Tafakuri ya WARUMI; Sherehe ya kuwavisha medani majenerali wa kijeshi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
142,318
2,000
Katika utawala wa kirumi ilikuwa ni kawaida sana kufanya GWARIDE katika mitaa mbalimbali siku ya kuwapa MEDANI MAJENERALI wa KIJESHI wanaokuwa wamefanya mambo MAKUBWA na ya KISHUJAA katika nchi.
.
Baada ya gwaride kuisha, jukumu la kumvisha TAJI (crown) jenerali aliyekuwa anapewa heshima lilikuwa ni la MTUMWA mmoja anayechaguliwa ambaye maarufu alikuwa anaitwa jina la “Auriga”.
.
Kazi kubwa ya “Auriga” haikuwa KUVISHA taji bali haswa MANENO ambayo alitakiwa kuongea anapomvisha taji jenerali wa jeshi. Alitakiwa kusema kwa KUMNONG’ONEZA “Memento Homo’(Kumbuka wewe ni mwanadamu tu)(Remember, you are only a human).
.
Maneno haya ambayo ilikuwa lazima yasemwe yalilenga KUMKUMBUSHA kila jenerali kuwa bila kujali USHINDI aliopata, UWEZO aliouonyesha au SIFA anazomiminiwa,ASIRUHUSU hayo yote yakampa KIBURI na AANZE kujiona AMESHAFIKA.
.
Ni rahisi sana KUJISAHAU na mtu ukajiona HAKUNA kama WEWE, ni rahisi KIBURI kukuvamia kwa sababu ya SIFA zinazomiminwa kwako,ni rahisi sana KUDHARAU wengine kwa sababu ya CHEO au PESA ulizonazo.Usipokuwa makini unaweza kujikuta unajiona kama wewe ni “mungu mtu”.Kumbuka,wewe ni mwanadamu tu.
.
Inawezekana hauna mtu wa kukunong’oneza,hauna AURIGA pembeni yako, amua kujikumbusha mwenyewe hata leo na jiambie- “MEMENTO, HOMO”. Ukimuona rafiki yako,kiongozi wako,msanii au bosi wako anayejisahau kujikumbusha, kama unampenda usisahau kumnong’oneza leo-“MEMENTO, HOMO”. Bila Mungu, Bila Unyenyekevu hakuna anayeweza kufika mbali.
.
See You At The Top
.
@joelnanauka_
.
TIMIZAMALENGOYAKO

Jr
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
12,696
2,000
Kwetu hapa ni tofauti Jr. Kwetu kuna kundi lina hatimiliki ya taifa, hata bila kujali ridhaa ya wananchi (Zanzibar).

Kwetu watatumia vyombo vya dola na vya maamuzi kukudhulumu hata haki kidogo uliyonayo (bara). Wa kwetu ni mamiunguwatu. Wenye kutumika kupitia vyeti vyenye utata, wakati watumishi wakitumbuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
142,318
2,000
At the end... We are all humans!
Kwetu hapa ni tofauti Jr. Kwetu kuna kundi lina hatimiliki ya taifa , hata bila kujali ridhaa ya wananchi (Zanzibar).

Kwetu watatumia vyombo vya dola na vya maamuzi kukudhulumu hata haki kidogo uliyonayo (bara). Wa kwetu ni mamiunguwatu. Wenye kutumika kupitia vyeti vyenye utata, wakati watumishi wakitumbuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jr
 
Mapico

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
242
500
See You At The Top
.
@joelnanauka_

MEMENTO,HOMO”
Mi naweka tag labda watajikumbuka
naanza na hawa Policcm.
Lumumba,
wanajikuta mapilato huku Duniani.
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,414
2,000
Alietoa hilo wazo alikuwa na akili sana, hata hivyo naye memento homo.
 
Kaisari

JF-Expert Member
Nov 13, 2012
3,626
2,000
Katika utawala wa kirumi ilikuwa ni kawaida sana kufanya GWARIDE katika mitaa mbalimbali siku ya kuwapa MEDANI MAJENERALI wa KIJESHI wanaokuwa wamefanya mambo MAKUBWA na ya KISHUJAA katika nchi.
.
Baada ya gwaride kuisha, jukumu la kumvisha TAJI (crown) jenerali aliyekuwa anapewa heshima lilikuwa ni la MTUMWA mmoja anayechaguliwa ambaye maarufu alikuwa anaitwa jina la “Auriga”.
.
Kazi kubwa ya “Auriga” haikuwa KUVISHA taji bali haswa MANENO ambayo alitakiwa kuongea anapomvisha taji jenerali wa jeshi. Alitakiwa kusema kwa KUMNONG’ONEZA “Memento Homo’(Kumbuka wewe ni mwanadamu tu)(Remember, you are only a human).
.
Maneno haya ambayo ilikuwa lazima yasemwe yalilenga KUMKUMBUSHA kila jenerali kuwa bila kujali USHINDI aliopata, UWEZO aliouonyesha au SIFA anazomiminiwa,ASIRUHUSU hayo yote yakampa KIBURI na AANZE kujiona AMESHAFIKA.
.
Ni rahisi sana KUJISAHAU na mtu ukajiona HAKUNA kama WEWE, ni rahisi KIBURI kukuvamia kwa sababu ya SIFA zinazomiminwa kwako,ni rahisi sana KUDHARAU wengine kwa sababu ya CHEO au PESA ulizonazo.Usipokuwa makini unaweza kujikuta unajiona kama wewe ni “mungu mtu”.Kumbuka,wewe ni mwanadamu tu.
.
Inawezekana hauna mtu wa kukunong’oneza,hauna AURIGA pembeni yako, amua kujikumbusha mwenyewe hata leo na jiambie- “MEMENTO, HOMO”. Ukimuona rafiki yako,kiongozi wako,msanii au bosi wako anayejisahau kujikumbusha, kama unampenda usisahau kumnong’oneza leo-“MEMENTO, HOMO”. Bila Mungu, Bila Unyenyekevu hakuna anayeweza kufika mbali.
.
See You At The Top
.
@joelnanauka_
.
TIMIZAMALENGOYAKO

Jr
Cc@........
Aione .............
C/........................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom