TAFAKURI: Siku Lowasa akiamua kurudi CCM atapewa jina gani?

Dogo Lao

Member
Nov 2, 2011
94
38
Si vibaya kujiuliza. Ni kweli mimi si mtoa mada mara kwa mara katika jukwaa hili, ila ni mfuatiliaji mzuri sana wa mambo yanayoletwa humu. Nikiwa kama mwana-jf mwenye uhuru wa kufikiri ama kuwasilisha fikra zangu naomba msinihukumu kwa kuitumia nafasi hii bali kwa atakayependa kujiuliza kama mimi ninavyojiuliza basi ni ruksa tujiulize pamoja.

EL ktk siasa za Tz amekuwa na majina mengi mbali na yale yatokanayo na nyadhifa alizowahi kushika. Aliwahi kuitwa mzee wa maamuzi magumu, akaitwa fisadi, akaitwa muungwana, n.k mengine utaongezea.

Na kila jina alipewa baada ya kutokea tukio fulani. Mf. alipokuwa waziri mkuu (mtu wa maamuzi magumu), tukio la richmond (fisadi), alipohamia cdm (muungwana). sasa najiuliza ikitokea kama mwanadamu akaamua either kurudi ccm ama kwenda chama kingine atabaki na jina hili la sasa (muungwana) au tutegemee majina mengine kama waliyopewa wengine!!!!?

NOTE: Ni tafakuri tu ambayo kila mtu anauhuru wa kutoa anachokiwaza
 
"Ng'ombe aliyekatika mkia" Nina uhakika atarudi hata kabla ya Novemba 2019, subiri waanze kugusa vitega uchumi vyake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom