Tafakuri ya Faizafoxy 5: Mtego wa panya, Rushwa, Ufisadi, Siasa, Uchumi, vimenasa vyote?

Dada FaizaFoxy kuhusu kuendeleza reli ya mjerumani ama ya mchina hapo ukubali umekengeuka. Hivi sasa nchi nyingi zinajenga reli za kisasa. Serikali ya UK inatayarisha mpango wabjujenga reli mpya iitwayi HS2 kutoka Dar(London( mpaka Mwanza(Manchester) kwa kuanzia itafika Dodoma(Leeds). China nao wanazo mpya. Kuna ubaya gani kubotesha miundombinu kwa kuweka usafiri wa haraka. Kama unadhani SGR itaharibu biashara za malori je huoni unajichanganya pia kwa kupendekeza uboreshaji wa TAZARA na reli ya kati? Kwani hizo reli mbili hazitaharibu biashara za malori? Halafu nilitegemea usafiri wa haraka na uhakika ungechangia biadhara za wakazi wa hayo maeneo.

Ni mtazamo wangu tu.

Nadhani umeelewa nilichokiandika lakini hujaielewa nadharia.

Tunafanya nini wakati huu reli inapoendelea kujengwa kunusuru hiyo mitaji ya wengi wataoathirika?

Nadhani umeshaona yanayotokea Kenya? Kama hujaona hebu rejea ku google maandamano ya wakazi wa Mombasa na malalamiko ya uchumi wao kukwama kabisa kipindi hiki.

Pia sifahamu kama unaelewa kuwa mitaji mingi mikubwa ya usafirishaji imeshaanza kuhamishiwa nje ya Tanzania?

Hilo kwa wenye mitaji mikubwa ni rahisi kuanza kuhamisha mitaji na kuipeleka kwengine, vipi kwa wenye mitaji midogo? Ambao ndiyo wengi zaidi? Na vipi kwa waajiriwa wasoweza kuhama Tanzania mitaji inapohamishiwa kwengine?

Inabidi tuumize vichwa japo kidogo kuanza kupeana ushauri wa nini ya kutarajia.
 
Ubongo wa mleta mada unamshawishi kwamba ,Tanzania isipojenga viwanda ,kununua ndege, kujenga SGR , kuwa na bwawa kubwa la kufua umeme, hapo sasa Tanzania itapata maendeleo kwa kasi sana..
Usisahau umeme wa gas ulipigiwa singeli na Prof Muongo baada ya kudaka samaki kwenye dema au baada ya kutuingiza Mkenge haijulikani kama yupo au tiari yupo kwa malaika! Kwa vyovyote Ana kula kuku kwa mrija baada ya kutuingiza mkenge!
 
Kwetu Mkuranga, kuna mitego ya panya maarufu sana. Hutengenezwa kama dema la samaki na wengine hadi leo hii huiita "dema la panya". Mitego hii ni mizuri sana lakini kila kizuri huwa na changamoto zake. Mtego huo ukitegwa hunasa panya na vinginevyo.

Tanzania kabla ya hapo, Tanganyika, tunajitawala wenyewe kwa miaka 58 sasa, toka tulipokabidhiwa nchi, sifahamu na Umoja wa Mataifa au Uingereza.

Huwa najiuliza, kwanini miaka 58 bado tunategemea hata bajeti yetu kujalizwa na nchi za nje?

Uhuru tunaojivunia ulikuwa ni
"dema la panya?

Tanzania tuna reli ya Mjerumani na tuna reli ya Mchina na sasa tunaongeza reli ya tatu, ya Mturuki. Swali, tumeshindwa nini kuziendeleza reli za Mjerumani na Mchina hadi tuanze alifu kwa kijiti na reli ya Mturuki? Jee, siyo dema hili?

Reli mpya siyo dema litakalo unasa na uchumi wetu?

Vipi? Najaribu kufikiria magari mangapi makubwa ya mizigo yatakosa kazi kwa kuundwa reli hii, najaribu kufikiria vituo vingapi vya haya magari makubwa ya mizigo vitakosa biashara kuanzia Dar hadi mpakani? Maelfu (kama si malaki) ya Watanzania watakosa ajira za moja kwa moja (direct employment) na wangapi watakosa ajira na vipato vya "indirect"? Siyo dema hili?

Ndege:
Tunafanya la maana sana kuwa na ndege zetu wenyewe lakini nalo siyo dema? Maana ni muda mchache toka tuanzishe tena kuwa na ndege zetu wenyewe, kwa muda huu mchache
tumeshashuhudia ndege hizo watu wakianza ubadhirifu hata kwenye kuzichora nembo tu! Pia tumeshuhudia zikishikwa sasa mara ya tatu na watu wenye madai yao. Siyo dema hili?

Viwanda.
Nachelea kuuliza ya viwanda kwani nafahamu mfumo wetu wa sasa wa kuwekeza kwenye viwanda ni tofauti na ule tulioshindwa kabisa kuuendesha, wa awamu ya kwanza. Ule ulikuwa mfumo wa mali za umma, sasa tunawataka wawekezaji wawekeze kwenye viwanda. Hiyo ndiyo tofauti.

Lakini jee, likija suala la kukorofishana na wawekezaji hivi viwanda havitajosa vipuli na baadhi ya mahitaji ya nje ya kuviendesha? Siyo dema hili?

Nachelea zaidi kuongelea umeme wetu mpya kwa kuyatafakari hayo hayo ya kuwa labda tunaingizwa kwenye dema huku tunajiona mahodari?

Vipi? Tunasoma kuwa dunia ya leo inajikita katika teknolojia ya kuufanya umeme uwe (localized) kwa kuanza kubuni na kuijaribu teknolojia ya kuendesha umeme wa nyumba kwa nyumba, jumba kwa jumba, kiwanda kwa kiwanda badala ya kuwa na umeme wa kizamani wa kufuliwa sehemu moja (kama tufanyavyo) na kutawanywa. Siyo dema hili?

Tafakuri yangu inanipelekea kuona kuwa siasa, uchumi, rushwa na ufisadi vyote vinaweza kutumiwa na wasuka dema kutunasa tuliokuwemo na tusiokuwemo.

Cha kufanya? Tujadili.

"Damned if you do, damned if you don't".
Woote mantanange kazi kupiga makofi tu
 
Dema?ndugu faiza foxy!Mi nadhani DEMA kubwa ni huyo asieshaurika ambae chama chenu kilimpitisha!huyo ndo mwanzo wa utungu!!!2020 msituangushe Litoeni Dema mje mtu mbadala angalau mwenye masikio na nasaba za kitanzania!!!sidhani kama huyu ni wetu!angekuwa wetu angeshaurika!!!!
Na nani wa kabla yake ambae alilikwepa dema?

Fikiri kwa mapana zaidi na usijikite kwenye "personalities".

Nimeandika kuwa ni miaka 58 sasa bado tu tegemezi hata wa bajeti yetu, wakati tukiona nchi zingine zilizokuwa masikini kuliko sisi zikijikwamua kwa kipindi kama hicho au kichache kuliko hicho. Mfano Malaysia, Singapore na hata Dubai.

Ni dema tunalitengeneza wenyewe kisha linatunasa au dema limetengenezwa kiustadi na tunashindwa kuliepuka?
 
Asante kwa kunielewa kwahio tufike mahali tuache kuonyesheana vidole, tufike mahali tuongozwe na katiba, kanuni na sheria za nchi tukiamini kuwa Mpinzani sio mhaini na kwamba CCM si Mungu......wote tuna mapungufu yetu na sote tuna ubora wetu.

Kwa mfano, bungeni mnaweza kupitisha muswada wa kijinga kabisa ili tu kuwakomoa akina fulani, bungeni mpinzani anaweza kutoa hoja nzuri kabia lakini kwakua imetolewa na mpinzani itaonekana si lolote si chochote, tukumbuke mwisho wa siku woet tunabaki kuwa Watanzania.
Hilo nalo neno.

Kuna watu hawapendi fulani akosolewe hata kama kafanya kosa.

Bado tuna tatizo la "critical thinking". Mawazo yetu tunayakita kwenye kusifia si kwenye kutafuta ufumbuzi.

Ufumbuzi hupatikana kwenye kukubaliana kuto kukubaliana. Ikiwa hatutakuwa na uwezo wa kukubaliana kutokubaliana basi maendeleo ya kweli yatachelewa sana.

Binafsi siamini kama yote ya CCM ni sahihi na pia mpaka leo hii siamini vyama vya upinzani ni vya kweli (genuine).

Binafsi naamini wana siasa wetu wote, iwe CCM au kwengine, siasa ndiyo kazi yao ya kuwapatia mahitaji yao ya kimaisha ya kila siku.

Matokeo yake ni kuwa raia tunajazwa ujinga wa kuwa tegemezi kwa wana siasa. Hata mkate wetu wa kila siku watuamulie wao tutaupata vipi. Ni hatari sana.
 
FaizaFoxy yawezekana watanganyika bado kujitambua kama taifa huru.
Labda tukipunguza wizi wa mali za umma,na kuwapata watawala wanaowajibika kwa wananchi wao.Tukiheshimiana na kusaidiana bila kubaguana tutapasua.
 
Hilo la magari ya mizigo kilio cha taiga wengine washaanza kuhamishia biashara nchi za jirani watakaopoteza ajira ni nduguzetu
Hiyo SGR itakuwa inashusha mizigo kwenye kila godown la Mfanyabiashara aliyepakia mzigo? Biashara ya malori haiwezi kufa. Ni ku add value tu..big companies za transportation ziweke warehouses and marshalling yards kwenye stations za SGR. Then watabeba mizigo from yards/warehouses hadi kwa Mtu wa mwisho.
 
Katika Mara chache ninazokubaliana nawe hii ni moja wapo, na inaweza kuongoza zingine kwa ubora.
Umeujibu kiweledi sana huo "mzigo wa ujinga" ingawa pengine ndio umeuchanganya zaidi badala ya kuuponya.
Hahahaha ameuvuruga hasa ubongo badala yakuutuliza huko aliko atakuwa anajiharishia tu saizi
 
Kichwani mwangu kunakosa vingi sana ambavyo wewe unavyo. Hilo si tatizo lako wala siyo mada iliyopo.

Au nikikosa kitu kichwani mwangu tatizo ni lako wewe?

Shule za kusomea ujinga zinafahamika haraka sana.
kawe alumni Umeona watu waliokwenda shule wanatumia hekima na busara
Ati tumeshindwa nini kuendeleza reli ya mjerumani na reli ya mchina

Niliposoma hiyo mistari tu nikajua kuna kitu unakosa kichwani kuhusu miundo mbinu ya reli

Sijaribu kukubadilisha mtazamo wako japo unaonekana dunia imekuacha mbali mno kifkra
 
Kwetu Mkuranga, kuna mitego ya panya maarufu sana. Hutengenezwa kama dema la samaki na wengine hadi leo hii huiita "dema la panya". Mitego hii ni mizuri sana lakini kila kizuri huwa na changamoto zake. Mtego huo ukitegwa hunasa panya na vinginevyo.

Tanzania kabla ya hapo, Tanganyika, tunajitawala wenyewe kwa miaka 58 sasa, toka tulipokabidhiwa nchi, sifahamu na Umoja wa Mataifa au Uingereza.

Huwa najiuliza, kwanini miaka 58 bado tunategemea hata bajeti yetu kujalizwa na nchi za nje?

Uhuru tunaojivunia ulikuwa ni
"dema la panya?

Tanzania tuna reli ya Mjerumani na tuna reli ya Mchina na sasa tunaongeza reli ya tatu, ya Mturuki. Swali, tumeshindwa nini kuziendeleza reli za Mjerumani na Mchina hadi tuanze alifu kwa kijiti na reli ya Mturuki? Jee, siyo dema hili?

Reli mpya siyo dema litakalo unasa na uchumi wetu?

Vipi? Najaribu kufikiria magari mangapi makubwa ya mizigo yatakosa kazi kwa kuundwa reli hii, najaribu kufikiria vituo vingapi vya haya magari makubwa ya mizigo vitakosa biashara kuanzia Dar hadi mpakani? Maelfu (kama si malaki) ya Watanzania watakosa ajira za moja kwa moja (direct employment) na wangapi watakosa ajira na vipato vya "indirect"? Siyo dema hili?

Ndege:
Tunafanya la maana sana kuwa na ndege zetu wenyewe lakini nalo siyo dema? Maana ni muda mchache toka tuanzishe tena kuwa na ndege zetu wenyewe, kwa muda huu mchache
tumeshashuhudia ndege hizo watu wakianza ubadhirifu hata kwenye kuzichora nembo tu! Pia tumeshuhudia zikishikwa sasa mara ya tatu na watu wenye madai yao. Siyo dema hili?

Viwanda.
Nachelea kuuliza ya viwanda kwani nafahamu mfumo wetu wa sasa wa kuwekeza kwenye viwanda ni tofauti na ule tulioshindwa kabisa kuuendesha, wa awamu ya kwanza. Ule ulikuwa mfumo wa mali za umma, sasa tunawataka wawekezaji wawekeze kwenye viwanda. Hiyo ndiyo tofauti.

Lakini jee, likija suala la kukorofishana na wawekezaji hivi viwanda havitajosa vipuli na baadhi ya mahitaji ya nje ya kuviendesha? Siyo dema hili?

Nachelea zaidi kuongelea umeme wetu mpya kwa kuyatafakari hayo hayo ya kuwa labda tunaingizwa kwenye dema huku tunajiona mahodari?

Vipi? Tunasoma kuwa dunia ya leo inajikita katika teknolojia ya kuufanya umeme uwe (localized) kwa kuanza kubuni na kuijaribu teknolojia ya kuendesha umeme wa nyumba kwa nyumba, jumba kwa jumba, kiwanda kwa kiwanda badala ya kuwa na umeme wa kizamani wa kufuliwa sehemu moja (kama tufanyavyo) na kutawanywa. Siyo dema hili?

Tafakuri yangu inanipelekea kuona kuwa siasa, uchumi, rushwa na ufisadi vyote vinaweza kutumiwa na wasuka dema kutunasa tuliokuwemo na tusiokuwemo.

Cha kufanya? Tujadili.

"Damned if you do, damned if you don't".
Jamii za kiafrika FaizaFixy
 
Attachments

  • Screenshot_20191124-175131.png
    Screenshot_20191124-175131.png
    64.2 KB · Views: 2
Asante kwa kunielewa kwahio tufike mahali tuache kuonyesheana vidole, tufike mahali tuongozwe na katiba, kanuni na sheria za nchi tukiamini kuwa Mpinzani sio mhaini na kwamba CCM si Mungu......wote tuna mapungufu yetu na sote tuna ubora wetu.

Kwa mfano, bungeni mnaweza kupitisha muswada wa kijinga kabisa ili tu kuwakomoa akina fulani, bungeni mpinzani anaweza kutoa hoja nzuri kabia lakini kwakua imetolewa na mpinzani itaonekana si lolote si chochote, tukumbuke mwisho wa siku woet tunabaki kuwa Watanzania.
Kama nilivyokuambia. Binafsi siamini kama kuna mpinzani wa kweli. Tumeona, changamoto kidogo kwa upinzani makundi kwa.makundi wakahama. Halikadhalika tuliona changamoto kidogo makundi kwa makundi wakaihama CCM, mara wamerudi.

Wanasiasa wa Tanzania achana nao, ukiwategemea maendeleo utayasikia tu. Kwani wote, narudia, wote wapo kwenye siasa kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku. Hatuna mwanasiasa "genuine" ambae yupo kwa ajili ya wengine iwe wa CCM au wa chama kingine chochote.

Wateja wakubwa wa waganga wa kienyeji ni wana siasa pia, jiulize kwanini?

Tujikite kwenye dema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom