Tafakuri: Tupo tayari kununua bidhaa na kupata risiti?

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
2,165
3,655
Ni wazi mpaka sasa wengi hasa waliopata/walio na kazi Rasmi pamoja na wenye vipato vya uhakika wanafurahia sana zoezi linaloendelea la wamachinga kuondolewa kufanya biashara zao barabarani ambazo kiukweli walisaidia kwa kiasi kikubwa watu kujipatia bidhaa/vitu kwa bei nafuu zaidi.

Ok tuseme zoezi likamilike na hatimae tubaki na maduka/biashara Rasmi za dukani.

Je, tupo tayari sasa kununua vitu kwa bei ya risiti Ili kuchangia kodi ya Serikali?

Waungwana hivi vifaa vya electronic vitanunulika kweli?

Je, sisi tunaonunua bizaa Kariakoo kwa jumla na kuweka madukani kwetu,tutaweza kuendana na speed hii kweli?

Tafakuri.

Nawasilisha
 
Vifaa vya electronics nahisi itakua balaa,Ninampango wa kuingia fridge week hii ya hisense na bei yake KWA Sasa Bila reset nishaambiwa ni 830000 240liter.

Sijui inakuaje asee,Sipigi kodi ila kodi yetu BADO haijakaa mazingira rafiki kwetu hasa KWA bizaa zinazotoka nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom