Tafakuri tunduizi: Tutafakari pamoja kama ni kweli Rose Kamiili katoa rushwa

mama rose alikuwa anahonga wapigakura ,hilo.liko wazi. hizi nyingine ni bla bla tu. huu uchaguzi chadema hawatoki. wanakalenga wamewakataa...
 
wabunge wa viti maalum chadema wamepata kwa kutoa rushwa za aina mbalimbali. bila rushwa chadema haiwezekani
 
wabunge wa viti maalum chadema wamepata kwa kutoa rushwa za aina mbalimbali. bila rushwa chadema haiwezekani

Mkuu.

Naamini unaweza kuumiza kichwa! hebu rudi usome tena namba 1, 2 na 3 kisha urudi uchangie kwa kusimamia hapo kwa hoja.
 
Hivi CHADEMA mlipomkamata yule mama DC kule Igunga akiwa kwenye kikao cha ndani na kumdhalilisha ilikuwa ni sawa lakini CCM kumkamata mbunge wenu mnaanza kulia lia!

Haya mambo ya kukamata watu mlianzisha wenyewe na sasa mchezo umewageukia.

Na hili ndilo CCM walilotakiwa kulisema kuwa tumefanya hivi kwa ajili ya kulipiza kisasi wengeweza kueleweka kidogo kuliko kuleta propaganda zao zisizo kuwa na ukweli wowope.
 
Mods:

Kwa heshima na taadhima nawaomba msiunganishe thread hii bali muiache tujadili kwa hoja na tafakuri tunduizi kwa wale ambao watakuwa tayari kuumiza vichwa vyao na kushusha nonda za uhakika

Kwanza nikiri kuwa sina uhakika kuwa Rose Kamili katoa rushwa kama alivyotuhumiwa na wana CCM kwenye tukio la jana usiku kule Kalenga, lakini kama ni kweli iliyo kweli tupu bila chembe ya shaka naomba tutafakari pamoja kwa kutumia tafakuri tunduizi kwa kujiuliza maswali kadhaa.

1. Kama CCM wana greenguard ya kuzuia rushwa kama ni kweli kama wanavyosema, ipo kwa ajili ya kuwazuia wapinzani tu? Kwa nini wasitumie greenguard hiyohiyo kumsaidia Mzee Mangula aliyewapa siku 90 viongozi wa NEC walio chaguliwa kwa rushwa wajisalimishe kwake?! Siku 90 zilisha isha kwa nini wasisaidie?! kumbuka pia jk alisha wahi kusema rushwa itaiua ccm, kwa nini wasisaide kusimamia kauli ya mwenyekiti wao ili chama kisizidi kuwa kichaka cha rushwa?

2. Kama Mama rosekamili alikuwa anagawa rushwa kwa nini wasiwaite maafisa wa Takukuru na matokeo yake walienda naye kwenye ofisi ya chama chao na sio Polisi?! Kama waliweza kwenda nae kwenye ofisi ya chama kwa nini isiwe Polisi? Kwa nini wawaite Polisi wamchukulie kwenye ofisi yao ya chama wakati walikuwa na gari waliyokuwa na uwezo wa kuikimbiza Polisi au Takukuru moja kwa moja?

3. Kama kosa liko kwa Mtoa na Mpokea rushwa kama sheria zinavyo elekeza, mbona waliokuwa wanapokea hizo rushwa hawajakamatwa na kikosi cha greenguard cha kuzuia na kupambana na rushwa kule Kalenga? Wao hawakuwa na kosa?! Dhamira ya kumkamata Rose Kamili pekee na kuwaacha wengine ni safi na haiibui mashaka hujma kwa mtu makini?!

4. Je tukio hilo lilikuwa la kupangwa au limetokea kwa bahati mbaya?! Bahati mbaya kwa maana ya kumkamata na kumpeleka ofisi za ccm nasi Polisi au kuwaita maofisa wa Takukuru waje eneo la tukio?

5. Tuna uhakika CCM huwa hawashirikiani na vyombo vya dola kukandamiza upinzani na kuwabambikiza kesi?! Kama jibu ni "HAPANA" Kwa nini mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni rais aliwahi kuwaambia CCM "...Na nyinyi acheni kuwategemea polisi kupambana na upinzani.." alikuwa ana maana gani?! Je inaweza kuwa CCM na Polisi hawakumsikia ndio tunashuhudia haya ya rose kamili?!

6. Je CCM waliomkamata Rose Kamili wanaweza kuaminika mbele ya Macho ya watu makini wanapomtuhumu Mpinzani wao kisiasa kuwa ni mtoa rushwa?! Ni dhana zipi tunaweza kuzitumia kuwa amini? Je tutawaamini?

7. Je zinaweza kuwa Propaganda za kisiasa na kuzitumia kwa kasi kwenye vyombo vya habari ili wananchi waone CCM na CHADEMA ni walewale na hivyo wananchi hawana haja wala hoja ya kufanya mabadiliko maana heri zimwi likujualo hali kuli likakwisha?!

Majibu ya maswali hayo yakikuridhisha bila chembe ya shaka changanya na zako na uanze kufungau ukurasa mpya wa kujifunza kutafakari kwa kina na mapana na marefu.

Tafakari ukiwa sober


Nionavyo mm tukio hili ni janja ya ccm kwa maslahi yao. Ni janja ya nyani(ccm) kula mahindi mabichi! Greenguard(ccm) hawana 'moral authority' ya kupambana na rushwa. Sababu ni moja tu kuwa rushwa ni 'sera' ya chama chao! Mungu ibariki CHADEMA!
 
Haiwezekani ukawa na akili nzunri halafu ukawa unatoka CHAMA FULANI na ukazungumzia rushwa kwa ubaya kila mtu anajua at least wana CHAMA FULANI WANAJUA KUWA CHAMA BILA RUSHWA HAKIENDI
KWA sababu leo hii rushwa ingekuwa ni kosa viongozi asilimia kubwa ndani ya CHAMA FULANI wangekuwa mahakamani kujibu tuhuma za rushwa
HEBU TUSEME ROSE KAMILI KATOA RUSHWA ,HII LAZIMA IWE NI AJABU KWA WATU WENGINE NA SIO KWA CHAMA FULANI
CHAMA FULANI HAWAPASWI HATA KUZUNGUMZIA RUSHWA KWA SABABU WALISHAIKUBALI
 
kosa la Rose kamili hakuvaa hijabu, otherwise pangechimbika leo na ijumaa ijayo mngetutambuwa kwenye maandamano. kwakuwa ni kafir atajijuwa na kafir mwenzake tuliyemuonea huruma na kumfutia mashtaka ya kubuni Costa Mahalu.
 
Mkuu.

usiingie kichwa kichwa! ninacho kiongelea hapa ni msingi wa kawaida kabisa unapo mkamata mtoa na mpokea rushwa! je, unampeleka ofisi kwako au unaita/kupeleka kwenye vyombo vinavyohusika? je unamkamata mtoa rushwa tu na kumuacha mpokea rushwa?
Hakuna cha kujadili hapa,

Kasome kifungu cha 16 na 14(a-h) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai Sura ya 20 utapata majibu yako.
 
Mods ningeomba msimamie weledi wenu wa kazi na msikubali kuendeshwa na matamanio ya members humu ndani.

Kama ni kweli mlijiwekea majukwaa wenyewe humu JF na mijadala yote ufanywa kwenye jukwaa lake husika. Kwanini hii mada isipelekwe kule "jukwaa la chaguzi ndogo" maana ndio mahala pake? Naomba hatua zichukuliwe.

Invisible, Moderator

Kuhusu Rose Kamili: Hapa hakuna cha tafakuri tundizi wala lisuizi, huyo mwanamama hiyo tabia ya kutoa hongo si ngeni kwake, inasemekana hata huo ubunge wa viti maalumu alitoa hongo mbalimbali, leo iwe uchaguzi wa ubunge tena wa rafiki yake?

Tuiache TAKUKURU ifanye kazi yake. CHADEMA acheni kupepesuka, shughuli ndio kwanza imeanza.
Mbona haya ndio matamanio yako?
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ndo nafasi pekee ambayo CCM wanataka kuitumia kama udhaifu wa CHADEMA kuwa hawaishi wayasemayo na hata wakishinda leo huko kalenga basi ionekane CHADEMA walihonga.Dirty minds of CCM
 
Mohamedi Mtoi

Nawewe umeanza lini kunywa gongo?????


1.Green Gurd kushindwa kuwakamata CCM wanaotoa rushwa hakuhalalishi Chadema kuachwa wafanye uhuni wao.
 
Last edited by a moderator:
mama rose alikuwa anahonga wapigakura ,hilo.liko wazi. hizi nyingine ni bla bla tu. huu uchaguzi chadema hawatoki. wanakalenga wamewakataa...

Leta Ripoti ya TAKUKURU hapa.Hizi siasa za kijinga ambazo muda sio mrefu zitakuja kuonekana sio za kweli zitakuja kuwadhalilisha.
 
Hakuna cha kujadili hapa,

Kasome kifungu cha 16 na 14(a-h) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai Sura ya 20 utapata majibu yako.

Acha kupotosha! kwa hiyo hicho kifungu ndio kinasema mpokea rushwa asikamatwe na ukimkamta mtoa rushwa unamteka na kumpeleka ofisini kwako?! weka na hicho kifungu acha porojo.
 
CCM ni vinala wa kutoa na kupokea rushwa hawawezi wakashinda pasipo kutoa rushwa hawezi wakapiga kura mpaka wauziane kwa pesa.Kura kwa CCM ni kuuziana na kununuliana.Akili za wana ccm zimevia kwa kutoa na kupokea rushwa hawana uwezo wakutambua kuwa wapo wanaopiga kura zao bila kupokea rushwa.Wanashindwa kuelewa kuwa wapo wanaoshinda bila ya kutoa hata senti yao. Wanashindwa kuelewa kuwa wananchi wamewachoka kiasi ambacho wanatumia uwezo wao binafsi na nguvu zao kuwaondoa madarakani bila ya kutegemea hongo ya mtu yeyote furaha yao ni kuing'oa CCM madarakani.Vinala wa kutoa na kupokea rushwa wamegeuka na kuwa wakamata rushwa kila wanaye muona kwa vile wamebobea kutoa na kupokea rushwa wanadhani ni mpokea rushwa na mtoa rushwa.Akili za wanaccm na damu zao zingekuwa zinachunguzwa zingikutwa kila sehemu zimeandikwa rushwa.Damu zao zikichanjwa zinajiandika rushwa rushwa rushwa.CCM rushwa rushwa rushwa rushwa kwa kuwazuga wananchi wanaita takrima.
 
Back
Top Bottom