Da vincci
Member
- Aug 9, 2009
- 61
- 9
[h=6]Salaam wanabodi,
Kama inavyofahamika kwa wengi kiini cha filamu bora siku zote huanza na muswada bora wa filamu ambao ni zao la hadithi iliyotimilika katika nyanja zote za fasihi.Siku zote nimekua nikiamini muswada wa filamu ni kama ramani au mchoro wa nyumba na mchoraji wa ramani ya nyumba ni kama mwandishi wa filamu! Wote hawa hufikirisha akili zao na kuwasilisha mawazo yao katika Makaratasi,lakini mara nyingi watu hawa hukosa ama taaluma ya kutosha au uwezo wa kutosha kuweza kuyatoa mawazo yao kutoka kwenye makaratasi na kuyaweka katika hali ya uhalisia zaidi (jengo/filamu) ambayo uma au hadhira huvutiwa nayo na kunufaishwa kwa namna moja au nyingine.Ikitokea mchoraji wa ramani ya jengo (architect) akawa na taaluma ya uhandisi (engineering) kimaadili ya taaluma ni ruksa akaendelea na ujenzi vivyo hivyo basi ikatokea mwandishi wa muswada wa filamu akawa na taaluma ya uongozaji wa filamu ni ruksa pia akaendelea na mchakato huo wa utayarishaji wa filamu husika.Lakini ijulikane wazi ya kuwa kila kazi ina miiko yake na walioleta mgawanyiko wa kazi hawakua majuha.
Ndugu zangu leo hii ukimuacha mwandishi wa muswada wa filamu akawa muongozaji hata kama ana taaluma zote mbili kuna hatari kubwa ya kuzuia wigo wa ubunifu ambao ungeweza kuongezwa kwa kuwagawanyia majukumu watu hawa. Mfano huu unakwenda sambamba na maamuzi ya kumuacha mchora ramani ya jengo akawa mhandisi! Kwa mantiki hii katu hautotegemea kupata jipya habadani.
Wandugu,kukosekana huku kwa 'a clear demarcation line of responsibilities' (mstari angavu wa mpishano au mpaka wa majukumu) baina ya pande hizi mbili ambazo kimsingi ndio mihimili ya tasnia nzima ya filamu umepelekea kuwa na zao la 'bora filamu' nyingi zisizo na mguso kwa jamii.
Wengi watakuja na kueleza matatizo mengine lakini mgogoro mkuu utabaki huku chini! Tukitibu huku kwenye shina huko juu itatuwia rahisi,lakini tukiendelea kushupalia huko juu wakati huku chini kumetushinda hatutafanikiwa kamwe!
Watu wanalalamikia maswala ya location (muktadha),casting (ushiriki) n.k vyote hivi ni rahisi ukavirekebisha endapo utakua na msingi mzuri wa waandishi na waongozaji kama mhimili mkuu wa tasnia nzima ya filamu.
Nimekua nikisema mara nyingi ya kwamba uandishi mzuri wa filamu huanza na kipaji kikifuatiwa na mafunzo lakini uongozaji wa filamu huitaji mafunzo ya kitaalamu zaidi kabla ya kipaji binafsi.
Wandugu,ningependa kuwaasa wadau wa tasnia hii kutosingizia mitaji midogo ya kufadhili utayarishaji wa filamu kama chanzo cha kujipachika vyeo siyo tu wasivyoviweza bali wasivyostahili kwa minajili ya uzao wa kazi za mikono na fikra zao (tumeziona)!
Wandugu,wenzetu wa magharibi wana taasisi na wakala za uwezeshaji fedha wa filamu (film financing agencies and institutions), mwandishi unapeleka muswada wa filamu ,afisa mikopo na baraza lake wanaupitia na kama una tija mnaingia mkataba wa kufadhili filamu kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa hatua ya usambazaji.
Lakini haya yote hayatawezekana endapo hakutakua na miswada bora ya filamu yenye uwezo wa kumvutia mwekezaji kama hii tuliyokua nayo sasa.
Wandugu uwezo tunao na nafasi husika tunazo mfano Tanzania Investment Bank,benki za kibiashara kama NBC, CRDB ,NMB, donors (wahisani) n.k.Nina uhakika kama tutakua na mipango sahihi na ushawishi wa kutosha tutaweza kuyakabili makundi tajwa hapo juu na kuweza kufinance filamu zetu kuelekea kwenye ubora tunaouona kwa wenzetu na kuuota huku tukitamani ungekua wa kwetu.
Tumechoka kuwa na filamu za bajeti ndogo zisizozidi milioni kumi huku tukitegemea kazi zenye viwango bora. Nawaomba Wadau wenye njia mbadala na mitizamo jengefu na watujuze tukajuzike ili tupate kujua tunatokaje hapa na kuendelea mbele kwani tulipotoka twapajua.
Natumai wachangiaji watatoa maoni huru kulingana na utashi na weledi wao na siyo mapenzi binafsi wala kuegemea mrengo fulani.
Ahsanteni na poleni kwa kusoma waraka huu na majukumu mengine yanayowakabili.
Nawasilisha.[/h]