eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Kwanza angalia na sikiliza vizuri hii video. Dawa ya Asubuhi.
Utaona ni jinsi gani Mhe Mwanri anatumia saikolojia ya uongozi kuteka nyoyo na hisia za anaowaongoza. Katika hili anaongea na bodaboda ambao wako kwenye ugomvi na polisi. Nitafanya tafakuri tunduizi katika mambo machache
1. Mavazi na hadhira yako
Huku akijua fikra yeye ni kiongozi na polisi wako chini yake aliamua kuvaa mavazi ambayo yanapendwa sana na makondakta pamoja na bodaboda. Pia akaamua kuvaa kofia ambayo ni nadra sana kwa viongozi na wakuu wanaweza kuvaa. Hii kofia hutumika sehemu zenye baridi lakini kwa Tanzania ni mavazi ya watu wa chini sana. Wenye kipato au wadhifa huwa hawavai za namna hiyo labda sehemu iwe na baridi sana.
Mavazi yake yanamfanya awe mmojawapo wa bodaboda ambao ndio nia yake kuwaelimisha. Bodaboda wanajisikia vizuri kumuona RC kavaa kama kondakta au Mchumia jua.
2. Hoja za kukubaliana
Anawasilisha hoja zake kama maswali ambayo anahitaji pande mbili wakubaliane, yaani polisi na bodaboda. Akiwasilisha anawauliza Bodaboda kama anachosema hakifai basi waseme huku kaweka adabulugha yakini yenye kusisimua na kuchekesha ili kumteka msikilizaji. Mhe angeweza kuweka vitisho na kuwaambia bodaboda kama hawataki atawanyoosha lakini badala yake anaongea nao kama marafiki ambao anahitaji sana wabadili tabia.
3. Mapumziko kwenye maelezo
Huku akionekana mtu mwenye unyenyekevu sana anakuwa anazipishanisha hoja zake kwa mapumziko ya vichekesho kabla hajahamia kwingine. Nakumbuka shuleni mwalimu mwenye kipindi cha muda mrefu kuna wakati anasema simameni kidogo kisha rukaruka kidogo. Ni kuamsha tuu ari ya kusikiliza na kuchakata maelezo.
4. Mifano ya kumuelewesha mtu wa kawaida
Rais Magufuli alishawahi kumwambia yule dada wa SSRA kuwa yuko "too academic" ndio maana haeleweki na wengi. Mhe Mwanri akiwa kama kiongozi wa siku nyingi anafahamu jambo hili vizuri ndio maana kila hoja yake anaisindikiza na mifano mirahisi kabisa ili walengwa ambao ni BodaBoda wakubaliane nae na wabadili mienendo. Kwenye Movie Slumdog Millionaire, yule muhusika mkuu anaonyesha jinsi gani "experience" ya matukio hueleweka. Hata biblia na vitabu vingine vya dini hutumia "parables" ili kuweka uelewa wa hadhira mezani.
5. Uongozi unaoacha alama
Kama kiongozi, Mhe Mwanri, anataka kuacha alama ya upendo na uongozi bora. Huku akijitapa kuwa bodaboda wakifuata sheria za barabarani vizuri basi ajali zitapungua kwa sababu mkoa wake ni kama TORONTO. Huku akisema ulishawahi kuona Toronto wanavunja sheria? Kimsingi anawajengea watu wake hisia kwamba ukifuata sheria basi maisha yako yanakuwa "civilized" kwa kuwa unaishi mkoa ambao ni "civilized". Kimsingi anataka kila anaemsikiliza akiondoka aende akafanye mabadiliko ya tabia zake barabarani. Lakini kuna uwezekano akitoka hapo anaenda kuwaambia polisi wakamate wanaovunja sheria wakiwa kikaoni lakini JUKWAANI ameamua kuwa mnyenyekevu ili bodaboda nao wafanye kwa unyenyekevu. Uongozi unaocha alama hujikita katika kutoa UHURU kwa watu na kuwaheshimu. Haujikiti katika majivuno na mashindano. Hulka ya binadamu au Temperament yake hutulia endapo itapepewa.
Nawasilisha wadau.