote waliokuwa wanaopinga sheria hizi na mikataba kuwekwa wazi,watajwe hadharani na kuwaomba radhi watanzania!.

8.Maspika wote walioongoza utungwaji wa sheria hizi nao wafikishwe mbele ya vyombo ya sheria kwa tuhuma za kuhujumu uchumi!.

9.Waandishi wote waliokuwa wanaandika habari ama kutengeneza vipindi vya kutetea wawekezaji nao waombe radhi kwa kutetea wizi huu!.

10.Yote katika yote kama watanzania hatutaanzisha vuguvugu la kuitaka Rasimu ya Warioba tutakuwa hatuvitendei haki vizazi vijavyo na tutakuwa tunapoteza muda!.

11.Usalama wa taifa watuambie je walikuwa wanatoa taarifa kwenye mamlaka juu ya wizi huu?kama hapana nao washughulikiwe!.

11.CCM ya Mkapa na Kikwete iseme wazi kwa nini iliacha kuisimamia serikali na kuacha wizi huu uliolipotezea taifa Trilioni karibu 180?kwa ni waliacha kuisimamia serikali kama alivyowahi himiza Katibu mkuu Kinana?.
 
uchochezi usio vimilika !! NAKUOMBA CENTRAL KESHO... OVER !!!

CCM ni ile ile hakuna wa kumkosoa mwingine!!

#UTANI_TU_SIPO_SILIAZI
 
Natamani hao ulio wataja japo wajibu tu kwa hoja kwanini hayo uliyopendekeza yasifanyiwe kazi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom