Tafakuri Yangu Ya Leo; Nani Kasema Sumu Ya Nyoka Ipo Kwenye Gamba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri Yangu Ya Leo; Nani Kasema Sumu Ya Nyoka Ipo Kwenye Gamba?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KAMBOTA, Apr 21, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  ………….CCM imejivua gamba…………
  Hii ndio kauli inayoendelea kutikisa vichwa vya habari nchini Tanzania kwa sasa kufuatia kikao cha Dodoma kilichokuja na safu mpya ya uongozi ndani ya CCM, ajabu ni kuwa wanahabari wengi wamekumbwa na kamsemo haka pasipo kufikiri mara mbilimbili nini maana sahihi ya msemo huu halikadhalika uhalisia wake upo wapi?
  Naomba niweke wazi kuwa kutokana na CCM kufinywangwa ndani ya kashfa za ufisadi hasa kwa baadhi ya vigogo wake hakuna ubishi kuwa damu ya CCM ilichafuka na gamba lake likazeeka lakini kwa watanzania wengi hata CCM yenyewe imekuwa gamba sasa kutokana na maisha magumu kwa wananchi CCM ndiyo gamba sasa watu wanashangaa
  CCM imejivua nini? Wao CCM watulie waone watanzania watakavyojivua gamba mwaka 2015.
  Hata kama imejivua gamba wenye busara wanauliza kwani gamba la nyoka lina athari gani kwa binadamu? Badala yake ni kuwa nyoka akijivua gamba ndio anakuwa na kasi zaidi ya kutembea hivyo ndio anakuwa hatari zaidi kwa binadamu kwani anaweza kung’ata bila shida, sasa CCM kujivua gamba ina tafsiri gani kwa walalahoi?
  Ipo wazi kuwa licha ya CCM kujivua gamba tena kwa kujilazimisha hakuna hoja ya msingi kwani sumu ya nyoka ipo kwenye damu sio gamba hivyo damu ya CCM ina sumu haifai na hili hata Kikwete analifahamu na anafahamu naposema damu ya CCM na maana gani? Hivyo hii ya CCM kujivua gamba ni bora mjadala ukafungwa rasmi kwani hauna maana kwa maana nani kasema sumu ya nyoka ipo kwenye gamba?..Tafakari!

  Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
  Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai.
   
 2. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe ni mwendawazimu kama si mwendawazimu basi utakua mkaskazini CHADEMA MPAKA KIINGIE MADARAKANI KINATAKIWA KISUBIRI MUDA MREFU KAMA CUF ZANZIBAR ILA CHADEMA WATANGOJA KWELI KWELI KUTOKANA NA UKUKUBWA WA ENEO LA TANGANYIKA LILIVYOKUA KUBWA.WHAT I SEE NCCR ITAKIFUNIKA CHADEMA MUDA SI MREFU,WAIT AND SEE
   
 3. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  naona mzee unakunywa chang'aa!!!

  bado una hangover wewe!!!

  nyie ndio mnaovalishwa matisheti mnachekelea!! na wake zenu kupewa kanga mkaona mmewini!!
   
 4. K

  KAMBOTA Senior Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wanashindwa kujadili hoja wanarukaruka kwa hasira za mkizi bila kujua wanamfurahisha mvuvi, NCCR naqcho chama au just ka NGO? wana nini?
   
Loading...