Tafakuri ya Uzalendo: Tanzania na Fumbo la "Uzalendo-pofu"

Nietzsche

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
206
391
Nimeisikia kauli hii mara nyingi sana, mara nyingi kiasi kwamba karibu inakuwa ni istiari chakavu: "usiichafue Tanzania unapokuwa nje." Kauli hii inabeba ghiliba na utata; utata uliofichama uvunguni mwa "uzalendo-pofu." Utata uliokusudiwa. Utata huu uko katika kile kinachofichwa na watumiaji wa kauli yenyewe, na katika jinsi kiarifu chake chenye kubeba jina "Tanzania" kinavyotumika nusu-nusu; Tanzania katika muktadha upi? Muktadha wa "nchi" au muktadha wa Serikali? Wanaficha nini? Kwa manufaa ya nani? Maswali ni mengi. Hivyo, leo nimeazimia kuutanzua utata wa kauli hii, kwa kuijadili dhana halisi ya "uzalendo."

Kwamba Mh Tundu Lissu (MP) "aliichafua Tanzania" alipozungumza juu ya yale yanayotokea Tanzania akiwa pale BBC, ni 'kauli tata' isiyoingia akilini mwangu. Kwanza, kuna hoja ya kikanuni inayohitaji kuzingatiwa hapa. Kikanuni, jina "Tanzania" likiwa peke yake, haliwi na maana sawa na jina "Serikali ya Tanzania"; hivi ni vitu viwili tofauti. Tanzania kama nchi ni unganiko la vitu vikuu vitatu: ardhi yake, watu wake, na Serikali yake. Hivyo, Lissu anapoituhumu Serikali kwa ukandamizaji kwa mfano, anakuwa anatuhumu kitu kimoja kati ya hivi – Serikali. Si watu wa Tanzania, na wala si ardhi yao.

Hata hivyo, bado kuna swali muhimu linalohitaji jibu hapa. Je, Lissu "anaichafua serikali" au serikali inajichafua yenyewe? Nauliza hivi kwa sababu, jambo moja liko wazi: kila kitu alichokisema Lissu, kilikuwa kimeshatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kabla Lissu hajazitoa tuhuma zile pale BBC. Benki ya Dunia ilipokuwa na dukuduku kuhusiana na tatizo la wasichana wajawazito kupigwa marufuku kuendelea na masomo, hakuwa Lissu aliyelisababisha hilo; EU ilipomwondoa balozi wake kwa sababu ya hatua ya mkuu wa mkoa dhidi ya mashoga, siyo Lissu aliyechukua hatua hizo dhidi yao; n.k. Hivyo basi, ni nani anayeichafua serikali hapa, Lissu au serikali yenyewe?

Jambo moja lililo muhimu kulielewa ni kwamba, serikali sio "nchi." Serikali huitumikia nchi – serikali ni taasisi inayopewa jukumu la "kuwatumikia" watu. Kama watu hao wana bahati, wanaweza wakaishia kuwa na "mtumishi mzuri" katika serikali yao; kama wana bahati mbaya, wanaweza wakaambulia "mtumishi jeuri", asiyeambilika wala asiyerekebishika! Serikali inaweza ikashikiliwa na magaidi, wakoloni, au wabishi wasiokuwa na ufahamu, wala wasiowasikiliza wale wanaowatumikia; au inaweza ikashikiliwa na watu wema, wenye heshima, maadili na bidii ya kuitumikia nchi. Nchini Tanzania kwa mfano, wakoloni waliishikilia serikali, lakini wakamwita Mwalimu Nyerere "mwasi" (rebel); huko Afrika Kusini, makaburu walikuwa serikalini, lakini walimwita Mandela "gaidi"; na mwanzilishi wa taifa la Marekani, George Washington, aliitwa "mwasi" na serikali ya siku hizo. Dhana ya "serikali" mara nyingi imekuwa ikichukuliwa kama aina fulani ya “ufalme” – huu ni upotofu. Hii si sahihi hata kidogo, hasa katika kizazi hiki na karne hii.

Dhana ya uzalendo pia inaeleweka vibaya, kama dhana ya serikali inavyoeleweka vibaya. Tunapoongelea uzalendo, kuna aina mbili za uzalendo. "Uzalendo halisi" (patriotism) na "uzalendo-pofu" (chauvinism). Nitaanza na dhana ya uzalendo-pofu. Uzalendo-pofu ni aina ya uzalendo uliokithiri, na ni imani katika 'ukuu' na 'utukufu' wa kitaifa, na hata kitabaka. Unaweza pia ukaelezewa kama "imani isiyo na mantiki inayojikita katika 'ukuu' (superiority) na 'utawala' (dominance) wa kikundi cha mtu au watu." Mzalendo-pofu (chauvinist) huwa na hulka ya kuwatetemekea, au kama anavyosema Prof Heywood, "kuwaabudu" na kuwapenda watawala wa nchi kuliko anavyoipenda nchi yake (Heywood, 2015). Aidha, wazalendo-pofu huchukuliwa kama "watu wa pekee" au "wateule" ndani ya jamii husika, ilhali raia wengine wakichukuliwa kama watu "duni" na dhaifu (Heywood, 2015).

Chimbuko la "uzalendo-pofu" ni askari wa Kifaransa Nicolas Chauvin aliyejeruhiwa katika vita vya Napoleon, na kutunukiwa nishani ya "Sabre" na Napoleon mwenyewe. Lakini rekodi yake ya utumishi na mapenzi yake mazito kwa Napoleon, ambavyo vilidumu kwa muda mrefu licha ya gharama yake ya kashfa kutoka kwa Wafaransa wenzie kutokana na ukereketwa wake kwa Napoleon, havikumsaidia chochote zaidi ya kumzidishia dhihaka kutoka kwa wenzie katika kile kipindi cha "Kurejeshwa kwa Ufaransa" (Restoration of France) kilichoanza mwaka 1815 baada ya anguko la Napoleon pale itikadi yake ya "Bonapartism" ilipozidi kuchukiwa. Ukereketwa wa Chauvin wa 'kiupofu-pofu' (blind devotion), na mapenzi yake kwa Napoleon, ndivyo vikawa chimbuko la "uzalendo-pofu." Aina hii ya uzalendo ni hatari, na ndiyo inayotusumbua hata Tanzania. Ndiyo maana nafikiri tunaihitaji sana elimu ya uraia sasa hivi. Mnaotaka kusoma zaidi juu ya hili, tafuteni kitabu kinachoitwa "Global Politics" cha Prof Andrew Heywood.

Aina ya pili ya uzalendo, "uzalendo halisi," huhusisha upendo wa dhati kwa taasisi fulani, kujitambua kama mtu wa taasisi fulani, na hangaiko la pekee (special concern) kwa ajili ya taasisi hiyo. Taasisi hii ni "patria" ya mtu – nchi ya mtu – siyo serikali yake. Horace, mshairi wa Kirumi, aliwahi kuandika "dulce et decorum est pro patria mori" (Horace’s Odes, III.2.13), maneno ambayo kwa tafsiri ya juu-juu yana maana "ni raha sana na inastahiki mtu kufa kwa ajili ya nchi yake." Neno la Kilatini "patria", linalomaanisha nchi ya mababu wa mtu, ni chimbuko la neno la Kifaransa "patrie", linalomaanisha "nchi ya kuzaliwa" – siyo serikali, pia ni chimbuko la neno la Kiingereza "patriot", ambalo kwa Kiswahili linatafsiriwa kama "mzalendo", na ambalo linamaanisha "mtu aipendaye 'nchi' yake" – siyo serikali. Kinyume na upotoshaji unaoendelea sasa hivi, serikali haiimiliki nchi; bali nchi inaiimiliki serikali. Serikali ni chombo kinachoundwa na "wazalendo halisi" wa nchi, kuwatumikia wazalendo.

Kwamba walio wengi kati ya watu wetu mpaka sasa bado hawaielewi dhana hii, hata baada ya miaka 57 ya uhuru, inatokana na mabaki ya ukoloni na dhana za kale za kitemi ambazo zinahitaji kung’olewa.
 
Asante, andiko zuri lenye elimu ya kutosha....

Kwa maoni yangu ni kuwa, wapotoshaji hawa wanaelewa fika kuwa wanapotosha....

Lakini ndiyo hivyo tena, watu wanatumia "ujinga" wa wachache kuendeleza harakati zao za kujinufaisha...

Ukijaribu kutoa elimu kama hii kuleta uamusho kwa wanaodanganywa ili waamuke na kuipambania nchi na hatima yao, utajibiwa kwa risasi....

Tundu Lissu is right. Haichafui nchi, bali anaonesha uchafu unaofanywa na serikali ya sasa chini ya CCM na Rais wao Pombe kuichafua nchi yetu MAMA YA TANZANIA....

Kwa ufupi kabisa, ni kuwa, serikali inajichafua yenyewe, ilishajichafua sana na itaendelea kuichafua na kupitia uchafu wake, inaichafua hadi NCHI YETU....!!

Ni haki kabisa kuisema na kuikosoa serikali hii kwa matendo yake machafu dhidi ya raia wake na dhidi ya nchi yetu...
 
Asante sana Kitaturu. Taratibu tu mwisho wataelewa. Kama alivyosema Tundu Lissu juzi, sisi sote tunao wajibu wa kuipigania Tanzania yetu, kila mtu katika nafasi aliyo nayo. Mimi na wewe leo tumetimiza mchango wetu, japo mdogo, katika jukwaa hili. Hivi, nakushukuru sana mkuu, na Mungu akubariki.
 
Wow! Hii ni elimu ni kali. Jamani kuna watu wana akili. Sidhani kama kuna upinzani katika haya uliyoandika! Ndiyo maana huwaoni kina Pascal Mayala hapa. Hizi ni hoja nzito mno kuhusiana na uzalendo.
 
Mkuu Nietzsche Andiko makini na lenye madini. Nimesoma hili andiko ili ku intergrate na lile ulilochambua hotuba ya Tundu Lisu Maryland. Nimekuelewa vizuri sana. Am appriciate.
 
Ahsante ndugu kwa andiko murua, watu wanaenda kwa mkumbo tu uzalendo wa sasa nchini definition imebadilika. Nakumbuka kuna mbunge USA mwenye asili ya Somalia alisema patriotism is not an allegiance to the president.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu Nietzsche Andiko makini na lenye madini. Nimesoma hili andiko ili ku intergrate na lile ulilochambua hotuba ya Tundu Lisu Maryland. Nimekuelewa vizuri sana. Am appriciate.

Nami niwashukuru sana wakuu emalau na 2013 kwa kuchukua muda wenu out of schedule kutoa maoni yenu adhimu. Nasikitika kusema kuwa, japokuwa nina mengi ya kusema kuhusu nchi yetu, mimi huwa siandiki sana humu kwa sababu ya kukosa muda. Na ukiona nimeandika kitu humu, basi ujue hicho kitu kimenikereketa kweli. Na hili ni moja ya mambo ambayo yamekuwa yakinikera kwa muda mrefu.

Kwa muda sasa, watu wetu wameburuzwa sana kwa kutumia hii 'loophole' ya hiki kitu kinachoitwa "uzalendo." For what? It's not right. Tanzania mambo mengi tunaumia kwa kukosa awareness, uelewa wa mambo, na nidhamu kwenye principles na kwenye vitu vinavyohitaji adherence to principles.

Nidhamu yetu tuliyofundishwa toka utotoni ni "nidhamu ya uwoga" ambayo ni self-defeating and that's why we never question things. We refrain from questioning anything and we never take constructive criticisms well. We are conditioned to "blind submission," and that's not good at all.

Hakuna kitu muhimu kama kujitambua; kuzitambua haki zako (rights) kama raia wa nchi na kama binadamu, na kuutambua wajibu wako (duty) kama raia wa nchi na kama binadamu. Kujitambua humweka mtu huru, na kuchochea fikra na afya ya fikra za mwenye kujitambua.
 
Nimeisikia kauli hii mara nyingi sana, mara nyingi kiasi kwamba karibu inakuwa ni istiari chakavu: "usiichafue Tanzania unapokuwa nje." Kauli hii inabeba ghiliba na utata; utata uliofichama uvunguni mwa "uzalendo-pofu." Utata uliokusudiwa. Utata huu uko katika kile kinachofichwa na watumiaji wa kauli yenyewe, na katika jinsi kiarifu chake chenye kubeba jina "Tanzania" kinavyotumika nusu-nusu; Tanzania katika muktadha upi? Muktadha wa "nchi" au muktadha wa Serikali? Wanaficha nini? Kwa manufaa ya nani? Maswali ni mengi. Hivyo, leo nimeazimia kuutanzua utata wa kauli hii, kwa kuijadili dhana halisi ya "uzalendo."

Kwamba Mh Tundu Lissu (MP) "aliichafua Tanzania" alipozungumza juu ya yale yanayotokea Tanzania akiwa pale BBC, ni 'kauli tata' isiyoingia akilini mwangu. Kwanza, kuna hoja ya kikanuni inayohitaji kuzingatiwa hapa. Kikanuni, jina "Tanzania" likiwa peke yake, haliwi na maana sawa na jina "Serikali ya Tanzania"; hivi ni vitu viwili tofauti. Tanzania kama nchi ni unganiko la vitu vikuu vitatu: ardhi yake, watu wake, na Serikali yake. Hivyo, Lissu anapoituhumu Serikali kwa ukandamizaji kwa mfano, anakuwa anatuhumu kitu kimoja kati ya hivi – Serikali. Si watu wa Tanzania, na wala si ardhi yao.

Hata hivyo, bado kuna swali muhimu linalohitaji jibu hapa. Je, Lissu "anaichafua serikali" au serikali inajichafua yenyewe? Nauliza hivi kwa sababu, jambo moja liko wazi: kila kitu alichokisema Lissu, kilikuwa kimeshatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kabla Lissu hajazitoa tuhuma zile pale BBC. Benki ya Dunia ilipokuwa na dukuduku kuhusiana na tatizo la wasichana wajawazito kupigwa marufuku kuendelea na masomo, hakuwa Lissu aliyelisababisha hilo; EU ilipomwondoa balozi wake kwa sababu ya hatua ya mkuu wa mkoa dhidi ya mashoga, siyo Lissu aliyechukua hatua hizo dhidi yao; n.k. Hivyo basi, ni nani anayeichafua serikali hapa, Lissu au serikali yenyewe?

Jambo moja lililo muhimu kulielewa ni kwamba, serikali sio "nchi." Serikali huitumikia nchi – serikali ni taasisi inayopewa jukumu la "kuwatumikia" watu. Kama watu hao wana bahati, wanaweza wakaishia kuwa na "mtumishi mzuri" katika serikali yao; kama wana bahati mbaya, wanaweza wakaambulia "mtumishi jeuri", asiyeambilika wala asiyerekebishika! Serikali inaweza ikashikiliwa na magaidi, wakoloni, au wabishi wasiokuwa na ufahamu, wala wasiowasikiliza wale wanaowatumikia; au inaweza ikashikiliwa na watu wema, wenye heshima, maadili na bidii ya kuitumikia nchi. Nchini Tanzania kwa mfano, wakoloni waliishikilia serikali, lakini wakamwita Mwalimu Nyerere "mwasi" (rebel); huko Afrika Kusini, makaburu walikuwa serikalini, lakini walimwita Mandela "gaidi"; na mwanzilishi wa taifa la Marekani, George Washington, aliitwa "mwasi" na serikali ya siku hizo. Dhana ya "serikali" mara nyingi imekuwa ikichukuliwa kama aina fulani ya “ufalme” – huu ni upotofu. Hii si sahihi hata kidogo, hasa katika kizazi hiki na karne hii.

Dhana ya uzalendo pia inaeleweka vibaya, kama dhana ya serikali inavyoeleweka vibaya. Tunapoongelea uzalendo, kuna aina mbili za uzalendo. "Uzalendo halisi" (patriotism) na "uzalendo-pofu" (chauvinism). Nitaanza na dhana ya uzalendo-pofu. Uzalendo-pofu ni aina ya uzalendo uliokithiri, na ni imani katika 'ukuu' na 'utukufu' wa kitaifa, na hata kitabaka. Unaweza pia ukaelezewa kama "imani isiyo na mantiki inayojikita katika 'ukuu' (superiority) na 'utawala' (dominance) wa kikundi cha mtu au watu." Mzalendo-pofu (chauvinist) huwa na hulka ya kuwatetemekea, au kama anavyosema Prof Heywood, "kuwaabudu" na kuwapenda watawala wa nchi kuliko anavyoipenda nchi yake (Heywood, 2015). Aidha, wazalendo-pofu huchukuliwa kama "watu wa pekee" au "wateule" ndani ya jamii husika, ilhali raia wengine wakichukuliwa kama watu "duni" na dhaifu (Heywood, 2015).

Chimbuko la "uzalendo-pofu" ni askari wa Kifaransa Nicolas Chauvin aliyejeruhiwa katika vita vya Napoleon, na kutunukiwa nishani ya "Sabre" na Napoleon mwenyewe. Lakini rekodi yake ya utumishi na mapenzi yake mazito kwa Napoleon, ambavyo vilidumu kwa muda mrefu licha ya gharama yake ya kashfa kutoka kwa Wafaransa wenzie kutokana na ukereketwa wake kwa Napoleon, havikumsaidia chochote zaidi ya kumzidishia dhihaka kutoka kwa wenzie katika kile kipindi cha "Kurejeshwa kwa Ufaransa" (Restoration of France) kilichoanza mwaka 1815 baada ya anguko la Napoleon pale itikadi yake ya "Bonapartism" ilipozidi kuchukiwa. Ukereketwa wa Chauvin wa 'kiupofu-pofu' (blind devotion), na mapenzi yake kwa Napoleon, ndivyo vikawa chimbuko la "uzalendo-pofu." Aina hii ya uzalendo ni hatari, na ndiyo inayotusumbua hata Tanzania. Ndiyo maana nafikiri tunaihitaji sana elimu ya uraia sasa hivi. Mnaotaka kusoma zaidi juu ya hili, tafuteni kitabu kinachoitwa "Global Politics" cha Prof Andrew Heywood.

Aina ya pili ya uzalendo, "uzalendo halisi," huhusisha upendo wa dhati kwa taasisi fulani, kujitambua kama mtu wa taasisi fulani, na hangaiko la pekee (special concern) kwa ajili ya taasisi hiyo. Taasisi hii ni "patria" ya mtu – nchi ya mtu – siyo serikali yake. Horace, mshairi wa Kirumi, aliwahi kuandika "dulce et decorum est pro patria mori" (Horace’s Odes, III.2.13), maneno ambayo kwa tafsiri ya juu-juu yana maana "ni raha sana na inastahiki mtu kufa kwa ajili ya nchi yake." Neno la Kilatini "patria", linalomaanisha nchi ya mababu wa mtu, ni chimbuko la neno la Kifaransa "patrie", linalomaanisha "nchi ya kuzaliwa" – siyo serikali, pia ni chimbuko la neno la Kiingereza "patriot", ambalo kwa Kiswahili linatafsiriwa kama "mzalendo", na ambalo linamaanisha "mtu aipendaye 'nchi' yake" – siyo serikali. Kinyume na upotoshaji unaoendelea sasa hivi, serikali haiimiliki nchi; bali nchi inaiimiliki serikali. Serikali ni chombo kinachoundwa na "wazalendo halisi" wa nchi, kuwatumikia wazalendo.

Kwamba walio wengi kati ya watu wetu mpaka sasa bado hawaielewi dhana hii, hata baada ya miaka 57 ya uhuru, inatokana na mabaki ya ukoloni na dhana za kale za kitemi ambazo zinahitaji kung’olewa.

Jamani kumbe Tanzania tuna vichwa vimetulia tu. Hili andiko ni kiboko! Halafu mbona maada kama hizi wale wachambuzi nguli kina Paschal Mayala na wengine huwa hawagusi? Kaka Paskali, njoo huku unaitwaa :)
 
Hili bandiko nimelikubali. Mkuu mleta hoja heshima yako kuu sana mkuu. Maada za watu vichwa kama nyinyi watu wanaojifaraguaga na uchambuzi wao uchwara, hasa wale wana Lumumba, hawazigusi. Wanaziogopa kama ukoma!! :D:)
 
Anayehubili uzalendo anatakiwa uonekane kuanzia kwake mwenyewe.Mwalimu Nyerere alikuwa mujamaa lakini ulikuwa ukimutazama unaona ujamaa unamufanana kwa maneno na kwa vitendo.
umenena poa... Magufuli hafanani hatakidago (anatuzuga) kwa kunywa Madafu mbele ya camera huku wapambe wakimwita Rais wa Wanyonge.. Sifa uchwara kabisa... Eti Rais wa Wanyonge huku akitupiga kweli kweli kama 1.5 til.. au 2.4 til.. Ametupiga kweli kweli kwenye chaguzi za hovyo hovyo namengine mengi tu kama uwanja wa chato na... na... na... na anafikili anatuzuga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom