FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,878
- 109,185
Kwetu Mkuranga, kuna mitego ya panya maarufu sana. Hutengenezwa kama dema la samaki na wengine hadi leo hii huiita "dema la panya". Mitego hii ni mizuri sana lakini kila kizuri huwa na changamoto zake. Mtego huo ukitegwa hunasa panya na vinginevyo.
Tanzania kabla ya hapo, Tanganyika, tunajitawala wenyewe kwa miaka 58 sasa, toka tulipokabidhiwa nchi, sifahamu na Umoja wa Mataifa au Uingereza.
Huwa najiuliza, kwanini miaka 58 bado tunategemea hata bajeti yetu kujalizwa na nchi za nje?
Uhuru tunaojivunia ulikuwa ni
"dema la panya?
Tanzania tuna reli ya Mjerumani na tuna reli ya Mchina na sasa tunaongeza reli ya tatu, ya Mturuki. Swali, tumeshindwa nini kuziendeleza reli za Mjerumani na Mchina hadi tuanze alifu kwa kijiti na reli ya Mturuki? Jee, siyo dema hili?
Reli mpya siyo dema litakalo unasa na uchumi wetu?
Vipi? Najaribu kufikiria magari mangapi makubwa ya mizigo yatakosa kazi kwa kuundwa reli hii, najaribu kufikiria vituo vingapi vya haya magari makubwa ya mizigo vitakosa biashara kuanzia Dar hadi mpakani? Maelfu (kama si malaki) ya Watanzania watakosa ajira za moja kwa moja (direct employment) na wangapi watakosa ajira na vipato vya "indirect"? Siyo dema hili?
Ndege:
Tunafanya la maana sana kuwa na ndege zetu wenyewe lakini nalo siyo dema? Maana ni muda mchache toka tuanzishe tena kuwa na ndege zetu wenyewe, kwa muda huu mchache
tumeshashuhudia ndege hizo watu wakianza ubadhirifu hata kwenye kuzichora nembo tu! Pia tumeshuhudia zikishikwa sasa mara ya tatu na watu wenye madai yao. Siyo dema hili?
Viwanda.
Nachelea kuuliza ya viwanda kwani nafahamu mfumo wetu wa sasa wa kuwekeza kwenye viwanda ni tofauti na ule tulioshindwa kabisa kuuendesha, wa awamu ya kwanza. Ule ulikuwa mfumo wa mali za umma, sasa tunawataka wawekezaji wawekeze kwenye viwanda. Hiyo ndiyo tofauti.
Lakini jee, likija suala la kukorofishana na wawekezaji hivi viwanda havitakosa vipuli na baadhi ya mahitaji ya nje ya kuviendesha? Siyo dema hili?
Nachelea zaidi kuongelea umeme wetu mpya kwa kuyatafakari hayo hayo ya kuwa labda tunaingizwa kwenye dema huku tunajiona mahodari?
Vipi? Tunasoma kuwa dunia ya leo inajikita katika teknolojia ya kuufanya umeme uwe (localized) kwa kuanza kubuni na kuijaribu teknolojia ya kuendesha umeme wa nyumba kwa nyumba, jumba kwa jumba, kiwanda kwa kiwanda badala ya kuwa na umeme wa kizamani wa kufuliwa sehemu moja (kama tufanyavyo) na kutawanywa. Siyo dema hili?
Tafakuri yangu inanipelekea kuona kuwa siasa, uchumi, rushwa na ufisadi vyote vinaweza kutumiwa na wasuka dema kutunasa tuliokuwemo na tusiokuwemo.
Cha kufanya? Tujadili.
"Damned if you do, damned if you don't".