Tafakuri ya FaiizaFoxy 4: Historia. Professor Rudolph T. Ware III ni Mohamed Said wa USA?

Kunautofauti mkubwa sana wa uchangiaji mada kati ya nyakati hizi na nyakati za nyuma kidogo.
Hii ni kutokana na vijana wengi kujihusisha kwa wingi kwenye mambo yasio na tija wala staha, na ndipo wanapoona kila kilichopo leo ni mrengo huo huo walioko.
Mada kama hii haikupaswa kuwa na coment mithili za chit chat, ila ujinga wetu ulio mwingi ndio unatufikisha hapa na pengine kubaya zaidi tusiko kujua.
Sio mwenyeji sana hapa jamii forum,nipo tokea 2013.
Naamini kabisa kila mtu alieko hapa ni mwenye heshima zake, sasa mtu anapomtukana mtu au kumuita kwa sifa isio njema ni heshima gani tunaonyesha?
Kama aina hii ya vijana tulioko leo ambao ndio msingi mwema wa vijana wa kesho, basi tutarajie hali ngumu sana ijayo kama hakutafanyika juhudi za lazima za kubadilisha fikra zetu leo.



Nimependezwa na hii mada pamoja na hoja zote za msingi, nami nikubali bila hiana japo simjui ipasavyo mheshimiwa Mohamed Said
Kwa kiasi kikubwa amekua mchango mkubwa sana wa historia isio fahamika.
Wengi wamehukumu udini udini, ok
Mimi ni mkristo na nimeweza kusikia historia ya ukristo hapa kwetu tokea ujio wao mpaka leo,sio yote yameelezwa mengine yamefichwa.
Lakini pia pamoja na ukristo kuwepo hapa kuna wasio wakristo pia nao wana historia yao kuhusu uwepo wao hapa.
Mimi siwezi kuhukumu historia yao sio kweli eti kwa sababu sio mmoja wao!
Mimi ninachosikia kwao ndio nasahihisha kile changu maana mimi siwezi kujisahihisha mwenyewe bila kijipendelea.

Nakupongeza mleta mada FaizaFoxy pamoja na matukano yote utukanwayo usijali ,pole.
Naamini nitapata vingi vya kujifunza iwapo nitakufuatilia na kwa lengo la kujifunza .

Video ilioambatanishwa nimeshindwa kupata yaliomo kutokana na lugha na udogo wa elimu yangu.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom