Tafakuri: Serikali 3 za Tume ya Warioba hazina tofauti kimantiki na iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,912
2,000
Kama utakuwa umefatilia kwa makini juu ya iliyokuwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, utaona havina tofauti yoyote na mapendendekezo ya tume ya jaji Warioba juu ya muundo wa Serikali tatu (3) nchini Tanzania.

Iliyokuwa Halmshauri ya jiji la Dar es Salaam kimsingi haikuwa na eneo la kiutawala, ilikuwa inaelea tu au unaweza kuiita ilikuwa ya kufikirika au yakusadikika.

Halmshauri ya jiji ilikuwa inatengewa baheti lakini haikuwa na vyanzo vya mapato, ukiangalia ilikuwa inapokonya vyanzo vya mapato toka vyanzo vya manispaa zake, sometime miradi ya manispaa ilikuwa ina bajeti kotekote yaani manispaa husika imetenga bajeti yake na pia jiji lina bajeti ya mradi uouo unatekelezwa na manispaa.

Ili kufika hadhi ya kuwa jiji lazima kuwe ngazi za kufikia huko, huwa tunaanza na Mji=> Manispaa=> Jiji

Sasa sijui aliyokaipa hadhi ya jiji Dar es Salaam aliangalia nini mpaka kujumuisha manispaa zote 3 kuwa sehem moja.

Mapekezo ya Jaji Warioba juu ya Serikali 3 yasingeibua mgogoro wa kikatiba juu ya vyanzo vya mapato?

Hili ndo swali la msingi tulilopasea kujiuliza, maana serikali zote 2 zingekuwa zinaichangia serikali kuu ambayo haina eneo la kiutawala wala halina miradi yake specific zaidi kujitwalia miradi ya washirika wake wa bara na visiwani.

Karibuni
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,818
2,000
Umeelezea vizuri sana kuliko hata Rais alivyoelezea sababu za kuivunja Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam. Rais amefanya maamuzi kwa kuvutia upande fulani.

Tatizo kubwa, watawala wanajua vizuri sana kwamba mapendekezo ya Jaji Warioba ni ya msingi mkubwa kwa faida na ustawi wa taifa letu, ila kwakua roho zao zina ubinafsi wa kushika dola milele, solution wanayoiona ni kutekeleza baadhi ya mapendekezo ya Jaji Warioba kwa chini chini bila kubadilisha "SHERIA NA KATIBA", ili wao wachukue point kana kwamba ni mawazo na fikra zao. Hii ni kumkosea heshima yule mzee aliopoteza muda na jasho lake kulifanyia kazi taifa.

Kila kitu kinachofanyika na mabadiliko yanayofanyika ni "MAWAZO NA JUHUDI ZA JAJI WARIOBA NA TUME YAKE", watanzania wanatengenezewa sinema za kusifia awamu hii na kutengeneza "HISTORIA YA KIGUGUMIZI".

NB: Historia hutengenezwa na mshindi wa vita, hata kama mshindi amepigania udhalimu, na alieshindwa alipigania haki. Mwisho wa siku mshindi huandika historia hupotosha na kuhalalisha ushirika wake katika hio vita na kumchafua aliemshinda.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,207
2,000
Hiyo hoja wapelekee Polepole, Kabudi, na makada wengine walioandaa rasimu ile ya Katiba Mpya na kuitetea kwa nguvu zote leo hii wanajifanya hawaitambui! Kwa unafiki hakunaga kama CCM.
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,342
2,000
Kwa serikali Tatu kuwepo kwa hiyo layer ya Tatu kunafaida maana kunaondoa malalamiko mengi.

Sasa usifananishe kuunganisha nchi na kutenganisha majiji ya nchi moja.

Haijaleta mantiki.
Naomba kutofautiana
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
42,675
2,000
Kwa serikali Tatu kuwepo kwa hiyo layer ya Tatu kunafaida maana kunaondoa malalamiko mengi.

Sasa usifananishe kuunganisha nchi na kutenganisha majiji ya nchi moja.

Haijaleta mantiki.
Naomba kutofautiana
Huyo ni zwazwa, kwanza jiji siyo serikali ni sehemu ya serikali za mitaa(TAMISEMI) ambayo ipo chini ya serikali kuu
 

King klax

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
3,316
2,000
Aya,,mheshimiwa,, ndiyo unatufundisha inamaana walikuwa wapuuzi walotaka kuanzisha serikali 3???
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,891
2,000
Ukitaka kuelewa hii kitu kwa urahisi ni kama ifuatavyo:

1. Ilala ndio jiji kwa sasa hivyo mapato na matumizi ya Ilala yanakua ya jiji.

2. Halmashauri nyinginezo, Kinondoni, temeke, Ubungo, Kigamboni zitajitegemea 100.

Hivyo gharama kwa hizi manispaa nyingine hazitakuwepo.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,199
2,000
Acheni kututoa kwenye mstari. Tunahitaji Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, ili mambo yote Nchini yaende sawa.
 

Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,486
2,000
Kwa serikali Tatu kuwepo kwa hiyo layer ya Tatu kunafaida maana kunaondoa malalamiko mengi.

Sasa usifananishe kuunganisha nchi na kutenganisha majiji ya nchi moja.

Haijaleta mantiki.
Naomba kutofautiana
Ni uelewa tu. Tunapaswa kujifunza kinachoendelea kwa majiji mengine duniani-
".....sio lazima kwa taasisi kuwa na eneo lake la kijiografia ambalo ni la kwake pekee- Majukumu mengine yanavuka mipaka kwa mfano huduma za barabara, fire, polisi n.k. Kuna manufaa mengi kiuchumi huduma na mipango ikawa inaratibiwa na mamlaka moja! Tusiwaonee jere wale wanaozishika nafasi za kiutawala bali tuangalie ule uratibu wa shughuli za jiji! Ingekuwa kama tunavyojielekeza, amini usiamini tusingekuwa na Majiji Makuu (Metropolitan Cities) duniani- Angalia London, Kuala Lumpur, Johannesburg!
 

Attachments

  • File size
    186.8 KB
    Views
    5

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom