Tafakuri: Walimu wa ngazi ya cheti, na walimu wa muda mrefu kazini, ni vibaraka (puppets) wa cwt. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafakuri: Walimu wa ngazi ya cheti, na walimu wa muda mrefu kazini, ni vibaraka (puppets) wa cwt.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ZeTicha, Apr 8, 2012.

 1. Z

  ZeTicha Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka ming sasa, mambo yamekua hayaendi sawa ktk hii fani ya UALIMU, ualimu sasa umekua n kama kapu la kutupia uozo wa kila namna, dharau, dhulma na matusi, huku chama cha walimu, ambacho n mdhamana mkuu wa kutetea haki izo Akionekana hana MENO,
  harakat znahtajka kujkomboa, lakn tatzo kuu n walimu wa cheti, ni waoga mno na walimu wenye diploma wa muda mrefu wamerdhka na mshahara mkubwa..ivo wote n vbaraka wa Cwt, n kwel? Nin kfanyke? Walimu wa shahada(degree) tuunde chama che2?
  Nawasilsha
   
 2. vanmedy

  vanmedy JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 2,246
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Count me in, cwt is very disgusting
   
 3. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Unataka waalimu waende wapi wakifukuzwa?hakuna kazi ambayowatafanya tofauti na ualimu.
   
 4. Z

  Zedikaya Senior Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao hawana pa kwenda na hawafikirii popote zaid ya hapo,hata ukitaka kuwachapa vbk uktan ni ww 2,
   
 5. n

  nonga Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na walimu wa private sector? Let's b broad.
   
 6. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jamani kwa muda sasa nimekua nikisoma na kusikia walimu wengi wakilalamika juu ya chama cha walimu. Yawezekana madai yao yana msingi, hata hivyo nina maoni binafsi;
  1. Kusema walimu wenye vyeti na diploma ni vibaraka wa CWT na hawana pa kwenda, ni kuwatukana wazee wetu ambao kwakweli hata mtoa mada wamemfikisha hapo anapoona ni pa juu sana SHAHADA.
  2. Nyerere alianza safari ya ukombozi na wa nchi akiwa na hao wa elimu ya chini. Shahada zilipoongezeka kwa zama hizi na ufisadi ukaongezeka, hatuna jambo kubwa la kujivunia kwa wingi wa shahada nchini isipokua kitakwimu. Wenye shahada wameongezeka lakini ndo kwanza nchi yetu bado ina mgao wa umeme na hata maji. Shahada zimeongezeka lakini vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 bado viko juu. Tunashada nyingi lakini watoto wetu wanafeli kwa wingi usioelezeka.
  3. Walimu mkianza kugawanyika kwa kufuata elimu zenu uwezekano wa kusonga mbele ni mdogo sana maana wote mnahudumiwa na wizara zilezile. Wenye shahada ingieni kwenye hicho chama shikeni mkiongoze wenyewe, msiiende kugombea nafasi mkiwa mmeweka shahada zenu mbele haitawafaa kitu. Amini nawambieni mkijitenga na wa cheti wakasalia pekee yao chama chao kitakua na nguvu maana ni wengi na pili watajiona wamedhalilishwa na wasomi. Mtakua na maadui wawili serikali na chama cha walimu wenye cheti.
  3. Kuhusu CWT hapa nitaongea kwa uzoefu kidogo niliouona kwenye hiki chama, kuna wilaya hiki chama ovyo kabisa lakini lazima tukubali yapo maeneo walau kuna jambo unaweza kusema wanafanya kitu. Mfano nimeshuhudia CWT ikimshitaki DED kwa niaba ya mwl aliyekua amefukuzwa kazi kimakosa, nimejionea mwenyewe CWT ikiwasaidia wanachama wake kwa masuala ya kisheria, kifedha mara nyingi, na hata walimu wamepageuza kimbilio lao. Imefikia pahala walimu wanaenda kushtakiana CWT na si kwa DED.
  4. Walimu wote shikamaneni mkianza kugawanyika mambo mengi mtafanyiwa ya ajabu.
  5. Ukweli usiopingika CWT inahitaji sura mpya katika wilaya nyingi na mikoa mingi na hata taifa. Jitahidini vijana walimu muingie humo sasa, mfanye mapinduzi ya chama kiwe na sura ya kupigania haki za walimu si kama kilivyo sasa kwa sura ya jumla. Watoeni Msulwa na wengine maana ni watu wa serikali wapo kwa maslahi ya aliteyewatuma kazi na si walimu. Muda umefika kwa chama kuanza harakati za kudai mambo yanayowahusu walimu wote na si kudai madai ya hamisho na madaraja ambayo kimsingi si ya walimu wote.
  Tuendelee kujadili.
   
 7. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  wakuu
  nafikiri mtoa mada ana MAONO MAZURI SEMA KUSILISHA KWAKE KUMEONGOA ULE UZURI WOTE WA MADA,KWANI HAO ANAOWADHARAU,
  KWANZA NI WENGI MNO HIVYO WANAWEZA KWAMISHA MPANGO WAKE,
  PILI NADHANI NI MUDA MUAFAKA KWA MTOA MADA KUTUMIA ELIMU YAKE KUWAELIMISHA HAO ANAODHANI WANAKWAMISHA UFANISI HIVYO WAKIUNGANISHA NGUVU ZAO PAMOJA WATAFANIKIWA
  KINYA
   
 8. I

  Ilongailunga JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 1,132
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  CWT ni chama cha kikuwadi(comprodorial organisation) ni vema wanachama wake wakitafakari upya muundo wake, ni kweli kuwa sitawakosea heshima kusema kuwa walimu wengi wa shule za msingi na wale wa muda mrefu wako too conservative na waoga mno, vilevile CWT imehodhiwa mno na walimu wa shule za msingi na kwahivyo inashughulikia na ina uelewa mkubwa wa mambo ya shule za msingi na kutojali maslahi ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu. Nakumbuka wakati nikiwa mwalimu tulianzisha vuguvugu la kudai mambo matatu, kwanza, kubadilishwa kwa mfumo wa upatikanaji wa viongozi ili kuwa na uwiano mzuri kati ya walimu wa msingi, sekondari na vyuo, pili, walimu wa matawi yote(shule na vyuo) wahusike katika uchaguzi wa viongozi wa CWT wilaya, na, ugawaji wa rasilimali ya CWT sawa kwa makundi yote, vuguvugu hili lilipoanza kushika kasi miongoni mwa walimu wachache hasa Mkoani Arusha na baadae kigoma CWT ikajibu kwa kufuta matawi katika muundo wa CWT na muundo kuanzia wilayani ili tawi litatuma mwakilishi, hivyo hata fungu dogo lilikuwa likifika tawini nalo likawa limefutika. CWT sasa imebaki kuwachezea fool game walimu kwani mara tatu mfululizo wanaitisha mgomo kipindi cha likizo shule zikikaribia kufunguliwa wanatoa tamko la kusitisha migomo hii ni dharau kubwa kwa walimu. Sasa ni vema walimu wote wa serikali na binafsi(hasa wa sekondari na vyuo) ni vema wakatafakari kwa makini uwepo wao CWT, kwa upande wetu tunatafuta njia ya kisheria kudai mabadiliko CWT! A LUTA CONTINUA!
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mtu muoga anahitaji kuelimishwa au kubadilishwa fikra ili awe jasiri? Waalimu wa ngazi ya cheti wanatumiwa kila siku huku wakijiona na hawabadiliki.
   
 10. Z

  ZeTicha Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu hayo mawazo nimeyatoa bila kumung'unya maneno, n mara nyng wa2 hudhulumiwa haki zao kw kuhofia aidha wing wa adui wake au nguvu, blv me mabadliko yanahtajka lakn n lazma mgawanyo (separation) uwepo, n lazma tujtenge na hao....
  Msimamo:sina dharau na walimu wasio na degree, na hata ktk post yangu ilo haljionesh
   
 11. Z

  ZeTicha Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  n kwel tuna matatzo meng hapa Tz, ila n lazma tuwe na utaratbu wa kudeal na tatzo moja moja, kwanza tuanze na hil la cwt, nakir kuwa cwt inatatua matatzo meng ya walmu, lakn hlo peke ake sio tija, n sawa na kumshukuru mkolon kwa kujenga reli kutoka mwanza kuja dsm, wakat unajua alikua na lengo gani...
  N lini Cwt imetangaza mali ambazo inazo? Lini imetangaza kiac kinachopata kw mwez kutoka ktk vtega uchumi vyake?
   
 12. Z

  ZeTicha Member

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muundo wa uongozi n tatzo, pia upataj wa taarfa za chama n tatzo pia....nin kfanyke
   
Loading...