Tafakuri yangu kwenye masuala nyeti ya Kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri yangu kwenye masuala nyeti ya Kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MushyNoel, Jan 28, 2011.

 1. M

  MushyNoel Senior Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwamba tupo katikati ya matatizo makubwa ya kitaifa sio swali la kujiuliza kwa sasa.Miaka yote 50 ya uhuru bado hatujaweza kuacha kufikiria vyanzo endelevu vya nishati.Badala yake watu wametumia matatizo yeliyopo kuleta mikataba ya kinyonyaji ili tu wajinufaishe kibinafsi.Mwananchi masikini bado na hata hategemei kupata ahueni.Sasa ile kusema kwamba kuna maisha bora kwa kila mtanzania kwangu hiyo ni siasa tupu.Ipo wapi mipango ya muda mrefu na mfupi kumkomboa mwananchi wa kawaida.Nchi yetu yetu inajeuka kuwa shamba la bibi- kwamba unaingia na kuchuma matunda ya bibi utakavyo.Wale walioko kwenye ofisi kubwa wala hawana muda kuangalia nini kinatokea kwa mwananchi wa kawaida.

  Nimepata uchungu sana kusoma habari moja kutoka geita ambapo bwana Hamis Charles baada ya kuhamishwa kwenye makazi yake ya asili ili kupisha upanuzi wa mradi wa Geita Gold Mines amekuwa kama mkimbizi kwenye nchi yake.Miaka mitatu na nusu sasa anaishi kwenye mahema-mvua na jua vyote vyake.Zile nyumba alizoahidi waziri wa Nishati na Madini Mh Adam Malima kwa zaidi ya mwaka sasa zimebaki kitendawili.Charles kawa kama kichaa kwa sasa.Ndipo tulipofikia watanzania.Wakati mwenye nguvu anapotaka kujijenga kiuchumi mwananchi wa hali ya chini hana chake.Anaishia kutangatanga tu kana kwamba Mungu alimpatia hiyo sehemu yenye madini kwa bahati mbaya.Siasa isipotumika vizuri huenda lengo lake likawa ni kuwanyanganya wananchi mali zao na kuziingiza kwenye mkondo wa kisiasa unaolindwa na silaha kali.Kinachotia kichefuchefu ni kwamba katika unyanyasaji huu sisi weusi wenyewe ndo tunakuwa madalali wa kuuza mali zetu na kukandamiza.Ndio tunaoagiza magari ya maji ya kuwasha kushambulia watu.bado tupo utumwani hasa wa kiakili na kifikra.

  Wakati haya yanatokea ni vizuri tukiendelea kujiuliza maswali ya msingi ambayo majibu yake yataleta hamasa mpya kwa wazawa.

  1) Kwanza watanzania tusisahau kwamba bado hatujamjua mmiliki wa Kagoda na hivyo ni haki yetu kujua na nani alichota hayo mabilioni kutoka kwenye mfuko wetu ambao wewe na mimi wote tunachangia kwa kodi zetu.
  2) Pili ni vizuri tukajiuliza kwamba kweli baada ya yote kusemwa na kamati ya akina mwakyembe bado tuna haja ya kuwalipa Dowans.Kwa nini deni lipunguzwe kutoka Bil 185 hadi bil 94?
  3) Tatu tuende kinyume kabisa na kauli ya Nimrod Mkono kwamba anaweza kusaidia serikali kisheria ili isilipe deni hilo au lipunguzwe.Watanzania tunaamini kampuni zote za Richmond na dada yake Dowans ni za kitapeli.Sasa yeye kutaka deni lipunguzwe ni janja toto ya kutaka kutuamisha kwenye msimamo wetu wa kukataa kulipa hadi kupunguziwa deni.hatutaki deni lipungue zaidi tunachotaka ni kutokulipa.Ndio msimamo wetu daima na milele.
  4) Katiba mpya ndio document ambayo kwa sababu itakuwa ya wananchi..itakayosimamia rasilimali zetu kimadhubuti.Sasa tutapata ushujaa wa kutenda na kujiamini kwani mamlaka waliyonayo walio ofisi kubwa yatapungua.Sasa ni vizuri kupigania kiungo hicho muhimu.Sasa ni vizuri kusema kwamba kama upatikanaji wa katiba mpya utafanyiwa mizengwe basi jitihada nyingine zote za kujikomboa zitakuwa kazi bure.

  Raisi wa marekani Obama wakati anaapishwa alisema kwamba ‘Lazima serikali ifanye mambo yake katika mwanga kwani ni njia pekee ya kuleta maelewano kati ya watawala na watawaliwa’ .Sasa hayo mambo tunayoambiwa ni siri za serikali hayana maslahi yeyote kwetu wananchi.Tanzania ndo nyumba yetu na serikali tumeikodisha tu nyumba hiyo waitunze sasa nashangaa mpangaji anakuwa na nguvu kuliko mmiliki.Hii haijakaa sawa sawa.Tubadilike.
   
Loading...